Makapuku Forum

Makapuku Forum

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa kuanzia sasa Covid-19 si tena janga la dharura kimataifa kutokana na hatua kubwa iliyopigwa tangu ugonjwa huo kugunduliwa Wuhan, China Desemba 2019.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangaza taarifa hiyo Ijumaa Mei 5, 2023 na kueleza kwamba shirika hilo limejifunza mengi kuhusu namna ya kukabiliana na majanga ya afya.

“Alhamisi Kamati ya Dharura ya Janga la Covid-19 ilikutana kwa mara yake ya 15 na ikanipendekezea kwamba nitangazia umma wote wa ulimwengu kwamba Covid-19 si tena janga la dharura kimataifa.

Nimekubali ushauri huo. Kwa matumaini makubwa ninatangaza kwamba Covid-19 si tena suala la dharura kote ulimwenguni,” amesema Ghebreyesus.
Screenshot_20230507_073855.jpg
 
Mkazi wa kijiji cha Kibitilwa kata ya Ilula wilayani Kwimba mkoani Mwanza, Marko Samwel (32) amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando baada ya kujikata na kuziondoa sehemu zake za siri kwa kutumia kisu.

Samwel anadaiwa kujifanyia kitendo hicho cha kikatili Mei 3 mwaka huu Saa 7 usiku baada ya kwa madai kuwa amechoka kuuguza maradhi yanayomsumbua (yamehifadhiwa) kwa zaidi ya miaka mitano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza amesema hayo leo Mei 6, 2023 alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.

View attachment 2612818
😅😅😅😅😅 Hayawani kweli huyo.. ngoja afe
 
KARIAKOO DERBY KUNA MBRAZIL MSIMU UJAO

Wamejaa wanawake wa kinyaturu, ila niamini mimi katikati ya nyumba za tembe na vibeyu inueni macho yenu kisha tazameni juu ya nyuzi 180° kwenye nusu duara uwanjani!! Look on that beautiful leggs, and read the truth in his fair page. Hapo masela wa Banda Umiza tunapaita shimoni, basi hio miguu ya kibrazil iliyopiga goti ndio inavutia watalii wengi Singida. Ngoja nikuweke wazi, vichaa wa ghetto tumechagua CCM Riti Stadium hatutaki tena maandazi

Ule wa utamu wa sekunde chache katikati ya mapaja ya mrembo, huku Banda Umiza tunaupata dakika 90 nyuma ya runinga!! Kwanini nisitabasamu wakati zinapigwa pasi pasi na papara, zinapigwa Freekicks kama Paul Dybala, Volleys na Outer sio masikhara, Your Smile yet more our smile, njoo tupate mkate mtakatifu wa Soka

Ni fundi haswa anayetuonyesha tofauti ya Wauza Matango kutoka Brazil na Wachezaji wa mpira wa kibrazil kutoka ardhi ya Mfalme Pele mpaka maskani kwa Mwalimu Nyerere, iweke pembeni atapita nayo, mpe mbaya atakupa nzuri, tangulia tu utaikuta, Simple sana kwake!! Wale mashabiki vichaa wa Athletic MG, River na Jacobienence walikihusudu sana kipaji halisi cha soka

Juzi wakati anaenda kusalimia benchi la Ufundi la Wananchi.....
Screenshot_20230507_074409.jpg
 
KOMBE LILEE LINANUKIA !!
.
FT: MAN CITY 2–1 LEEDS UTD
19’—️ Gundogan
27’—️ Gundogan
85’—️ Rodrygo
.
Mbio za Ubingwa EPL
1. Man City — (34)— 82pts
2. Arsenal — (34) — 78pt
.
Screenshot_20230507_074730.jpg
 
CAF KUHUSU VIP NA VVIP KWA MKAPA
.
Kamati ya CAF Super League wamesema wanataka Uwanja wa Mkapa ufungwe viti maalum kwa ajili ya mashabiki au viongozi wanaokaa kwenye eneo hili na hawataki viti vya kuwekwa na kutolewa kama ambavyo inafanyika kwenye baadhi ya michezo kwa sasa.
.
Wanasema viti hivyo vinatakiwa kuwa na umbali ambao hauwezi kumsumbua mtu kupita, lakini lazima viwe kiwango cha juu chenye hadhi ya eneo lenyewe.
Screenshot_20230507_074830.jpg
 
CAF YATAKA OFISI YA MADAKTARI KWA MKAPA
.
Hii ni ofisi maalumu ambayo inatakiwa kuwepo kwenye Uwanja wa Mkapa na taarifa hiyo inasema iliyopo haina viwango vinavyotakiwa na Caf. Hii inaelezwa itakuwa maalumu kwa ajili ya kuwapa huduma ya kwanza wachezaji pamoja na waamuzi.
.
Imesema ofisi hiyo inatakiwa kuwa na; Meza moja, vifaa maalum kwa ajili ya matibabu ya dharura vifaa kwa ajili ya upasuaji mdogo, vifaa kwa ajili ya kupima upumuaji, vitanda, sindano za dharura na dawa, mashine maalum kwa ajili ya vipimo vya moyo, vipimo kwa ajili ya presha, vipimo vya kupima sukari mwilini pamoja na vingine vingi. [ image credit eliabennet ]
Screenshot_20230507_074933.jpg
 
“Naomba msamaha kwa klabu na Wachezaji wenzangu lakini nipo tayari kwa hatua zozote ambazo klabu zitachukua dhidi yangu” Mchezaji bora wa muda wote duniani, Lionel Messi.

GOAT kapewa adhabu ya wiki mbili, GOAT kaomba radhi halafu GOAT karejesha tena mpira kwa klabu juu ya hatua zozote ambazo wataamua dhidi yake.

GOAT hajatafuta huruma kwa Mabillion ya Mashabiki duniani, hajatumia uhusiano wake mzuri na FIFA kujitakasa wala hajataka mambo ya chama cha soka, wala suala la Wanasheria ila yeye ameipigia goti klabu yake.

Tunakumbusha mastori kuhusu Lionel Messi ambaye mkataba wake umesalia mwezi mmoja tu

Screenshot_20230507_075114.jpg
 
Farhan Jr

LIONEL MESSI, Mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona na Argentina, Ballon dor saba kabatini, mataji ya kila aina ikiwemo World Cup, Nahodha wa zamani wa Barcelona na sasa timu ya taifa Argentina! AMEOMBA RADHI KWA KLABU YAKE PSG BAADA YA KUFANYA KOSA.

Rudia mstari huo! Ndio ameomba radhi licha ya kuwa ni Mchezaji bora wa muda wote moja wapo kwenye watatu yeye hakosekani ila ameomba radhi tena kwa video.

Rudia rudia rudia! Licha ya kuwa amebakiza muda mchache PSG na hatoongeza mkataba, licha ya kwamba zimesalia mechi chache sana ila amesema anataka kucheza hizo mechi na kumaliza mkataba wake.

Namzungumzia GOAT Messi hapa ambaye mpira haumdai chochote kile ila yeye ameamua kuonesha nidhamu ya hali ya juu sana, kwa kuomba msamaha ule, ile ni last point of defamation lakini Messi ameamua kusimama na weledi huo mkubwa.

Alikuwa na uwezo tu wa kukaa kimya baada ya PSG kumsimamisha, lakini anawaza yeye kama mfano kwa watoto wengi lakini anawaza yeye kama Balozi wa Makampuni mengi hii haimlipi kukiwa na mvutano na taasisi yake.

Hivi ndivyo Washauri husimama na kuhakikisha brand inasimama, Messi wakala wake ni Baba yake Mzazi Jorge, busara kubwa sana kutoka kwa Mshua na watu wake wa karibu.

Kama Lionel Messi anaelewa thamani na ukubwa wa klabu dhidi yake, wewe Msomaji umeelewa nini?
Screenshot_20230507_075114.jpg
 
Farhan Jr

Tufanye YANGA hawajui sheria, tufanye TFF kupitia Kamati yake hawajui sheria lakini kwenye kutojua kwako chochote wamefanya kitu kimoja cha busara sana ambapo Feisal Salum anaweza kuchagua njia ipi sahihi.

YANGA ambao hawajui sheria wamesema Kijana anaweza kufika klabuni wakamalizana bila shida yoyote ile kwakuwa wao wanataka hilo pia litimie, okay tufanye hili Feisal halitaki.

TFF wao kupitia kamati wametoa nakala za hukumu zao zote, hivyo Feisal Salum kwakuwa anaamini yupo sahihi anaweza kubeba nakala yake na kuelekea CAS, akapata haki yake.

TFF na YANGA hawajui sheria kama inavyoaminika ama sio? Basi kuna CAS wanafahamu zaidi, kwanini hii hatua haipigwi na mwanzo ilionekana ndio suluhisho?

Mwanzo wakati wa kesi ilitajwa sana CAS, ghafla nakala za hukumu zimetolewa CAS haitajwi tena! Hapa napata shaka sana hapa! Nafikiri tumshauri Kijana aende CAS ili haki hiyo ipatikane ama sio?

Ili Kiungo asipoteze muda wake kukaa tu ni vyema aende huko iishe haraka na maisha yaendelee kama kwenda Yanga haiwezekani.

Au ninyi mnaonaje Ndugu zangu!
Screenshot_20230507_075312.jpg
 
Farhan Jr

TAJIRI MO, pale pale ulipoanza na uteuzi wa CEO Barbra kutoka Colombia basi ulipaswa kuendelea kushikilia vision ile ya kimapinduzi kwenye soka, Matajiri wenzako wengi sana wamepita hiyo njia wamefanikiwa.

Kabwela Mimi kutoka Morogoro naweza nisiwe na maana sana ila acha nikupe mifano! Wakati Sheikh Mansour achana na Kaka wa Tandale bali Mansour mwenyewe wa Man City alipoinunua timu alianza na ‘Wakongwe’ kisha baadae akaibadili City mazima.

Alijua anahitaji Watu wa mpira ila dunia ya kisasa ilitaka zaidi vision na mission! Akaenda Barcelona akabeba Ferran Soriano na Xhiki Berigistein, City ile pale na ndoo za kutosha! Aliacha kitu mazoea.

TAJIRI MO, hata Roman Abramovich pale Chelsea alianza na hao Watu wa mpira ikawa timu ya kutumia sana ili ipate mafanikio ila baadae akafanya kama wewe! Akamchukua Mtu wake wa karibu Marina na kumpa timu, the rest is history! Kuna usela aliumaliza hasa usajili na sasa chama lilifika pakubwa.

Tajiri sisemi kuwa ukatae Wanao, mimi sijui mlipotoka ila kila kitu na muda wake, mfumo na njaa zake! Marina hakuaminika ila Cobham ilizalisha sana, Chelsea ilifanya sana biashara na taji la Ulaya wakabeba, tazama kuna kitu cha kujifunza.

TAJIRI MO kila siku unalia watu wanakupiga pesa za usajili, lakini mwisho wa siku? Majibu ni mfumo, kama ambavyo Swahiba wako mwingine GSM kutoka Salamander, ameweka Mtu wake pale Rais wa Yanga na kila kitu wapo front wenyewe, hakuna anayetaka utani kwenye biashara yake.

Sijui naeleweka Tajiri? Leo hii unasikia stori za 10% Jangwani? Leo hii unaona aina ya wachezaji na ubora wao? Wameboresha mfumo na kupunguza watu wengi sana, sasa wana sura nyingi za vijana mpya na ndoto mpya, njaa kali ya underground mithili ya Njombe Mji ama Majimaji.

Tajiri sina mengi ila kinachomtesa PSG kuna namna pia kinakutesa, mfumo mfumo mfumo! Sura zile zile kila siku nadhani ipo haja ya njaa kali mpya ikufikishe sehemu kama ambavyo ulianza kwa Barbra, ndio njia ile.

Tajiri nenda kawacheck Barcelona wanateseka na klabu ina madeni kwakuwa wanaishi kimazoea, sura zile zile zinapokezana tu! Kamtazame Madrid anavyonawiri kwakuwa Perez nyuma yake ni damu changa zenye mtazamo mpya na njaa kali mithili ya Brighton.
Screenshot_20230507_074830.jpg
 
Mtwara | Kocha Msaidizi wa Azam FC Kali Ongala amsema, timu yao ilipata fursa ya kucheza mechi mbili za kirafiki ili kuwaweka tayari wachezaji kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Simba.

“Tumecheza mechi mbili za kirafiki ambazo hazihusishi mashabiki [behind closed doors] kwa ajili ya kuwapa wachezaji utayari wa mechi.”

“Tupo kwenye kipindi ambacho tunaelekea mwishoni mwa msimu, wachezaji wameshapitia mambo mengi kuanzia pre-season hadi hapa walipo, ndio maana hata wenzetu kikosi chao kilichocheza juzi kilikuwa na mabadiliko makubwa.”

Mara ya mwisho Azam kucheza mechi ya ushindani ilikuwa ni Aprili 22, 2023 [Ruvu Shooting 1-3 Azam FC], Ongala amesema anawaamini wachezaji wake na timu yake kuelekea mchezo wa kesho.

Screenshot_20230507_075647.jpg
 
Mtwara | “Maandalizi yote ya kucheza mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup yamekamilika, hakuna ambae hajui uzito wa mchezo huo. Tunacheza dhidi ya timu yenye wachezaji wazuri na benchi la ufundi zuri.”

“Naamini mchezo utakuwa wenye ushindani mkubwa, kwa kulielewa hilo maandalizi yote ya kucheza mchezo wa aina hiyo yamekamilika.”

- Juma Mgunda, Kocha Msaidizi Simba.
Screenshot_20230507_075847.jpg
 
CAF YATAKA OFISI YA MADAKTARI KWA MKAPA
.
Hii ni ofisi maalumu ambayo inatakiwa kuwepo kwenye Uwanja wa Mkapa na taarifa hiyo inasema iliyopo haina viwango vinavyotakiwa na Caf. Hii inaelezwa itakuwa maalumu kwa ajili ya kuwapa huduma ya kwanza wachezaji pamoja na waamuzi.
.
Imesema ofisi hiyo inatakiwa kuwa na; Meza moja, vifaa maalum kwa ajili ya matibabu ya dharura vifaa kwa ajili ya upasuaji mdogo, vifaa kwa ajili ya kupima upumuaji, vitanda, sindano za dharura na dawa, mashine maalum kwa ajili ya vipimo vya moyo, vipimo kwa ajili ya presha, vipimo vya kupima sukari mwilini pamoja na vingine vingi. [ image credit eliabennet ]View attachment 2612834
Auntie sasa picha ya konde inahusianaje na hii habari?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom