@AhmedAlly_ alianza kufanya hamasa kuita mashabiki uwanjani kwa kuzunguka mitaa tofauti ya Dar kwa kutumia ‘kispika’ akafanikiwa.
Baadae tukaona @AliKamwe na maandamano kule Mabagala na baadae jogging na yeye pia akafanikiwa kwa upande wake.
Jana Ally kamwe aliendelea na hamasa kuelekea mchezo wao dhidi ya Real Bamako, tumeona watu wanakula ugali kwa sukari pale maeneo ya Buguruni.
Leo Ahmed Ally amekuja tena na kitu kipya, safari hii amesema hatazunguka na kispika chake kakini amewaita mashabiki wa Simba wakutane Coco Beach ‘Wenye nchi Beach Party’.
Ahmed anasema mashabiki wanakutana, wanakula upepo, wanafahamiana, wanafurahi na kukubaliana namna bora ya kushangilia siku ya mechi lakini vilevile kutakuwa na wauzaji wa tickets za mechi yao dhidi ya Vipers.
Alichofikiria Ahmed naona ni kitu kizuri na vitu vipya vinaingia kwenye mpira wetu! Pata picha siku hiyo kunakuwa na sound nzuri pale Coco Beach halafu kunakuwa na wasanii kadhaa kwa ajili ya kutengeneza vibe kwa mashabiki.
View attachment 2536490