Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli la Tanzania (TRC), Aidha, ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandishi John Nzulule.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus leo Jumapili Aprili 9, 2023 imeeleza kuwa Rais Samia amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwaelekeza Makatibu Wakuu wa Watendaji Wakuu kusoma ripoti hiyo, kujibu na kuzifanyia Kazi hoja zote.
Screenshot_20230410_055259.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linatarajia kumfikisha mahakamani, Kizito Odilo Achula (42), mkazi wa Ligula C, Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa tuhuma za mauaji ya mke wake, Victoria Almas (41).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Aprili 9, 2023, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo alisema siku ya tukio Achula aliingia ndani na kufunga mlango kisha kuanza kumpiga mkewe.

Kwa mujibu wa kamanda huyo mtuhumiwa alikuwa akimpiga mkewe mateke maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo tumboni, kifuani na usoni, shambulio ambalo lilisababisha kukatisha uhai wa mwanamke huyo.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara hivyo wamekuwa na ugomvi wa muda mrefu.
Screenshot_20230410_055457.jpg
 
Mjue Mbakaji na Muuaji Kutoka Afrika Kusini aliyekamatiwa Tanzania.

Huyu jamaa anaitwa Thabo Bester ni raia wa Afrika Kusini. Thabo alikuwa anatumikia kifungo cha maisha huko Afrika Kusini. Thabo alikuwa anakutana na wanawake kwenye mtandao wa Facebook anawadanganya kwamba atawasaidia wafanikiwe kwenye masuala yao ya urembo. Baada ya kukutana nao wengi alikuwa anawabaka kisha anawaibia na wengine anawaua. Mwaka 2012 akahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Sasa mwaka jana mwezi wa 5 selo aliokuwa anaishi katika gereza la Bloemfontein ikaungua moto na mwili wa mtu mmoja ukakutwa ndani ya selo hiyo ukiwa umeungua. Mamlaka za serikali ziliamini kwamba Thabo ndie aliyekuwa amekufa. Kadri miezi ilivyokatika tetesi zikaenea Afrika Kusini kwamba Thabo alikuwa ametoroka gerezani na ule mwili uliokuwa gerezani haukuwa wake ni mtu mwingine aliuwawa na kuingizwa gerezani. Vipimo vya DNA vilionyesha kwamba ni kweli mwili ule uliokutwa gerezani ukiwa umeungua haukuwa wa Thabo bali wa mtu mwingine. Inadaiwa Thabo alitoroka gerezani kwa msaada wa mpenzi wake Dokta Nandipha Magudumana kwa kushirikiana na walinzi wa gereza hilo. Gereza hilo linalindwa na walinzi wa kampuni binafsi ya G4S.

Mwezi uliopita polisi nchini humo wakaanzisha msako mkali wa kumsaka Mbakaji Thabo. Hatimaye jana Thabo akakamatwa huko Arusha akiwa pamoja na mpenzi wake daktari wa binadamu Dr. Nandipha Magudumana, inadaiwa alikuwa njiani akitoroka kwenda nchini Kenya.
Screenshot_20230410_055715.jpg
 
Huyu ndie Dr. Nandipha, daktari aliyemsaidia Mbakaji na Muuaji Kutoroka Gerezani..!

Hapa duniani kila mtu ana sababu ya kufanya jambo lake, lakini wakati mwingine kuna watu wanaweza kufanya jambo la ajabu kila mtu akabaki anashangaa.

Mmojawapo ya watu hao ni Dokta Nandipha, mwanamke msomi aliyekuwa amefikia mafanikio nje na ndani ya fani yake ya utabibu usingeweza kufikiria angeshirikiana na Thabo Bester mtu aliyekuwa anachukuliwa kama kituko, mhalifu, Mbakaji na Muuaji hadi kumsaidia kutoroka Gerezani.

Jina lake kamili ni Dokta Nandipha Magudumana, alizaliwa mwaka 1989 huko Eastern Cape Afrika Kusini na kulelewa na mama yake katika mji wa Port Edward huko KwaZulu-Natal.

Dokta Nandipha ni daktari bingwa wa upasuaji. Alikuwa amepata mafanikio makubwa sana katika fani yake ya utabibu. Alikuwa ana kliniki binafsi iliyokuwa inajishughulisha na masuala ya urembo pamoja na matibabu ya ngozi.

Mwaka 2018 alitajwa kuwa miongoni mwa vijana wenye ushawishi mkubwa Afrika Kusini lakini pia alikuwa kwenye orodha ya vijana 200 wenye ushawishi katika jumuiya ya SADC kwa mujibu wa gazeti la Mail&Guardian.

Dr. Nandipha alikuwa ameolewa na Bwana Vugo Magudumana na katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, Aziza na Ayana.

Watu wengi wanasema kwamba Dr.Nandipha alikuwa anamsaidia Thabo Bester kutakatisha fedha.

Bado wanawake wenzake hawajajua Thabo Bester Mbakaji na Muuaji alikuwa anamkuna wapi Daktari huyu hadi kufikia hatua ya kutelekeza familia yake na kuambatana naye.

Wote Dr.Nandipha pamoja na Thabo wamekamatwa jana na polisi huko Arusha.
Screenshot_20230410_055910.jpg
 
MESSI AMPIKU RONALDO
.
Supastaa wa Paris Saint-Germain, Lionel Messi amechangia kupatikana mabao 1,000 katika ngazi ya klabu na akapachika bao lake la 702 dhidi ya Nice.
.
Messi aliweka rekodi hiyo katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata kwenye mchezo wa Ligue 1 wikiendi iliyopita huku akifikisha asisti 298.
.
Nyota huyo wa kimataifa Argentina aliyebeba Kombe la Dunia mwaja jana alimpiku Ronaldo ambaye alikuwa akishikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote Ulaya mwenye mabao 701.
.
Messi mwenye umri wa miaka 35, amekuwa akihusishwa kutaka kuondoka PSG mwisho msimu huu na mkataba wake wa sasa unamalizika.
Screenshot_20230410_073746.jpg
 
MIAMBA
.
21—MANCHESTER United ilipiga mashuti 21 dhidi ya Everton kipindi cha kwanza, ikiwa ni rekodi kubwa ya mashuti tangu msimu wa 2003-04 kwenye mchezo mmoja wa Ligi Kuu England. Ni mengi pia kuliko yaliyopigwa na timu yoyote katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Screenshot_20230410_073904.jpg
 
Farhan Jr

MCHAWI GUARDIOLA USIKU KABLA YA FAINALI 2009.

Ni usiku mmoja kabla ya fainali, ni tarehe 26 Mei, 2009 ni jiji la kihistoria, majengo ya kuvutia na wenyewe walilibatiza jiji la milele! Jijini Rome nchini Italia ni ambapo itapigwa fainali ya UEFA kati ya Mashetani Wekundu dhidi ya Barcelona ya Hispania.

Usiku ule baada ya mkutano na Waandishi wa Habari, Pep Guardiola alirudi hotelini kwake Pallazo Galla na kuwaita watu wake wote wa bench la Ufundi, kisha akatoa picha yao waliyopiga wiki moja kabla.

Akawaambia hii picha nipo Mimi lakini hii picha haina maana yoyote bila ninyi, anaongea Mwanaume Bishoo kutoka Catalunya, anaongea Fashionista wa kweli kama Platnumz wa Tandale, njaa ya kweli ya Kiunderground kama Millard Ayo, anawajaza wenzake roho ya ushindi.

Baada ya pale Pep aliwaruhusu wakapumzike huku ikumbukwe aliwaruhusu Wachezaji wake wote wawe na Wapenzi wao usiku ule kuelekea fainali, ila yeye alikuwa mwenyewe chumbani kwake akipitia vitu kadhaa muhimu sana.

Katikati ya usiku mwingi na kibaridi cha Roma, Pep anawasha simu yake na kuanza kuwapigia watu muhimu sana kwake! Alianza na Carlo Mazzone ambaye alikuwa Kocha wake pale Brescia.

“Yo Carletto this is Pep, i want you to come tomorrow to watch our Barcelona” aliongea Pep kwa sauti ya uchovu sana! Mwalimu wake wa zamani mwenye miaka 72 wakati huo akamjibu “No worry Son, get some rest i will turn up” simu ikakatwa.

Pep alijua fika Man United ina nguvu sana kwa Waandishi na Media zote waliipa coverage kubwa United, hivyo yeye akawa anawapigia Wanae wote aliocheza nao wakati yupo Italia, ambao wote waliahidi watamsupport.

Mwanaume Pep bado hajazima taa za chumba chake, akapitia tena email za Kachero wa Barcelona kuhusu hali ya uwanja usiku ule, maji yaliyomwagwa na namna gani pitch itaenda na Tik Tak, ile soka lake, akaahidi kuifanyia kazi report asubuhi sana.

Kabla hajalala mlango wake unagongwa! Mashetani watatu Xavi, Iniesta na Messi wanataka kusema nae jambo maana hawana usingizi pia, Mwanaume anasimama kwenda kufungua…..

ITAENDELEA…..
Screenshot_20230410_074104.jpg
 
Huyu ndie Dr. Nandipha, daktari aliyemsaidia Mbakaji na Muuaji Kutoroka Gerezani..!

Hapa duniani kila mtu ana sababu ya kufanya jambo lake, lakini wakati mwingine kuna watu wanaweza kufanya jambo la ajabu kila mtu akabaki anashangaa.

Mmojawapo ya watu hao ni Dokta Nandipha, mwanamke msomi aliyekuwa amefikia mafanikio nje na ndani ya fani yake ya utabibu usingeweza kufikiria angeshirikiana na Thabo Bester mtu aliyekuwa anachukuliwa kama kituko, mhalifu, Mbakaji na Muuaji hadi kumsaidia kutoroka Gerezani.

Jina lake kamili ni Dokta Nandipha Magudumana, alizaliwa mwaka 1989 huko Eastern Cape Afrika Kusini na kulelewa na mama yake katika mji wa Port Edward huko KwaZulu-Natal.

Dokta Nandipha ni daktari bingwa wa upasuaji. Alikuwa amepata mafanikio makubwa sana katika fani yake ya utabibu. Alikuwa ana kliniki binafsi iliyokuwa inajishughulisha na masuala ya urembo pamoja na matibabu ya ngozi.

Mwaka 2018 alitajwa kuwa miongoni mwa vijana wenye ushawishi mkubwa Afrika Kusini lakini pia alikuwa kwenye orodha ya vijana 200 wenye ushawishi katika jumuiya ya SADC kwa mujibu wa gazeti la Mail&Guardian.

Dr. Nandipha alikuwa ameolewa na Bwana Vugo Magudumana na katika ndoa yao wamebahatika kupata watoto wawili, Aziza na Ayana.

Watu wengi wanasema kwamba Dr.Nandipha alikuwa anamsaidia Thabo Bester kutakatisha fedha.

Bado wanawake wenzake hawajajua Thabo Bester Mbakaji na Muuaji alikuwa anamkuna wapi Daktari huyu hadi kufikia hatua ya kutelekeza familia yake na kuambatana naye.

Wote Dr.Nandipha pamoja na Thabo wamekamatwa jana na polisi huko Arusha.View attachment 2582760
... Shunie kwa wale wapenzi wa Isindingo "The Need" jina hili Nandipha ni maarufu sana.
Dokta katenda zaidi ya majukumu yake
 
dr mrembo,kadata na msela
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom