Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Tanzania milango iko wazi kwenye uwekezaji wa Sekta ya Nishati kutokana na uwepo wa mahitaji makubwa ya Nishati katika uzalishaji na usambazaji kwenye maeneo ya Sekta hiyo.

Waziri Makamba ameyasema hayo Dar es salaam katika mkutano wa Wadau wa Nishati, Wawekezaji, Makampuni ya Nishati kutoka Nje, Mabalozi wa Nchi mbalimbali ambao unaangazia hali ya Nishati sambamba na maendeleo yaliyofikiwa.

Waziri Makamba amesema “Kwanini Tanzania?, Kwanini sasa? Tanzania ni mahali sahihi penye amani katika kufanya uwekezaji, hivyo tunawakaribisha Wawekezaji wenye tija kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati Nchini”

Kwa upande wao Washiriki katika Mkutano huo wamepongeza juhudi za Serikali katika Sekta ya Nishati kwa kufungua wigo wa uwekezaji sambamba na kutatua changamoto zinazoikabili Sekta hiyo ikiwemo urasimu.

Mkutano umeandaliwa na EnergyNet kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati, EWURA, TPDS na TANESCO.
Screenshot_20230203_051525_OGInsta%2B.jpg
 
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe atakuwa nje kwa takribani wiki tatu baada ya kuumia jana kwenye mechi dhidi ya Montpellier na alicheza dakika 21 tu.

Sasa Mbappe atakosa mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich Februari 14.
Screenshot_20230203_051717_OGInsta%2B.jpg
 
Kesi ya ubakaji na kutishia kuua iliyokuwa ikimkabili kinda wa Manchester United Mason Greenwood imefutwa rasmi leo baada ya ushahidi kujitosheleza.

Mara ya mwisho Greenwood kutinga mahakamani kwaajili ya kusikiliza kesi yake ilikua Novemba mwaka jana lakini kesi hiyo ikaghairishwa na ingesikilizwa tena Novemba 23 mwaka huu.

Greenwood alikamatwa na polisi nyumbani kwao Januari mwaka jana baada ya kushtakiwa na mpenzi wake aliyedaiwa kutendewa vitendo hivyo.
Screenshot_20230203_051808_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limeanza uchunguzi wa tukio la mtoto mwenye umri wa miaka 10 anayedaiwa kukamatwa na wasamalia wema katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza katika harakati za kutoroka na mtoto wa mwajiri wake kwenda mkoani Mbeya.

Taarifa ya mtoto huyo ilisambaa kuanzia jana Jumatano Februari Mosi mwaka huu katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha binti huyo akihojiwa na mwanamke ambapo alinukuliwa akitaja jina la kichanga hicho huku akishindwa kujibu maswali mengine aliyoulizwa.

Akizungumza leo na Mwananchi Digital Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema katika mahojiano binti huyo alidai kusafirishwa kutoka kwa wazazi wake mkoani Mbeya na mwalimu wa Shule ya Msingi Ilendeja iliyoko Kisesa wilayani Magu mkoani hapo kwa lengo kuja kumsaidia kazi huku kukiwa na ahadi ya kumsomesha jambo ambalo halikufanyika.

"Februari Mosi mwaka huu aliamua kutoroka na mtoto huyo kwa lengo la kwenda Mbeya kwa sababu alikuwa amechoka kukaa na yule mwalimu ambaye anamtuhumu kwamba alikuwa akimfanyia vitendo vya ukatili kwa kumchapa mara kwa mara," amesema Mutafungwa

Mutafungwa amesema jeshi hilo pia lilikutana na mwalimu huyo, Diana Mwaihoji ambaye alikiri kuwa kichanga hicho ni chake huku akikiri kuwa binti huyo alikuwa hausigeli wake ambaye alimtoa mkoani Mbeya kwa ajili ya kumsaidia kazi za ndani.
Screenshot_20230203_051904_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu ameagiza jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Wilaya Tukuyu kumalizika kwa wakati na kuanza matibabu ifikapo Machi, 2023.

Akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama amefanya ziara fupi katika hospitali hiyo leo Alhamisi Februari 2, 2023 na kuzungumza na wagonjwa wanaopata huduma katika hospitali hiyo.

Aidha, amepongeza kwa kasi kubwa inayoendelea ya upanuzi wa hospitali hiyo ambapo jumla ya majengo mawili yanaendelea kujengwa.

Jengo jingine linalojengwa ni la wagonjwa wa nje (OPD) ambapo lipo hatua ya umwagaji jamvi ghorofa ya kwanza.

Screenshot_20230203_051958_OGInsta%2B.jpg
 
Watu watatu wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa katika mapambano kati ya maofisa misitu na wakazi wa Kijiji cha Chakulu Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye zinasema tukio hilo lilitokea juzi Jumatatu Januari 31, 2023.
Kupitia ujumbe mfupi wa maneno, Mkuu huyo wa mkoa amesema waliofariki katika tukio hilo ni afisa mmoja wa idara ya misitu Wilaya ya Uvinza na askari mgambo wawili, ambao hata hivyo hakuwataja majina.

Taarifa zaidi zinadai wakati askari mgambo wanne wamejeruhiwa, wenzao watano watano, kati yao, watatu wakiwa na silaha hawajulikani walipo tangu juzi tukio hilo lilipotokea.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu amethibitisha kutokea kwa mapambano kati ya wananchi na maofisa misitu lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu ndio alikuwa njia kwenda eneo la tukio.

“Nitatoa taarifa rasmi baada ya kufika eneo la tukio; kwa sasa ninachoweza kusema ni kweli tukio hilo limetokea na niko njiani naelekea huko,” amesema Kamanda Makungu
Screenshot_20230203_052310_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amemshukia Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina akimtaka kuwa na uhakika juu ya taarifa anazotoa hasa zinazohusu masuala ya kiuchumi.

Akijibu hoja ya Mpina kwamba mfumuko wa bei umetokana na utekelezaji usio mzuri wa sera za fedha na mambo mbalimbali ikiwamo kufanya malipo nje ya bajeti, Dk Mwigulu amesema, “embu tujadili mambo mengine yanayohusu uganga wa kienyeji… kwenye uchumi hii ni taaluma yangu, mnajadilije vitu ambavyo viko wazi?”

Akichangia taarifa za Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira leo Februari 2, 2023 Dk Mwigulu amesema fedha zilizolipwa nje ya bajeti ni Sh86 bilioni baada ya kugundulika kuwa wanafunzi 29,000 waliokuwa wamedahiliwa kwenye elimu ya juu walikuwa nje kwa kukosa ada na kwamba fedha hizo zilitolewa baada ya Bunge kuazimia kuwa Serikali itafute fedha za kuwapa mikopo.

Dk Mwigulu amesema Serikali pia ilitoa Sh160 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 8,000 ili wanafunzi waliokuwa wakijiunga na shule waweze kuendelea na masomo akisisitiza kuwa kutoa fedha nje ya bajeti hakuwezi kusababisha mfumko wa bei huku akionyesha mshangao juu ya hoja kwamba kujenga madarasa kunasababisha mfumuko wa bei.

“Anapotokea mbunge na kusema tumetoa nje ya bajeti na kuishambulia Serikali kama vile imefanya uamuazi usio mzuri lazima kuwe na kasoro katika kufikiri kwake huwezi kuchukia fedha ambazo zinaenda kwenye ujenzi wa madarasa,” amesema.

Amesema angetamani kuona wabunge wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi huo wa kutoa fedha zilizowezesha wanafunzi wote kupata mikopo na kujenga madarasa.
Screenshot_20230203_052411_OGInsta%2B.jpg
 
Tulifanya kila kitu kuhakikisha Enzo anabaki mpaka angalau dirisha kubwa lakini Mchezaji hakuwa tayari, baada ya kugundua kuwa hayupo tayari kuvaa jezi yetu nikaamini hafai hata kuingia kwenye vyumba vyetu ndio maana tukamruhusu aende, Mchezaji akitaka kuondoka basi unamruhusu aende.

- Rui Costa, Rais wa Benfica.
Screenshot_20230203_052633_OGInsta%2B.jpg
 
Manchester United wamekiri kupokea rasmi taarifa kumhusu Kinda Mason Greenwood kuwa mashtaka yote dhidi yake yameondolewa lakini United wamesema watakaa chini na kulitazama vyema jambo hilo kabla ya kutoa taarifa rasmi juu ya hatma ya kinda huyo.

Ukipitia comments nyingi wengi wanataka Mason aondolewe Manchester United japo baadhi wanapinga.
Screenshot_20230203_052727_OGInsta%2B.jpg
 
Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya tano (5) kwa ubora barani Afrika na ya 39 duniani kwa mwaka 2022
Screenshot_20230203_052826_OGInsta%2B.jpg
 
Shaffih Dauda

Jambo lililotokea kati ya Yanga na mdhamini wao mkuu naona ni makosa ya kiutendaji zaidi.

Hizi klabu kila siku zimekuwa zikihubiri mabadiliko ya kiuendeshaji, wanasema wamefanya mabadiliko na kutengeneza mifumo mipya ya kuendesha klabu kwa weledi.

Wamekuja na watu wanaoitwa CEOs [Watendaji wa Wakuu wa klabu], mimi ninachokiona kwa picha ya nje wametenegeneza tu structure kutuonesha uongozi umekamilika.

Tena wameajiri watu kutoka nje ya nchi ambao tunaamini ni watu waliobobea kabisa kwenye masuala ya weledi ili kuja kutusaidia kwenye masuala ya uendeshaji wa klabu kwenye mambo ya utendaji wa kawaida.

Lakini yanayotokea yanatuonesha picha nyingine kuwa hao watu hawapo, wapo tu kwenye picha! Hawapo kwenye utendaji wa kawaida kutokana na haya makosa yanayojirudiarudia.

Mtendaji Mkuu na watu wa idara ya sheria ndio watu wanaowajibika na hili tunaloliona. Inawezekana kwenye picha ya juu tunamuona Rais wa klabu au Makamu lakini kiuhalisia wao sio watendaji.

Rais wa timu inawezekana hajui mambo ya sheria na mikataba lakini Mtendaji Mkuu ndio anajua mikataba yote ya washirika wao na wanapaswa kuwapa nini na wao wanapata nini.

Yanga wanasema waliwasiliana na mdhamini mkuu wakampa mapendekezo akaridhia, wao wakaendelea na mchakato.

Saa chache baada ya mdhamini mwingine kutangazwa na kukaa kifuani kwenye jezi, anaibuka mdhamini mkuu anatoa taarifa ya kulalamikia kitendo kilichofanyika.

Aliyetoa taarifa ya Yanga kuwasiliana na mdhamini mkuu ni Rais wa klabu ambaye kiuhalisia si mtendaji! Kiuhalisia Mtendaji Mkuu ndio anawasiliana na mhusika [mdhamini mkuu].

Rais anapotoka kuzungumza na umma tayari anakuwa amepewa miongozo/ripoti na Mtendaji Mkuu, Rais anapotoa taarifa halafu baadae inalalamikiwa na mshirika wao maana yeke watendaji ndio wanaotakiwa kuwajibika.

Mimi naona hili jambo linapaswa kujibiwa na Mtendaji Mkuu pamoja na mwanasheria wa klabu. Mtendaji Mkuu ndio atuambie nani kawaingiza chaka?
Screenshot_20230203_052910_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Simba Robert Oleveira baada ya kurejea nchini ameeleza mipango iliyopo mbele yake kuhakikisha Simba inafikia malengo yake.

Robertinho amesema anafahamu ana kazi kubwa ya kufanya kwani ana michuano ya Ligi Kuu, Kombe la TFF na Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo anatakiwa kuhakikisha malengo yanafikiwa.

“Simba ina malengo ya kufanya vizuri kwenye mashindano yote inayoshiriki [Ligi Kuu, Kombe la TFF na Ligi ya Mabingwa Afrika].”
Screenshot_20230203_053345_OGInsta%2B.jpg
 
Mchezaji wa Tanzania Prisons Zabona Hamis Mayombya amepata ajali mbaya na imegundulika fuvu lake limepata ufa ‘crack’.

Afisa Habari wa Tanzania Prisons Jackson Mwafulango amesema taarifa za awali kutoka kwa daktari wa timu hiyo zinasema, Zabona huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi miwili.

Tayari Zabona ameshafikisha Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mchezaji wa Tanzania Prisons Zabona Hamis Mayombya amepata ajali mbaya na imegundulika fuvu lake limepata ufa ‘crack’.

Afisa Habari wa Tanzania Prisons Jackson Mwafulango amesema taarifa za awali kutoka kwa daktari wa timu hiyo zinasema, Zabona huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi miwili.

Tayari Zabona ameshafikisha Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.

Pole sana Zabona, tunakuombea upone haraka urejee tena dimbani.
Screenshot_20230203_053431_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha Mohamed Abdallah ‘Bares’ ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha Tanzania Prisons na kuahidi kufanya vizuri kwenye michezo tisa (9) iliyosalia ya msimu huu 2022|23.

Bares amepata shavu la kuifundisha Tanzania Prisons muda mfupi baada ya kushinda ubingwa wa Mapinduzi Cup 2023 akiwa na Mlandege FC ya visiwani Zanzibar.

Jukumu la kwanza la Bares ni kuhakikisha Tanzania Prisons inabaki Ligi Kuu kwa ajili ya msimu ujao 2023|24.

Msimu uliopita Prisons ilicheza play offs za kujinusuru isishuke daraja na ikafanikiwa kubaki Ligi Kuu. Ikiwa imebakiwa na mechi 9 kabla ya msimu kufika mwisho, Prisons ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama 21 sawa na Dodoma Jiji ambayo ipo nafasi ya 13.
Screenshot_20230203_053807_OGInsta%2B.jpg
 
ANDREA PIRLO, THE PROFESSOR, THE BRAIN OF MILAN.

Imeandikwa na @jr_xavihernandez.

Kuna mtu mmoja aliyeitwa Mircea Lucescu alitabiri Andrea Pirlo atakuja kupata mafanikio makubwa sana kwenye soka ni muda ambao Pirlo hajafika miaka hata 19 lakini mtu yule alimtazama Pirlo kwa jicho la tatu.

Andrea Pirlo alikuwa zake akicheza pale Brescia akiwa na miaka 16. Baba yake alikuwa mmiliki wa viwanda vya kusindika chuma, Pirlo alipita njia yake akaamua kuchagua soka, Nini kilifuata?

Mwaka 2001 kocha Carlo Ancelotti anamtambulisha Andrea Pirlo kwenye timu ya Ac Milan, Waitaliano walimuona ni mwendawazimu unatuleteaje mchezaji ambaye hana hata nguvu tena kwenye eneo la ulinzi?

Waitaliano walizoea viungo wa shoka kwenye eneo la ulinzi viungo wababe wanaoweza kupambana kwa namna zote kucheza rough,tackling na roho mbaya kina Demetrio Albertini lakini Pirlo hakuwa hivyo.

Waitaliano walishindwa kubakiza maneno Ancelotti hakujali alimtumia Pirlo kama Deep-Lying Playmaker yani kiungo mkabaji anaehusika na ushambuliaji.

Ghafla waitaliano wakaanza kuimba wimbo mmoja wakaanza kumuita Professor wa mpira kila alipocheza majukwaa ya San Siro yaliwehuka na burudani alizokuwa anazitoa Andrea Pirlo.

Bado Wafaransa hawajasahau ile fainali ya kombe la Dunia 2006 kwa jinsi Pirlo alivyokuwa anawatawanya aliitoa timu kutoka kwa Gattuso akaipeleka kwa Luca Toni na Totti, Miguu ya Pirlo ilikuwa na rula,penseli,ufutio na bikari.

Alimeza dimba lenye mapafu wawili yani Vieira na Makelele, Waitaliano wakamuita tena The Brain of Milan, Achana na Pirlo kabisa, Joe Hart mpaka kesho anaiota ile Panenka kwenye Euro 2012.

Pirlo alikuwa mchawi wa Dimba, Waitaliano walikili hawakuwahi kuwa na kipaji kama yeye ndani ya miaka 25. Ni mwanadamu ambaye alipiga pasi za aina zote kwa usahihi sana(fupi,ndefu). Alitumia akili kuliko mabavu.

2011 Pirlo anamwambia Buffon kwamba nakuja Juventus, Buffon alisema maneno machache alisema Asante Mungu, Pirlo anakuja Juventus, San Siro hakukuwa na mtu fundi kama Pirlo.

Kwenye Ac Milan tishio pale ulaya ile Milan yenye Kaka,Gattuso na Seedorf, Juu inao Crespo na Shevchenko. Katikati yao alikuwepo Pirlo. Unaweza kumuita Proffesor au Brain of Milan.
Screenshot_20230203_053919_OGInsta%2B.jpg
 
Mjadala wa Pichichi unaweza kuisha mapema sana nchini Hispania, amezima kelele nyingi sana Mpoland Robert Lewandowski, kila siku anakata kamba tu kwenye LA LIGA.
Screenshot_20230203_054455_OGInsta%2B.jpg
 
WANAKUJA HIVYO!!
.
47—NEWCASTLE United wamefuzu katika fainali yao ya kwanza ya kombe kubwa tangu 1999 (Kombe la FA), na fainali yao ya kwanza ya Kombe la Ligi tangu 1976. Hilo ni pengo la miaka 47 kati ya mechi za fainali za Kombe la Ligi na ndilo refu zaidi kwa timu yoyote katika historia ya mashindano England.

Screenshot_20230203_054609_OGInsta%2B.jpg
 
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa katika tovuti ya IFHHS inayojihusisha na utoaji wa takwimu za michezo duniani imeonyesha kuwa Ligi Kuu ya NBC inakamata nafasi ya 5 barani Afrika na nafasi ya 39 Duniani.
Screenshot_20230203_054857_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom