Makapuku Forum

Makapuku Forum

Farhan Jr

Wakati nasikia tetezi za Yanga kuhusu Mdhamini mpya kwa ajili ya michuano ya kimataifa nilipata shaka kidogo, kwakuwa niliwahi kupitia scenarios mbili kuhusu suala kama hili, nikapata ukakasi hata wa kupost hizi jezi mpya na sikupost kabisa.

Mdhamini Mkuu wa Real Madrid miaka ya 2009 huko ilikuwa Kampuni ya ubashiri ya Mtandaoni (siwezi kuitaja kwakuwa mkataba wangu hauruhusu) sasa ikatokea Madrid wana mechi ya FC Zurich ya Uswisi kwenye UEFA, ambapo Uswisi haendani na kanuni za Ulaya.

Uswisi hawaruhusu matangazo ya Kampuni za ubashiri za mtandaoni, hivyo Madrid na Mdhamini wake Mkuu ambaye alikuwa kifuani hawakupaswa kuvaa hizo jezi, Madrid wakawasiliana na Mdhamini wao mkuu juu ya sakata hilo.

Madrid hawakujiamulia nini cha kufanya, bali wakawasiliana na Mdhamini Mkuu ambaye akawaambia nendeni mkacheze bila Mdhamini kifuani, yani shati iwe plain Madrid wasiweke kitu chochote, kweli Madrid ilicheza hivyo.

Nikaja kuitazama na issue ya Yanga siku wanazindua jezi mpya na kutangaza Mdhamini mpya kwa ajili ya CAF, nilichoka sana kwakuwa binafsi sikuwahi kuona scenario kama hiyo popote duniani yani timu ina Wadhamini wakuu wawili kifuani? Haijawahi tokea.

Yes CAF wana mkataba na Kampuni nyingine ya ubashiri na ili kuondoa mgongano timu zote zenye Kampuni kama hiyo hazipaswi kuvaa betting, sasa ni lazima Yanga na Mdhamini Mkuu wakar chini kujadili.

Yanga anapaswa kumsikiliza Mdhamini Mkuu nini anataka kwakuwa ndie mwenye haki kama ambavyo hata Real Madrid walifanya, sasa Mdhamini Mkuu alitaka muweke VISIT TANZANIA ninyi ikawaje mkajiamulia vinginevyo? Ni aibu wakati mwingine vitu kama hivi.

SIMBA wana scenario kama hii na walitumia VISIT TANZANIA, sio kwamba hakuna Kampuni zilitaka kukaa kifuani la hasha! Ni kuwa Simba wanaheshimu mkataba wao na hata Mdhamini Mkuu wa Yanga amewasifia wazi wazi, najaribu kuwaza taswira ya Yanga mbele ya wadhamini, inafikirisha.

Screenshot_20230202_072520_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati mtaani watu wanasema kwenye mashindano ya kimataifa SportOesa hawatoi hela.

Kwenye mkataba wa Yanga SC na SportPesa katika hatua hizi za makundi, robo fainali, nusu fainali na fainali kuna bonasi kutoka Sportpesa kwenda Yanga SC iwapo watashinda mechi, kuingia robo fainali, kuingia nusu fainali, kuingia fainali na kuchukua ubingwa.

Sasa kama mdhamini analipia yote hayo na anakuambia hataki uweke kitu kingine hapo unawezaje kumkiuka?

Wakati mwingine tufanye mambo kisasa kidogo, nafahamu Yanga SC na SoortPesa walikuwa kwenye majadiliano Yanga wakiomba kutumia eneo ambalo SportPesa wanastahiki kuwepo kimkataba.

SportPesa wakakataa kwamba hawapaswi kufanya hivyo.

Kimkataba pia SportPesa wanahaki ya kusema nani awekwe hapo nani asiwekwe na kila upande unafahamu hilo.

Unabaki unajiuliza haya yametokeaje ili hali mkataba ni makubaliano ya kisheria ambayo yanapaswa kuheshimiwa na pande zote zilizomo kwenye huo mkataba?

Kuna mahala pana tatizo ingawa hatutaki kukubali na kusema ukweli.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
Screenshot_20230202_085135_OGInsta%2B.jpg
 
Baraza la Ulama katika kikao chake kilichofanyika February 01 na February 02,2023 Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Multi na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir bin Ally limetengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum kama Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam kuanzia leo February 02, 2023.

Wakati huohuo Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dr.Abubakar Zubeir bin Ally amemteua Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dares Salaam kuanzia leo February 02, 2023.
Screenshot_20230203_043048_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Furaha Kashe, aliyekuwa akiishi katika Kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha mwili wake umekutwa ukiwa umefukiwa kwenye shimo la choo kwa zaidi ya siku tatu huku Mume wake akidaiwa kuhusika.

Said Salumu Mwenyekiti wa Kijiji cha Migungani ambapo tukio hilo limetokea amesema Mume wa Marehemu alikuwa akimtishia Mwanamke huyo kumuua na alipotoweka nyumbani kwa siku tatu alimuuliza Mume wake bila majibu na walipoanza kuchimba kwenye mashimo yaliyopo kwenye nyumba hiyo waliukuta mwili huo ukiwa umezikwa.

“Mume wake alikuwa akimtishia kumuua na kisha kumfukia kwenye shimo, nikaamuru Wananchi wafukue mashimo yaliyopo kwenye nyumba hiyo na baada ya hapo waliukuta mwili huo kwenye shimo la choo na Polisi walimshikilia huyo Kijana hadi leo”
Screenshot_20230203_044938_OGInsta%2B.jpg
 
Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya tano (5) kwa ubora barani Afrika na ya 39 Duniani kwa mwaka 2022.
Screenshot_20230203_051014_OGInsta%2B.jpg
 
Watu ambao majina yao hayajafahamika wamevamia Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa na kulima mazao mbalimbali yakiwemo maharage huku Watembea kwa miguu na Waendesha vyombo vya moto wakitumia njia zilizopo uwanjani hapo kupita na kufanya shughuli zao hata kupelekea changamoto wakati wa ndege kutua.

@ayotv_ imemtafuta Kaimu Meneja wa Airport hiyo Deodatusi Sungura na amekiri uwepo wa Watu hao waliovamia uwanja kutokana na uwanja huo kutoendelezwa na nyasi zimekuwa zikikua hadi kusababisha vichaka uwanjani hapo.

"Siku ambazo ndege inatua hapa inatupa wakati mgumu kuzuia Watu ndege itue salama, siku za nyuma tuliomba Polisi watusaidie kufanya hiyo kazi wakaja wakawa wanakamata baadhi ya Watu kweli ikapungua baada ya hapo wakatoweka tukaendelea kupata changamoto ya Watu na vyombo ya usafiri kukatiza ndani ya kiwanja"

"Na hii inatukabili kutokana na uhaba wa Watumishi hapa tupo wachache, tunashindwa kumudu kuwadhibiti Watu wa Bajaji, Pikipiki, Watu wa mifugo inakuwa kazi"

Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Sumbawanga, wameiomba Serikali kuuendeleza uwanja huo kwani ni muhimu kwa uchumi wa Taifa “Serikali itusaidie kujenga Uwanja kama kwa wenzetu, sasa hivi hapa imekuwa ni njia tu ya Watu kukatisha kwa miguu, Bodaboda, Bajaji na hata Malori yanapita hapa”
Screenshot_20230203_051103_OGInsta%2B.jpg
 
PICHA: Muonekano wa Kituo cha Daladala ya Kinyerezi pamoja na barabara ya lami yenye urefu wa KM 7.1 inayoingia katika stendi hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.

Kituo hiki kinauwezo wa kuhudumia Daladala 90 kwa wakati mmoja na ujenzi wake umetekelezwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kupitia mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es salaam unaosimamiwa na TARURA.
Screenshot_20230203_051152_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesimama Bungeni leo na kutoa ufafanuzi na mwelekeo wa Serikali kuhusu changamoto ya nidhamu, malezi na adhabu zinazotolewa Shuleni, taarifa hii ameitoa ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa taarifa zenye kuonesha matukio mengi dhidi ya Watoto kwenye Jamii na Shuleni.

Majaliwa amesema Serikali haitafumbia macho wala kukubaliana na aina ya adhabu kali Shuleni na tayari Serikali imechukua hatua za kinidhamu kwa Wahusika Wakuu huku akiwakumbusha Mamlaka za Elimu nchini kuhakikisha utoaji wa adhabu Shuleni unazingatia waraka namba 24 wa mwaka 2002 ambao umeainisha utaratibu wa utoaji wa adhabu.

Majaliwa ameesema baadhi utaratibu uliotolewa kwenye waraka huo ni pamoja na adhabu kuzingatia ukubwa wa kosa, jinsia na afya ya Mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja, pia Mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko mkononi na Mwalimu wa kike isipokuwa Shule hiyo kama haina Mwalimu wa kike, adhabu ya viboko itakapotolewa iorodheshwe katika kitabu kilichotengwa kwa kuonesha jina la Mwanafunzi, kosa alilotenda, idadi ya viboko na jina la Mwalimu aliyetoa adhabu.

Aidha Waziri Mkuu ametoa wito kwa wanaopata matukio haya kuwasilisha taarifa kwa Mamlaka husika na sio kuyarusha kupitia mitandao ya kijamii jambo ambalo linaleta taharuki na kwamba lengo sio kuficha taarifa bali ni kuzuia chuki na uhasama ndani ya Jamii na sio kwa Walimu tu bali kwenye nyanja zingine za utumishi kama Afya n.k.
Screenshot_20230203_051431_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom