Farhan Jr
ARSENAL, kuna mafuta maarufu ya Babycare, kuna mafuta maarufu ya Mwamposa kisha kuna mafuta maarufu ya Mtumishi wa mpira Mikel Arteta, madhabahu ya Emirates yanajibu maombi, kutoka nyuma kwa mabao mawili hadi kushinda mabao matatu na alama tatu.
Mhando Rose aliimba

Amepindua Agenda

The Arsenal Boys walinasa mashairi na wakamwomba Salim Kikeke awape maana ya mashairi yale kisha Nelson mwanakondoo akawapa Arsenal furaha jioni ya leo kwa sauti ya Mtu Imara Mwamba kachil.
Edo Kumwembe wa Mtwara alishashuka juu ya mwembe mara mbili kuwa hataki kuwa rahisi, Madee wa Manzese akawaambia kazi hii rahisi! Uhaba wa barabara za makombe London? Basi chagua Madee, uhaba wa ushindi London basi jibu ni Madee Ali Seneda.
Jamhuri ya watu wa kubet walianza kumtusi Arteta kuhusu Arsenal FT, vijana kutoka @tmichezo.tz wakaingia sana LIVE kumpa Bournemouth WIN ila walisahau Premier league is more than a league, football is more than a game! Arsenal took it personal.
The Gunners kwa majina, wanaimba Mama Amina tu mtaani kwasasa! Furaha isiyo kifani na tamko rasmi la Wizara ya mambo ya ndani ya Arsenal chini ya
Jamestupatupa ni kuwa watembee mafungu mafungu maana maadui ni wengi sana.
The comeback nights are not for everyone, Arsenal ni number one! Vaa miwani the Boys mean it this time!