Makapuku Forum

Makapuku Forum

Matokeo ya vipimo vinavyoonesha asili ya Mtu kupitia tovuti ya ancestry.com yameonesha kuwa Baba Mzazi wa Rapper Drake champagnepapi ana asili ya Nigeria kwa asilimia 30 ambapo asilimia nyingine zilizobaki zimeonesha kuwa ana asili ya Cameroon, Congo kwa asilimia 28, Ivory Coast na Ghana asilimia 11.

Matokeo ya Baba yake yamemfanya Drake ahoji kama yeye ni Mnaigeria japo kwenye orodha ya Nchi zilizotokea kwenye matokeo hayo zimemuonesha pia Mzee huyo ana asili ya Scotland, Mali, Benin na Togo pamoja na Ujerumani.

Drake aliandika yafuatayo kwenye Insta story yake “Haya ni majibu ya Baba yangu... Je, hii inamaanisha hatimaye mimi ni Mwanaume kutokea Nigeria?”
Screenshot_20230509_043451.jpg
Screenshot_20230509_043520.jpg
 
Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mbunge wa zamani wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, Stephen Wasira amesema hakuna mgogoro wowote wa kifamilia kuhusu maziko ya mwanasiasa huyo.

Mkono alifariki Aprili 18, 2023 huko Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu na hadi sasa mwili haujawasili nchini, jambo ambalo limekuwa likiibua maneno kwamba kuna mgogoro wa kifamilia kuhusu maziko ya mwanasiasa huyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wasira iliyotolewa leo Mei 8, 2023, amesema hakuna mgogoro wowote katika familia hiyo na kwamba wamekubaliana azikwe nyumbani kwake, Kigori, Busegwe.

“Kwa sasa taratibu za usafirishaji mwili kutoka Marekani zinaendelea vizuri kwa kushirikisha familia ya Wakili Mkono na Ubalozi wa Tanzania nchini jijini Washington, Marekani.

“Tunauhakikishia umma kwamba hakuna mgogoro wowote wa kifamilia juu ya suala hili. Familia imepanga mwili wa Wakili Mkono upumzishwe nyumbani kwake Kigori, Busegwe,” amesema Wasira katika taarifa yake.
Screenshot_20230509_043702.jpg
 
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amezungumza kwa masikitiko kuhusiana na hali wanayokumbana nayo wachezaji na viongozi wa timu hiyo baada ya kushindwa kupambania taji lolote msimu huu. Ahmed ameandika;

“Mara kadhaa utasikia shabiki anasema sisi tunaumia kuliko wachezaji au viongozi. Ndugu zangu ili mradi sote tuna damu ya Simba basi wote tunapitia maumivu, kinachotokea ni tofauti ya mtu na mtu kuhimili maumivu,”

“Ndiyo maana wengine wanalia, wengine wanazimia, wengine wanashindwa kula, wengine wanakasirika yote ni maumivu. Leo tumezomewa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaaam hali ambayo inawaumiza zaidi wachezaji, hakuna mchezaji anayetaka kufungwa makusudi ili azomewe kuzomewa ni kitendo cha aibu sana.

“Katika nyakati hizi ni vema kila mmojaakaheshimu maumivu ya mwenzie kwani hakuna anaejua mwenzie anaumia kiasi gani. Tufanye yote lakini tuwaache viongozi wamalize kuugulia baada ya hapo waje watutengenezee timu madhubuti kwa ajili ya msimu ujao. Hakuna mtu anaekubali kuharibikiwa katika kazi yake, viongozi wetu wanapambana usiku na mchana kuhakikisha sisi mashabiki tunapata furaha.

“Tuwaunge mkono kwenye kipindi hiki kigumu kwao kwani na wao wanaumia kama sisi na hawana mahala pa kupeleka lawama zao, lakini pia pamoja na kuumia kwao wanatakiwa warudi kazini kututengenezea Simba imara.”
Screenshot_20230509_043805.jpg
 
Wavuvi watatu wamefariki dunia wilayani Geita na wengine watatu kunusirika kifo baada ya mtumbi waliokuwa wamepanda kujaa maji kisha kuzama ndani ya Ziwa Victoria.

Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Geita, Cornel Magembe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wavuvi hao walizama ziwani jana Mei 07,2023 saa 12 jioni baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kujaa maji na kuzama.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nungwe leo Mei 8,2023 mara baada ya miili mitatu ya wavuvi hao kuopolewa, mkuu huyo wa wilaya amesema tukio hilo linaumiza na wavuvi wanapaswa kulitumia kama fundisho kabla ya kuingia ziwani.

“Tunapoingia majini tutambue ni mahali hatari na ndio maana mnapaswa muwe mnavaa ‘life jacket’ pamoja na maboya jambo la kusikitisha mtumbwi huu uliozama taarifa nilizopewa ulikuwa na vifaa vya kujikinga kama maboya na ‘lifejacket’ lakini hawa waliingia bila kuvaa na matokeo yake ndio haya mnayoyaona.” amesema Magembe
Screenshot_20230509_043856.jpg
 
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameshinda tuzo wa mchezaji bora wa mwezi Aprili Ligi Kuu Bara akiwafunika Jean Baleke wa Simba na Ayubu Lyanga wa Azam FC.

Naye Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohammed, amechaguliwa kocha bora wa mwezi huo.
Screenshot_20230509_044209.jpg
 
Mahakama nchini Kenya imeagiza kuzuiliwa kwa akaunti 15 za benki zinazomilikiwa na Mchungaji Ezekiel Odero kwa siku 30 kutokana na shutuma za utakatishaji fedha.

Hii inafuatia ombi lililowasilishwa na Ofisi ya Mkurungenzi Mkuu wa Upelelezi wa Mashitaka (DCI) kutaka akaunti zote zizuiliwe wakati uchunguzi ukiendelea.

Katika waraka uliowasilishwa mahakamani, DCI, imedai mchungaji huyo wa Kanisa la New Life Prayer Centre anashukiwa kwa utakatishaji wa pesa kutokana na uhusiano na mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International ambaye anachunguzwa kwa madai ya kuwalaghai wafuasi wa kanisa lake kufunga hadi kufa ili kukutana na Yesu.

Wapelelezi wameiambia mahakama kuwa akaunti za benki za mchungaji huyo zimekuwa zikipokea kiasi kikubwa sana cha pesa ambazo pesa zake zinashukiwa kuwa haramu zilizotoka kwa wahanga ambao wanadaiwa kulaghaiwa kuuza mali zao na kumpatia mchungani Mackenzie.
Screenshot_20230509_044339.jpg
 
Kiongozi wa dhehebu la New Jerusalem mjini Bungoma nchini Kenya maarufu, 'Yesu wa Tongaren,' amelisihi Jeshi la Polisi kutomkamata akidai hafanyi chochote isipokuwa kuhubiri injili ya kweli.

Kamanda wa Polisi wa Bungoma, Francis Kooli amesema wamemwita kumhoji kiongozi huyo ili kubaini iwapo njia za mafundisho yake ziko ndani ya mipaka ya sheria ili kuwalinda wananchi.
Screenshot_20230509_044454.jpg
 
Mechi ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na Marumo Gallants itapigwa Jumatano Mei 10 saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar na marudio yatakuwa Mei 17 nchini Afrika Kusini saa 1:00 usiku.

Screenshot_20230509_044627.jpg
 
Nyota wa PSG, Lionel Messi leo Jumatatu Mei 8 amefanya mazoezi peke yake leo ikiwa ni wiki moja tangu uongozi utangaze kumsimamisha kutokana na kukiuka utaratibu wa kusafiri kwenda Saudi Arabia bila ruhusa.

Messi amefanya mazoezi peke yake huku wenzake wakipewa mapumziko baada ya ushindi wa jana dhidi ya Lorient.

Adhabu yake ya wiki mbili inadaiwa imepunguzwa baada ya kuomba msamaha kwa umma Ijumaa iliyopita.
Screenshot_20230509_044714.jpg
 
KIPA wa Rivers United ya nchini Nigeria, Victor Sochima ameweka wazi malengo yake msimu ujao ni kucheza timu kubwa hapa Tanzania huku akitaja miongoni mwao zinazomvutia ni matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Nigeria, Sochima alisema timu nyingi zimefurahishwa na uwezo wake hivyo zilimfuata kuzungumza naye ingawa kwa sasa akili yake ameiwekeza kwa ajili ya kuhakikisha msimu huu unaisha.

"Siwezi kuweka wazi kwenye kila kitu kinachoendelea lakini itoshe kusema ni kweli nimefuatwa na baadhi ya timu ikiwemo Yanga kwa sababu baada ya mechi yetu kuisha nilifuatwa na kocha wao, Nasreddine Nabi," alisema.

Sochima aliongeza mbali na Yanga ila timu nyingine ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji saini yake ni Azam ambayo kwake binafsi anatamani kuichezea kwani miundombinu iliyonayo inamshawishi tofauti na kwingine.

"Pale Azam kuna rafiki yangu mkubwa anaitwa, Isah (Ndala) ni mchezaji mzuri ambaye nimekuwa naye kwa ukaribu hivyo nitafurahia kama itatokea siku moja tutacheza wote pamoja ingawa kwa sasa dili bado halijakamilika."
Screenshot_20230509_045407.jpg
 
KOCHA NASREDDINE NABI:
.
“Tunatakiwa kuwa makini na huu mchezo wa nyumbani, watu wanasema tunatakiwa kushinda mabao mengi, wako sahihi, kwangu mimi ni tofauti kidogo tunachotakiwa ni kuwa makini tusiruhusu bao hapa kwetu lakini ushindi wowote utatupa akili kubwa kule kwao.
.
“Tunakwenda kucheza na timu ambayo imekuwa ikitafuta njia nzuri ya kushinda kwao kuanzia ugenini, tumeona kosa ambalo Pyramids walilifanya kwao na matokeo yake wakaadhibiwa ugenini, tunacheza na timu isiyotabirika na wanaocheza kwa nidhamu kubwaa.
.
“Nimewaambia wachezaji wangu kama kuna mchezo tunatakiwa kuonyesha ukomavu wa nidhamu ya mchezo ni huu wa nyumbani, lakini ushindi wowote utatusaidia uwe wa bao moja au zaidi kitu bora kwetu ni kuwanyima njia ya kuanzia kwao.”
Screenshot_20230509_045857.jpg
 
MO MABAO
100—MOHAMED Salah amekuwa mchezaji wa kwanza katika Historia ya klabu ya Liverpool kufunga katika mechi tisa mfululizo za kwenye uwanja wa nyumbani katika michuano yote, huku pia bao lake la juzi dhidi ya Brentford lilikuwa bao lake la 100 kuifungia Liverpool Anfield
Screenshot_20230509_050113.jpg
 
Farhan Jr

KUFUNGWA NI MPIRA, LAKINI SABABU NI ZAIDI YA MPIRA.

FOOTBALL ni mchezo wa wazi sana, Coach Robertinho hana cha kulaumiwa na hata wachezaji hawana cha kulaumiwa haswa wa kikosi cha kwanza, wametumika sana wengine miaka mitatu sasa na michuano zaidi ya mitatu! Matokeo yake uchovu mkubwa sana.

Kocha anatamani sana kurotate kikosi ila bench halimpi nafasi hiyo! Bench lina Moses Phiri, Sakho, Banda ambao ndio wa daraja la juu! Na hakuna wengine, Mchezaji anayekaribiana na Chama bench, hakuna anayemkaribia Kapombe bench, hakuna anayemkaribia Inonga ama Saido bench! Hakuwa na namna.

Msimu umeisha kikatili sana, msimu wa pili mfululizo bila Mataji ya ndani kuanzia Ngao, Ligi Kuu na FA! Msimu mwingine tena wa kuondoka Kapa! Maana yake ni nini? Lazima kurudi kwenye drawing board na kuanza upya kuunda timu, haikwepeki, tayari timu imefikia mwisho na haiwezi kuvuka tena nje ya hapo.

TAJIRI MO kubali sasa unapaswa kuunda upya timu kuanzia Ofisini, muundo wa timu! Mifumo ya mishahara mpaka bonus! Football imefikia eneo ambalo inahitaji sana reinforcement lakini pia kukusanya nguvu ya kweli na MAONO mapya, hakuna namna.

Zidane sababu kubwa ya kuondoka Real Madrid alisema ameshinda kila kitu na kikosi hicho hivyo haoni kama wanaweza kutumana au kuwa na nguvu ya kuvuka pengine, hivyo timu iundwe upya, sauti mpya na uelekeo mpya.

Dark day in Simba Sports club history lakini the Lion has to rise again! The Lion has to wake up! Lakini mpaka kurejea drawing board na kupata njia mpya, bado tupo kwenye project ya Magori na Senzo ambayo inaishia ishia sasa, hatujaunda kitu kipya na Barbra ndio alikuwa anaimalizia kwenye zama za mwisho.

Downfall hii ni kwakuwa glory days zimeisha na project mpya haikuandaliwa, tulikuwa timu ya Media zaidi kuliko kwa ground, tukajisahau.

Kufungwa ni Football, lakini kwanini tumefungwa!? Kwanini misimu miwili bila kikombe?? Hapo ndio swali pekee, kufungwa na Azam wala sio issue!

Screenshot_20230509_050257.jpg
 
Kama kweli tunampenda Feisal Salum basi kwasasa walipaswa kuwa wameshafika FIFA kwa ajili ya hili sakata lake dhidi ya Yanga, kwakuwa CAS ni mfumo wa kimahakama changamoto yake ni MUDA na GHARAMA za kesi, hivyo wanaweza kwenda FIFA.

Wengine tunaoonekana hatumpendi Feisal ila kiuhalisia sisi tunampenda sana na tunahitaji sana Maestro arejee uwanjani kuendelea na soka lake! Jana nilipata wasaa wa kuongea na Wanasheria kadhaa na watu wa mpira.

Ibara ya 54 ya FIFA inasema kitu kuhusu Football Tribunal ambapo migogoro kama hii ina maeneo yake na utatuzi wake! Football Tribunal ina chemba tatu nazo ni Dispute Resolution Chamber, Player Status Chamber na Agents Chamber! Hapo Feisal angeenda tu kwenye Dispute Resolution Chamber (DRC).

Wanasheria wake wangefile suala lake (ground) kisha wangeomba nafasi kwa FIFA wamruhusu Kijana aendelee kucheza mpira kwenye timu yoyote wakati suala lake linaendelea kusikilizwa kwakuwa ni miezi mitano sasa yupo nje.

Nimepata mfano wa kesi kama ya Feisal! Ambayo imepishana kwenye vitu vidogo tu! Kwenye suala la Feisal ni rahisi sana kwakuwa maswali yangekuwa machache sana ndio maana hata Mwanasheria wake alipewa dakika 10 tu za maelezo.

FIFA kupitia DRC wangepitia vitu vichache sana kama ifuatavyo!

Mchezaji ana mkataba na Yanga? NDIO! Amevunja mkataba wake? NDIO! Sababu za kuvunja mkataba, ni just cause ama without just cause? Jibu ni Without Just cause (bila sababu maalum)! Amevunja muda gani? Wakati msimu unaendelea! HAPA NDIPO KUNA KOSA.

DRC wangeendelea! Ametumikia mkataba wake kwa muda gani? Amevuka nusu ya mkataba! Maana yake yupo kipindi gani? Yupo Unprotected period (ambapo) atapaswa kulipa faini bila adhabu ya kufungiwa.

DRC wangekuja kutazama tena kwenye malipo ya mkataba! Unilateral termination inasemaje? Anapaswa kulipa Million 100 na mishahara ya miezi mitatu! Je amebakiza muda gani kwenye mkataba? Inapigwa hesabu kisha inatajwa faini ya Kijana kulipa.

Mpeni ushauri sahihi Kijana, TAFADHALINI, wakati Feisal amekubali kugeuzwa content anapaswa atambue hatua sahihi za kupita! Yanga wametaka mkamalizane kwakuwa ndicho FIFA wataenda kukifanya hicho hicho, chagua busara usipoteze muda.
Screenshot_20230509_050418.jpg
 
Shaffih Dauda

Kocha aliyepita wa Manchester United Ralf Rangnick alisema wazi ili United ibadilike inahitaji wachezaji saba mpaka kumi wapya ili timu hiyo ifanye vyema.

Mabadiliko ni makubwa yanahitajika OT, wachezaji wengi mno wa kawaida ila wanafichwa na kelele za Harry Maguire pamoja na DDG ila the real agenda ni kuwa wachezaji wengi ni average.
Screenshot_20230509_050640.jpg
 
Shaffih Dauda

Wakati Mashabiki wa Manchester United hawataki David De Gea asalie Old Trafford, Kocha Erik Ten Haag amethibitisha kuwa wanamhitaji sana DDG na wapo kwenye hatua za mwisho za Kipa huyo kusaini kandarasi mpya OT.

Glazers wanabaki ambao ni Wamiliki na DDG nae anabaki kama Golikipa
Screenshot_20230509_050758.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom