Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230202_053418_OGInsta%2B.jpg
 
NABI: AZIZ KI DAK 40 TU
.
Kocha Nabi amesema ana muda mfupi wa kupandisha ubora wa Stephane Aziz KI ambaye kwa sasa katika mechi ngumu anahimili kucheza kwa umahiri dakika 40 tu.
.
“Amecheza vizuri, kuna kitu amefanya nakubali lakini bado hajawa katika ubora ambao nautaka na mimi kocha nikafurahi kama walivyofurahi mashabiki, Ile ni mechi ndogo sana (dhidi ya Rhino), tutakapokuja kucheza mechi ya ushindani mkubwa dakika nyingi sana Aziz anaweza kucheza ni 40 kwa sasa ili acheze kwa ubora mkubwa,”.
.
“Tunakwenda kucheza mechi ngumu sana dhidi ya Monastir, kuna kazi nilikwambia wiki iliyopita ambayo tunaifanya kuhakikisha Aziz na wengine ambao viwango vyao vipo chini tunavipandisha. Tuna siku 10 zimebaki kabla ya mechi hiyo ngumu lakini hapa kati pia tutakuwa na mechi ngumu dhidi ya Namungo ya ligi tutatumia hizi siku kuhakikisha tunaongeza ubora wake.”
Screenshot_20230202_053507_OGInsta%2B.jpg
 
HAKIM Ziyech mpango wake wa kutua Paris Saint-Germain umekwama. Uhamisho wake kutoka Chelsea hadi PSG umekwama, kwa sababu fomu za uhamisho zilichelewa kutumwa kutoka London.
.
Ziyech tayari alikuwa katika jiji la Paris takribani siku nzima, akifanyiwa vipimo vya Afya. Akisubiria uhamisho ukamilike aweze kucheza na mastaa kama Lionel Messi, Kylian Mbappe na Neymar .
.
Jioni ya jana lilikuwa linasubiriwa tangazo rasmi la vilabu vyote viwili kukamilisho uhamisho huo, lakini haikuwezekana. Usiku sana ripoti zikaibuka kwamba Chelsea ilituma nyaraka hizo nje ya muda, na kusababisha uhamisho usipitishwe kwa wakati. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari kutoka Paris France Bleu, Chelsea ilituma fomu zisizo sahihi kwa mara tatu.
Screenshot_20230202_053557_OGInsta%2B.jpg
 
MAZUNGUMZO yakidumu kwa zaidi ya mwezi mmoja, hatimaye Chelsea mwishoni kabisa imefanikiwa kumpata kiungo fundi Enzo Fernandez. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 bingwa wa dunia akiwa na Argentina anaondoka Benfica kwa euro milioni 120. Dili lake limethibitishwa dakika chache baada ya dirisha kufungwa, lakini karatasi na mikataba ilisainiwa kwa wakati.
.
Miamba ya Ureno, Benfica ilimchukua Enzo Fernandez kutoka River Plate Julai 14, 2022 kwa kiasi cha euro milioni 14. Fundi huyo wa Argentina pia alikuwa na asilimia ya mauzo ya asilimia 25. Hiyo ina maana kwamba kati ya euro 120 milioni, milioni 90 itakwenda Lisbon na milioni 30 kwa River Plate.
.
Kwa kukamilisha usajili wa Enzo Fernandez, mabosi wa Chelsea wametumia kiasi cha cha euro 610 milioni msimu huu katika kufanya sajili za wachezaji wapya.
Screenshot_20230202_053710_OGInsta%2B.jpg
 
Mazungumzo kati ya Thiago Silva na Chelsea yapo kwenye hatua nzuri juu ya kuongeza kandarasi mpya ya kucheza soka West London ambapo Chelsea wanamtazama yeye kama Kiongozi wakati wanawaandaa wachezaji vijana.
Screenshot_20230202_054438_OGInsta%2B.jpg
 
Shaffih Dauda

Kuna kitu tunapaswa kujifunza kutoka kwa KRC Genk kwa namna ambavyo wanaendesha klabu yao na mafanikio ya wachezaji wanaotoka kwenye klabu hiyo kusajiliwa na klabu nyingine hususan England.

Mbwana Samatta [Aston Villa, Fenerbahce] Leon Bailey [Leverkusen, Aston Villa] Leandro Trossard [Briton, Arsenal] Omar Colley [Sampdoria] Paul Onuachu [Southampton] hao ni baadhi ya wachezaji ambao Genk iliwauza kwenye vilabu vya Ligi Kubwa za Ulaya.

Wenyewe wamechagua kuwa sehemu ya kutengeneza bidhaa ambazo zinahitajika sokoni. Wanachukua wachezaji wenye umri mdogo ambao hawatamalizia soka Genk ili baada ya miaka miwili hadi mitatu wafanye bishara.

Wamechagua kuwa kiwanda kama ambavyo Ajax wanafanya, kuzalisha zaidi wachezaji kuliko kuwang’ang’ania wastaafie klabuni kwao.

Hapa kwetu Mtibwa Sugar walichagua kuwa kiwanda cha kutengeneza wachezaji lakini kadiri miaka inavyozidi kwenda wameamua kushindana na vijana hawapati nafasi kama ilivyokuwa zamani.
Screenshot_20230202_054812_OGInsta%2B.jpg
 
Shaffih Dauda

Usajili ambao mimi umenishangaza ni wa mshambuliaji Paul Onuachu kutoka KRC Genk [Belgium] Southampton [England] sio mchezaji mwenye jina kubwa ndio maana uhamisho wake haujawa habari kubwa.

Onuachu alikuwa mfungaji mahiri tangu amejiunga na Genk, kuna wakati alikuwa na rekodi ya mchezaji wa Afrika mwenye magoli mengi kwenye Ligi kubwa za Ulaya.

Akiwa Genk amecheza Mechi 134, amefunga Magoli 85, na kushinda tuzo ya mfungaji bora wa msimu mara 1.

Hivi karibuni wakati nipo Belgium nilipata fursa ya kushuhudia game ya Genk vs Zulte Waregem, ukimwangalia uwanjani kwa mazingira yetu ya Tanzania hapewi nafasi hata kwenye timu ya Ligi Daraja la Nne.

Wakati mechi inaendelea Onuachu ndio alikuwa mjadala kwa baadhi ya watanzania waliokuwepo uwanjani wanashuhudia mchezo ule. Wengi wao walikuwa wanahoji kwa nini Onuachu anacheza wakati kukimbia hawezi wala kumpita hata mchezaji mmoja!

Mimi nikawa nawaambia naheshimu sana maamuzi ya kiufundi kwa maana ya benchi la ufundi lazima watakuwa wameona kitu kwa mchezaji huyo hawawezi kumchezesha tu kama hana kitu.

Wenzetu wana vipaumbele vyao kulingana na nafasi. Mfano golikipa, beki wa kati na mshambuliaji wanaangalia umbo sio kipaji pekeyake. Mtu mrefu kwenye maeneo hayo wao watamchukua halafu hivyo vitu vingine watamuongezea wenyewe.

Hatakiwi kuwa kama Messi awe na uwezo wa ku-control na kupasia ila faida ya umbo lake ndio wanaitaka kwa sababu unaweza kumfundisha mchezaji ku-control na kupasia lakini huwezi kumpa kimo.

Kwa sasa sehemu ya ushambuliaji ni kumalizia tu, mshambuliaji anatakiwa kujua ni eneo gani awepo kwa wakati ili apate nafasi ya kumalizia lakini pia anatakiwa awe anajua ni namna gani ataifanya timu yake ifike kwenye eneo la kushambulia

Kama mshambuliaji ana uwezo mzuri wa kumalizia hana haja ya kukimbia na mpira umbali wa mita 10 au 20, makocha wanachotaka timu ikishambulia mshambuliaji awe kwenye aneo ambalo akipewa mpira atafunga.

Kwetu bado tunafikiria mchezaji mwenye kufanya vitu vingi uwanjani ndio mchezaji mzuri. Ndio maana hivi karibuni Anthony wa Manchester United amekuwa akikosolewa kwamba, akiwa uwanjani utaona ana vipande vingi ambavyo vita-trend YouTube lakini hajaisaidia timu kwa lolote.
Screenshot_20230202_055135_OGInsta%2B.jpg
 
Suala la kimkataba imezigonganisha vichwa Yanga na Mdhamini wake Mkuu ambaye analaumu kitendo cha Yanga kwenda nje na makubaliano yao, kwa tafsiri sahihi ni kuwa Yanga ana Wadhamini wakuu wawili mpaka hivi sasa na hii inaweza kuwa rekodi kwenye historia ya mpira wa miguu duniani.

Mdhamini Mkuu anadai fidia juu ya hicho kilichotokea na bado inaiweza Yanga kwenye parandesi juu ya namna wanaendesha mambo yao.

Screenshot_20230202_055511_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm (kulia) akiteta jambo na kocha wa Al Hilal, Florent Ibenge katika uwanja wa Uhuru wakati Singida BS ikifanya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Simba Ijumaa Februari 3, Al Hilal itacheza na Simba Jumapili Februari 5.

Screenshot_20230202_055649_OGInsta%2B.jpg
 
TAASISI ya Utoaji wa Huduma za Afya ya Aga Khan, Tanzania (AKHST) imeingia makubaliano ya kutoa huduma za matibabu, mafunzo na uchunguzi wa afya kwa ujumla na klabu ya Azam kwa kipindi cha miaka miwili.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo, Februari Mosi, 2023 kwenye moja ya kumbi za mikutano za hospitali hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwahusisha Watendaji wakuu (CEO’s) wa taasisi zote mbili, Sisawo Konteh wa AKHST na Abdul Kareem ‘Popat’ wa Azam sambamba na viongozi wengine.

Mkataba huo unalenga kuimarisha uhusiano kati ya AKHST na Azam Fc, ukijikita zaidi kwenye kutoa huduma mbalimbali za matibabu katika vituo vyote vya AKHST vilivyopo nchini ikiwemo upimaji wa afya, upatikanaji wa huduma za maabara na mionzi, mafunzo, ukarabati na huduma za uchunguzi, uhamasishaji wa habari za afya na elimu, na mashauriano zaidi ya kitaalamu kwa wachezaji, benchi la ufundi na wafanyakazi wanaotambulika wa klabu hiyo.
Screenshot_20230202_055752_OGInsta%2B.jpg
 
Taarifa iliyoshtua wengi ni juu ya wadhamini wakuu wa Yanga kampuni ya SportPesa kulalamika hatua ya klabu hiyo kuingia mkataba na wadhamini wengine wakuu maalum lakini bosi mmoja amefafanua.

Bosi mmoja wa juu wa Yanga amesema wameshangaa hatua ya wadhamini wao wakuu SportPesa wakilalamika juu ya uamuzi wao, na kwamba mapema waliwatafuta kwa nyakati tofauti na kuwaeleza juu ya nia yao hiyo.

Amesema kila hatua ya kuingia mkataba wa mechi sita na kampuni ya vifaa vya Kielektroniki ya Haier waliwajulisha SportPesa ingawa hawakuonyesha kukubaliana na mdhamini huyo.
Screenshot_20230202_060032_OGInsta%2B.jpg
 
Uongozi wa SportPesa umetoa taarifa ya kusikitishwa na uongozi wa Yanga kukiuka makubaliano ya kimkataba na kuzindua jezi mpya zenye mfadhili mpya.
Yanga iliingia mkataba wa muda mfupi na kampuni ya Haier Jumatatu usiku ambapo walizindua jezi zitakazovaliwa kwenye mechi za kimataifa za Kombe la Shirikisho Afrika.

Screenshot_20230202_072355_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom