Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 12,105
- 35,140
Duuuh!Huyu ndie Dr. Nandipha, daktari aliyemsaidia Mbakaji na Muuaji Kutoroka Gerezani..!
Hapa duniani kila mtu ana sababu ya kufanya jambo lake, lakini wakati mwingine kuna watu wanaweza kufanya jambo la ajabu kila mtu akabaki anashangaa.
Mmojawapo ya watu hao ni Dokta Nandipha, mwanamke msomi aliyekuwa amefikia mafanikio nje na ndani ya fani yake ya utabibu usingeweza kufikiria angeshirikiana na Thabo Bester mtu aliyekuwa anachukuliwa kama kituko, mhalifu, Mbakaji na Muuaji hadi kumsaidia kutoroka Gerezani.
Jina lake kamili ni Dokta Nandipha Magudumana, alizaliwa mwaka 1989 huko Eastern Cape Afrika Kusini na kulelewa na mama yake katika mji wa Port Edward huko KwaZulu-Natal.
Dokta Nandipha ni daktari bingwa wa upasuaji. Alikuwa amepata mafanikio makubwa sana katika fani yake ya utabibu. Alikuwa ana kliniki binafsi iliyokuwa inajishughulisha na masuala ya urembo pamoja na matibabu ya ngozi.
Mwaka 2018 alitajwa kuwa miongoni mwa vijana wenye ushawishi mkubwa Afrika Kusini lakini pia alikuwa kwenye orodha ya vijana 200 wenye ushawishi katika jumuiya ya SADC kwa mujibu wa gazeti la Mail&Guardian.
Dr. Nandipha alikuwa ameolewa na Bwana Vugo Magudumana na katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, Aziza na Ayana.
Watu wengi wanasema kwamba Dr.Nandipha alikuwa anamsaidia Thabo Bester kutakatisha fedha.
Bado wanawake wenzake hawajajua Thabo Bester Mbakaji na Muuaji alikuwa anamkuna wapi Daktari huyu hadi kufikia hatua ya kutelekeza familia yake na kuambatana naye.
Wote Dr.Nandipha pamoja na Thabo wamekamatwa jana na polisi huko Arusha.View attachment 2582760
Maisha ya binadamu yana mengi sana nyuma ya pazia.
strange