Makapuku Forum

Makapuku Forum

WANANCHIIII!?
Hii ni yenu sasa..Mabingwa wa kihistoria wa soka la Tanzania wanaianza Safari katika makundi ya Shirikisho wikiendi hii...Kabumbu litakujia LIVE kupitia @startimestz ...

Mechi kali Wikiendi Hii
J'pili Februari 12,
US MONASTIR vs YANGA SC
|1:00 Usiku.

J'pili Februari 12,
TP MAZEMBE vs REAL BAMAKO
|10:00 Jioni

Screenshot_20230209_112143_OGInsta%2B.jpg
 
BODI YAIBEBA COASTAL KIAINA
.
Bodi ya Ligi imefafanua juu ya maamuzi yaliyotengua adhabu walizokuwa wamepewa Mtunza vifaa wa Coastal Union, Mathayo Francis na kipa wa timu hiyo, Justine Ndikumana, baada ya maamuzi hayo kuzua maswali kwa wadau wa soka.
.
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi iliwaadhibu wawili hao kwa kosa walilofanya siku ya mechi ya Ligi dhidi Kagera Sugar wakitozwa Sh 1 Milioni kwa mtunza vifaa na Sh 500,000 kwa kipa sambamba na kufungiwa michezo mitatu kila mmoja kabla ya juzi kutenguliwa.
.
Taarifa mpya ya juzi ilisema kamati hiyo ilikutana Januari 31 kurejea shauri la wahusika hao wawili na kubadilisha hukumu baada ya kufanya tathmini ya maelezo kutoka vyanzo zaidi na kujiridhisha kuwa, awali zilizowasilishwa kikao chake cha awali cha Januari 26 hazikuwa sahihi.
Screenshot_20230209_112348_OGInsta%2B.jpg
 
NABI ATAJA MASTAA WANNE WAKUCHUNGWA
.
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi baada ya kwasoma US Monastir katika mechi zao mbili akizishuhudia kwa macho yake kisha kuangalia mechi za mikanda ya video amefunguka kuwa wanakazi ya kuwachunga mastaa wanne wa timu hiyo watakaovaana nao Jumapili hii mjini Tunis.
.
Amefichua kwamba wapishi wa US Monastir ni mabeki wao wawili wa pembeni. Amewataja wengine kuwa ni kiungo wao wa kati na nahodha wao huku pia wakiwa na mshambuliaji anayejua kufunga kwa vichwa katika safu yao uya ushambuliaji.
.
“Tunatakiwa kuwa makini na hao wachezaji wanne, timu yao inategemea ubora wao katika kutengeneza mashambulizi lakini mtu wa kumalizia ni huyo mshambuliaji wao, tutatafuta akili ya jinsi ya kuwadhibiti.”
Screenshot_20230209_112546_OGInsta%2B.jpg
 
Cleopatra Malkia Anayesadikika Kuwa Mwanamke Mzuri Zaidi Kuwahi Kutokea Duniani:


MALKIA Cleopatra ni maarufu zaidi kati ya malkia wote waliowahi kutawala Misri. Cleopatra alizaliwa Alexandria mwaka wa 69 K.K (kabla ya kristo) Wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII.

Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa. Cleopatra hakua Mmisri, isipokuwa alikuwa Macedonia familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander the Great. Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.

Cleopatra mwenye miaka 18 mapema anathibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususani katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania. Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.

Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia. Ametajwa katika vitabu kadhaa ikiwemo Biblia na aliishi kwa miaka 39. Cleopatra alikuwa ndiyo mtawala wa mwisho wa Kigiriki kutawala Misri na ndiyo aliyekuwa Farao wa Kwanza wa kike mgeni. Alizaliwa mwaka 69 na akiwa na miaka 18 akatawazwa kuwa Malkia.

Cleopatra ni neno la Kigiriki linalomanisha “baba yangu ni maarufu” Cleopatra ni jina walilolopewa mabinti wa kifalme wa kigiriki huku wale wa kiume wa kifalme waliitwa Ptolemy.

Hivyo Cleopatra huyu tunayemzungumzia hapa alikuwa ni Cleopatra wa Saba na wa mwisho. Dola la Misri lilitawaliwa na Ugiriki tangu mwaka 323 baada ya Alexander Mkuu kuishinda Misri na utawala huu uliisha mwaka 30 baada ya Cleopatra kujiua kwa kumruhusu nyoka aina ya Cobra kumgonga kifuani.



Imeandikwa😀unstan Mtili Erick kwa msaada wa Mitandao





Screenshot_20230209_205613_Opera%20Mini.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom