Farhan Jr
A message to the future! Mnaitazama hii picha leo March 20, 2509 najua kizazi chetu hakikuacha picha nyingi za maana, mabango ya Ujugu hayana maana, hatujaacha vitu vingi sana zaidi ya stori za Mashalove na Mfalme Zumaridi, hatujaacha urithi wa kutisha zaidi ya Harmorapa na Kikombe cha Babu.
Licha ya uzuri wetu wa mkakasi ila ndani kipande cha mti! A message to the future sahauni kuhusu stori mtakazoziona Youtube kuhusu Fair Competition au Kocha Adel kuwaacha wakina Zimbwe, tunajua hatuna vingi vya maana ila kuna hazina tumewaachia.
Nani mwenye hekima na busara kati yenu mtachaguana! Nani anajua kubadili picha kuwa maneno kama The Great Lufufu Mkandala au Juma Khan? Basi mtumeni mpaka Ghorofa ya 10 pembezoni mwa Bahari ya Hindi, kuna urithi wenu tumewaachia.
Atakayefunga safari kwenda Posta mwambieni asigeuke nyuma kwakuwa atapishana na wadada wenye shape kali akatengua udhu yake, mwambieni picha ya upako wa vizazi na vizazi ikafuatwe ile picha irejeshwe Makumbusho pale Jangwani, avae kanzu asiwe na tamaa! Mezani ataikuta.
Urithi pekee wa maana katikati ya penzi la Whozhu na Sepetu Wema, katikati ya hekaya za Kaka Vunjabei na Hamisa, Manara na Rushayna basi sie tumewaachia kumbukumbu bora katika picha, itunzeni sana! 25 ni Kennedy Musonda na 9 ni Fiston Mayele.
A message to the future msiipoteze hiyo picha! Itunzeni vizazi na vizazi! Ina maana kubwa sana kwa Yanga na harakati zao kwenye soka la Afrika.
Wenu Mtiifu, Babu Farhan Kihamu aliyepumzika kwenye makaburi ya Ifakara, Kilombero, Morogoro

Itunzeni hiyo picha