Makapuku Forum

Makapuku Forum

Vile itakavyokuwa siku nikimpa Shunie mkono😎😎😎
FkrpprUWABgIuNh.jpeg
 
Mahakama ya Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro imemuachia huru Askari Magereza wa Gereza la Mtego wa Simba, Samweli Mtelya baada ya kushinda rufaa aliyopinga kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka Mtoto wa Askari mwenzake (umri miaka 8) na hii ni baada ya vipimo vya Daktari kuonesha Mtoto huyo hajawahi kuingiliwa kimapenzi (Bikra).

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Paul Ngwembe ambaye amesema Mtuhumiwa huyo awali alishitakiwa kwa kosa la kubaka Mtoto wa miaka minane na kufikishwa Mahakama ya Wilaya Morogoro Agosti 11 mwaka 2021 kesi namba 27 /2021.

Baada ya kufikishwa Mahakamani April 25, 2022 Mahakama hiyo ya Wilaya ya Morogoro ilimkuta na hatia na kumuhumu kifungo cha maisha jela, baada ya hukumu hiyo Mtuhumiwa alikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro na kupewa kesi ya Rufaa Namba 67 /2022 .

Kesi hiyo ya Rufaa iliendeshwa Kwa muda wa miezi mitano ambapo Mahakama hiyo ilihitaji ushahidi zaidi kutoka Kwa Daktari Bingwa wa via vya uzazi ili Mwathirika huyo( Mtoto aliyebakwa) apimwe vipimo vya via vya uzazi kisha Daktari aliwasilisha taarifa ya vipimo mbele ya Mahakama na ilionesha Mtoto huyo hajawahi kuingiliwa sehemu zake za siri kwa namna yoyote ile(Bikra)

Hivyo basi baada ya kutolewa ushahidi huo Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Morogoro Paul Ngwembe leo amemfutia mashitaka Mtuhumiwa kisha kubadilisha hukumu ya kifungo cha maisha jela alichokua amehukumiwa awali na Mahakama ya Wilaya Morogoro na kumuachia huru.
Screenshot_20230202_045559_OGInsta%2B.jpg
 
Mfanyabiashara kutoka Sekta ya Viwanda nchini Nigeria Aliko Dangote, ambaye utajiri wake umeshuka kwa kiasi cha dola milioni 400 kufikia dola bilioni 13.5, bado ameendelea kuwa Mtu Tajiri zaidi kwa mwaka wa 12 mfululizo akifuatiwa na tajiri kutokea Afrika Kusini Johann Rupert ambaye anashikilia nafasi ya pili kwa mwaka wa pili mfululizo, licha ya kushuka kwa Dola Milioni 300 hadi kufikia Bilioni 10.7.

Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la Forbes, Watu matajiri zaidi Afrika wamepoteza USD Bilioni 3.1 wote kwa pamoja katika muda wa miezi 12, Mabilionea 19 wa kutokea Africa wana thamani ya wastani ya USD Bilioni 81.5 ikionesha kupungua kutoka USD Bilioni 84.9 mwaka mmoja uliopita.

Jarida la Forbes limemuorodhesha Mfanyabiashara kutokea nchini Tanzania Mohammed Dewji, akishikilia nafasi ya 13 kwenye list hiyo ya Watu Matajiri zaidi Afrika huku pia akionekana akishikilia nafasi ya 1,913 duniani akiwa na utajiri wa Dola Biliono 1.5, mwaka jana, Mo alishika nafasi ya 15.

Orodha ya Watu 15 Matajiri zaidi Africa ni 1.Aliko Dangote (Nigeria) - $13.5bn, 2.Johann Rupert (Africa Kusini) - $10.7bn, 3. Nicky Oppenheimer (Africa Kusini) - $8.4bn, 4. Abdulsalmad Rabiu (Nigeria) - $7.6bn , 5. Nasser Sawiris (Misri) - $7.3bn, 6. Mike Adenuga (Nigeria) - $6.3bn, 7. Issad Rebrab (Algeria) - $4.6bn, 8. Naguib Sawiris (Misri) - $3.3bn, 9. Patrice Motsepe (Africa Kusini) - $3.2bn, 10.Mohamed Mansour (Misri) - $2.9bn, 11. Koos Becker (Africa Kusini)- $2.6bn, 12.Strive Masiyiwa (Africa Kusini)- $1.9bn, 13.Aziz Akhannouch and family (Morocco) $1.5bn, 13. Mohammed Dewji (Tanzania) $1.5bn na 13.Youssef Mansour (Misri) $1.5bn.
Screenshot_20230202_050222_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230202_050242_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230202_050300_OGInsta%2B.jpg
 
Mwimbaji Peter Msechu @peter_msechu amebainisha kupungua kilo saba ikiwa ni siku 7 tu zimepita toka awekewe puto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila ili kumsaidia kupunguza uzito mwilini mwake.

Msechu ameelezea mafanikio hayo kwa furaha na kuonesha shauku ya kutamani kujua miezi sita kutoka sasa atakuwa katika hali gani kwani ndio utakua muda wa kulitoa puto hilo tumboni kwake "Niliwekewa puto January 25,2023 leo ni siku ya saba nimepunguza kilo 7 ina maana kila siku inazikwa kilo 1, Muhimbilii hii mmetisha, asante sana Mh. Rais wangu Dkt. Samia hii huduma umeileta Nchini kwetu hakika umekuja kunikomboa, asanteni sana Wizara ya afya kwa kuhakikisha mnajali afya zetu Watanzania, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu haki ya nani umetisha”

“Kipekeee kabisa asanteni Wataalamu wote na Madakatari kutoka Mloganzila, haki ya nani mmebadilisha maisha yangu tayari ndani ya wiki moja tu, Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili Profesa Janabi kongoleeeeeeee sanaaaaaaaa, nasema hivi hii ni wiki moja tu kilo saba je mwezi mmoja ? je miezi miwili? je mpaka nitakapolitoa mwezi wa sita?”
Screenshot_20230202_050433_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imesema kuwa uamuzi wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kutokutangaza Shule bora kwa kutegemea matokeo ya mwisho ya mitihani ni kwa sababu ya utata wa namna ya kutathmini Shule bora.

Ufafanuzi huo wa Serikali umetolewa Bungeni leo February 01, 2023 na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda baada ya mwongozo ulioombwa Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Mwita Getere.

Prof Mkenda ametoa mfano kuwa Shule yenye Wanafunzi 100 na nyingine ina Wanafunzi 20 waliomaliza kidato na nne, ya Wanafunzi 100, 70 wamepata A, 30 hawakupata A na yenye Wanafunzi 20 wote wamepata A, kwa kuangalia wastani wa ufaulu yenye Wanafunzi 20 itatangazwa kuwa Shule bora lakini wengine wanaweza kuona yenye Wanafunzi 70 wenye A ndio iwe Shule bora.

Prof. Mkenda amesema aina hiyo ya tathmini inaweza kupelekea shinikizo kwa Shule yenye Wanafunzi mathalani 100 kwa kuondoa wale 30 ambao hawakupata A ili iweze kutangazwa Shule bora kwa kupata A zote ambazo ni asilimia 100.

Mkenda amesema kuwa takwimu zote zipo hadharani lakini Baraza limejiondoa kwenye jukumu la kutangaza na hazijafichwa takwimu za matokeo ya Shule zote na ufaulu wake zipo.
Screenshot_20230202_050710_OGInsta%2B.jpg
 
"Mnadhani shule za Serikali zingekuwa zinaongoza wangeacha kutangaza, huu uwiano wa ufaulu ulianza tangu miaka ya 1990 mwishoni hadi juzi walipoitoa, nataka tujiulize walipoiweka baraza kabla ya kuitoa walikuwa wanalenga kitu gani na hicho kitu leo kimeyeyuka.

“Mitihani ni ushindani, ndiyo maana wanawaita watahiniwa na lengo ni mtu afaulu mitihani, huwezi kufaulu kama hujafanya bidii kwa maana hiyo unashindana ni ushindani' Suzan Lyimo - Mdau wa elimu
Screenshot_20230202_050933_OGInsta%2B.jpg
 
"Mfumo wa utangazaji wa matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ukurasa wa kwanza hadi 12 hauna tofauti.

“Ukitaka kuangalia ni shule ipi imekuwa ya kwanza hadi ya ngapi unaweza kuzipata kwa kuangalia GPA

“Tulipokuwa tukitangaza kwa kuweka watoto kumi bora kilichokuwa kikija kichwani ni kuwa tunaangalia namna uwekezaji katika sekta ya elimu inavyotofautiana.

“Ukiangalia shule 10 bora za Serikali mbili inakupa picha kuwa kadri unavyowekeza katika elimu ndiyo jinsi utakavyopata matokeo katika ufaulu na namna mtoto anachopata akiwa shuleni", Ochola Wayoga National coordinator Tenement.
Screenshot_20230202_051115_OGInsta%2B.jpg
 
“Hivi kweli sisi miaka yote tulikuwa hatujui kuwa tunashindanisha wasiokuwa sawa tulikuwa hatujui kweli, tulikuwa hatujui kuwa asilimia 100 ya watoto 30 katika namba halisi ni watu wachache kuliko asilimia 25 ya watoto 400.

“Kumsifia tu yule mwenye shule ya watoto wachache ambao wamefaulu wote daraja la kwanza na kumuacha huyu ambaye alikuwa na wanafunzi 400 na 120 au 125 wamefaulu.
“Si kweli kuwa wizara hii maprofesa na wataalamu wote waliokuwa wakiingia walikuwa hawalijui hili”

Waziri Kivuli wa Elimu ACT Wazalendo, Riziki Mngwali
Screenshot_20230202_051210_OGInsta%2B.jpg
 
"Tuliwahi kufanya uchambuzi wa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019, katika shule 100 zilizofanya vizuri shule za Serikali zilikuwa saba peke yake lakini uchambuzi ule tuliweza kufahamu shule hizi zinatoka mikoa gani na shule zilizoongoza katika mikoa ni ya ngapi kitaifa", Halili Letea Mhariri Takwimu Mwananchi
Screenshot_20230202_051542_OGInsta%2B.jpg
 
“Tulichokuwa tunaweza kukifanya kwa kupata madaraja ya ufaulu tulikuwa tunaweza kufahamu shule zilizofanya vizuri kwa maana ya umiliki yaani serikali au binafsi na jinsia za wanafunzi wanaofanya vizuri kupitia kumi bora.

“Kwa upande wa shule walizokuwa wanatoka ni shule mseto au shule ya wasichana au wavulana pekee au wote.
“Mara ya mwisho Necta kutoa rank ilikuwa ni matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa Mei 2022 na hii ya sasa ni mara ya tatu hawataji ranks” Halili Letea Mhariri wa Takwimu Mwananchi Communication
Screenshot_20230202_051634_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassoro Amduni amethibitisha kufungiwa kwa baadhi ya waamuzi kutokana makosa mbalimbali ya kujirudia kwenye Ligi Kuu.
.
Kauli yake ameitoa baada ya kuonekana taarifa mitandaoni ikieleza waamuzi 20, kati yao waamuzi wa kati 13 kuondolewa kwenye orodha katika michezo ya ligi iliyobaki na hawatakuwepo pia msimu ujao.
.
Licha ya kutotaja majina ya waamuzi na adhabu zao lakini taarifa zilizokuwa zikizagaa zinamtaja pia Emmanuel Mwandembwa, Hussen Athuman, Nassor Mwinchui, Florentino Zablon, Elly Sasii, Arajiga, Amina Kyando na Rafael Ikambi.
.
Waamuzi wa kati ni Jackson Palangyo, Hence Mabena, Hilbert Marine, Ahmed Simba wakati wa pembeni ni Mary Mwakitalama, Rashid Zongo, Hamis Chang’walu, Jesse Erasmo, Kassim Mapanga, Fredinand Chacha na Soud Lila.
Screenshot_20230202_052118_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom