Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mashabiki wa Ronaldo na Al Nassr taarifa iwafikie kuwa leo mmekubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Ittihad, kwenye nusu fainali huko Saudi Arabia.
Screenshot_20230127_042758_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Wigan Athletic imemfuta kazi rasmi Kocha wao Kolo Toure huku wakiamini maamuzi hayo yatawafanya wasalie kwenye Championship msimu ujao, kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo chini ya Kocha huyo.
Screenshot_20230127_043936_OGInsta%2B.jpg
 
Marcelo Bielsa amewasili nchini England ili kufanya mazungumzo na viongozi wa Everton juu ya kurithi mikoba ya Frank Lampard huku ikisemekana ametia ugumu kukubali dili hilo huku akitaka mipango yao kwanza.
Screenshot_20230127_044027_OGInsta%2B.jpg
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Gerald Kusaya amesema hawatawafumbia macho wanamichezo na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaotumia au kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Amesema kuna wanamichezo wanaotumia dawa za kulevya wakidai zinawasaidia kufanya vizuri kwenye tasnia hiyo.

Kusaya amesema wapo tayari kushirikiana na mashirikisho na vyama vya michezo nchini ili kudhibiti wanamichezo wanaotumia dawa za kulevya hususan Bangi.
Screenshot_20230127_044208_OGInsta%2B.jpg
 
TBT YA MSN NDANI YA BARCELONA (2014-17)

Messi: 153 goals, 66 assists
Suárez: 121 goals, 59 assists
Neymar: 90 goals, 46 assists

Utatu bora zaidi kwenye mpira wa miguu?
Screenshot_20230127_044408_OGInsta%2B.jpg
 
Mpenzi mpya wa Gerrard Pique baada ya kuachana na Shakira anaitwa Clara Chia Marti ambaye ana umri wa miaka 23, akiwa amezidiwa na Pique miaka kama 10.

Ni Mwanafunzi anayesomea Public Relation na ni moja kati ya wafanyakazi kwenye Kampuni ya Gwiji huyo iitwayo Kosmos.
Screenshot_20230127_044506_OGInsta%2B.jpg
 
SABABU LIGI KUCHEZWA KILA SIKU

Inawezekana unajiuliza kwa nini msimu huu 2022|23 mechi za Ligi Kuu zinachezwa karibu wiki nzima? Yaani kila siku kinapigwa!

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu @karim_boimanda ametoa ufafanuzi juu ya jambo hilo na kile ambacho kinasababisha mechi za Ligi Kuu kuchezwa karibu kila siku ya wiki.

“Ukiangalia hata kwa wenzetu, kuna ulazima mkubwa wa kufata matakwa au ushauri na maombi ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya Television.”

“Tunatamani mechi zote za Ligi Kuu ya NBC zioneshwe mbashara, mdhamini wa haki za matangazo ya Television anatamani kuona mechi zinaoneshwa kwenye channel moja.”

“Mtu akikaa kuangalia mechi kwenye television anaangalia mechi moja ikiisha anaangalia nyingine na sio mechi tatu au nne kuchezwa kwa wakati mmoja kwa sababu kuna watu wengine watakosa kushuhudia baadhi ya mechi.”

“Mdhamini mwenye haki za matangazo ananafasi kubwa sana kwenye hili jambo, ndio maana wamesaidia hata kuweka taa kwenye baadhi ya viwanja ili tuwe na machaguo mengi zaidi ya muda wa kucheza mechi za Ligi.”

“Ni kwa faida ya ukuaji wa Ligi yetu kwamba mechi zote zioneshwe mbashara ili hata mdau wa michezo akiamua kutazama mechi zote za Ligi Kuu awe na hiyo fursa.”

“Kwa hiyo ratiba ya mechi za Ligi kuchezwa karibu kila siku chanzo chake ni kuhakikisha michezo yote inaoneshwa mbashara na mdhamini mwenye haki za matangazo ya television ambaye ni Azam TV.”
Screenshot_20230127_045246_OGInsta%2B.jpg
 
NYUMA YA MUDA TULIWAHI KUWA NA HARUNA MOSHI BOBAN.

Imeandikwa na @jr_xavihernandez.

SIMBA wanae Clatous Chama kwenye eneo la kiungo mshambuliaji, Chama ni fundi wa mpira kweli anafanya kila kitu kwenye lile eneo anatimiza majukumu vyema akiwa kama kiungo mshambuliaji.

Tokea siku ya kwanza akiwa amevalia jezi ya Simba alianza kuimbwa kwa ufundi wake aliyoyafanya ni makubwa aliondoka lakini amerudi, Kwenye kiungo mshambuliaji yeye ni mwalimu mzuri, Achana na Mwamba wa Lusaka.

Zamani Simba waliwahi kuwa na kiungo mshambuliaji mwanadamu yule alikuwa fundi, Hakuwa anatokea Zambia,Ghana,Nigeria au Mali alikuwa ni fundi mmoja kutoka hapa hapa Tanzania tu.

Alifahamika kama Haruna Moshi miguu yake ilikuwa na ufundi ambao sitaweza kuuelezea ni kamaliza kwenye eneo la kiungo alipageuza kama nyumbani kwake utake nini Haruna Moshi asifanye.

Bukta yake ikiwa mlegezo lakini uwezo wake wa kuunganisha timu ulikuwa mkubwa sana pasi zake za kubembeleza kwa washambuliaji ile ball control,kufunga mabao vyote hivyo vikafanya apewe jina la Boban unamfahamu Boban?

Ukifika pale Italy, Waitaliano wenyewe walikuwa wanamuita Croatian Maestro ni Zvonimiri Boban fundi mmoja wa Croatia kwenye dimba la kati alichafua sana ni yeye aliyeiongoza Croatia kumaliza nafasi ya 3 pale Ufaransa wakati wa kombe la Dunia miaka ya 1998.

Haruna Moshi Boban aliingia kwenye ile Simba tamu ya Ulimboka Mwakingwe VCD,Joseph Kaniki Golota,Juma Kaseja ni 2004 hiyo. Haruna alijua kunyanyua watu majukwaani kwa ufundi wake mkubwa.

Mpira ulitumwa kila ulivyofika kwenye miguu ya Haruna,Akili yake ilijua nini cha kufanya kabla ya kupokea mpira kupoteza mpira haikuwa rahisi Haruna alikuwa kiungo kweli nyuma ya muda Simba walikuwa na mtu fundi sana.

Gefle If ya Sweden hawakusita kumsajili Haruna kutokana na ufundi miguuni mwake, Inawezekana angefanya makubwa kabla ya kina Samatta lakini haikuwa hivyo akarejea nchini.

Kwenye Simba ile yenye mapafu ya Patrick Mutesa Mafisango,juu kuna Afande Kazimoto. Haruna alikuwa kioo cha Simba wakina Okwi,Uhuru na Sunzu kazi zao ni kuuweka mpira wavuni tu. muda umetukimbia tuliwahi kuwa na Boban.
Screenshot_20230127_045338_OGInsta%2B.jpg
 
TFF KUMTANGAZA KOCHA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania [TFF] kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi Oscar Milambo limesema, litamtangaza Kocha wa Taifa Stars mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

Tangu kuondoshwa kwa Kim Poulsen mwezi Agosti, 2022 hakutangazwa mrithi wake badala yake alitangazwa Honour Janza kukaimu nafasi hiyo lakini pia aliondoka mwishoni mwa mwaka uliopita.

Oscar Milambo kupitia #SportsXtra amesema, wanatafuta Kocha anaeendana na mazingira ya nchi yetu ili kuepuka changamoto walizokutana nazo miaka iliyopita.

“Tupo kwenye huo mchakato wa kutafuta Kocha wa Timu ya Taifa na mchakato unaendelea, muda si mrefu sana tutaujuza umma tumefikia wapi na ni nani tunafikiri anaweza kuchukua hayo majukumu.”

“Tunafahamu na tayari tunaushahidi kwamba tumeshawahi kuwa na walimu na nini pengine kilisababisha hatukufikia malengo tuliyokuwanayo kama Shirikisho na kama nchi.”

“Tunajaribu kufanya hesabu vizuri ili mwalimu tutakaemtangaza tuwe tumejiridhisha kwamba hatutakutana na changamoto ambazo tumepitia siku za nyuma.”
Screenshot_20230127_045426_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia amesema Serikali imetenga hadi eka 10 kwa kila Kijana mwenye sifa za kufanya kilimo Nchini Tanzania ili kuiwezesha idadi kubwa ya Vijana wenye ari ya kufanya kilimo lakini wakakosa sifa zinazohitajika kwenye taasisi za fedha ili kupewa mikopo kwa ajili ya kilimo ambapo baadae watamilikishwa eka hizo.

Rais Samia ameyasema haya akijibu swali kuhusu namna ya kuvutia vijana kwenye kilimo, upatikanaji wa ardhi, teknolojia na fedha wakati wa ufunguzi wa mkutano unaohusu Kilimo unaofanyika Dakar nchini Senegal na kusisitiza kuwa Tanzania iko katika mchakato wa kupokea maombi kwa kundi la kwanza la Vijana watakaopata fursa ya kupata mafunzo ya miezi mitatu kuanzia katikati ya mwezi Februari ambapo watapewa ardhi hiyo.

Pamoja na Serikali kujizatiti, Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imetangaza kutoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 120 kwa ajili ya sekta ya kilimo ikiwemo umwagiliaji na kujenga kituo cha usafirishaji na usambazaji mbolea kwenye mpango huo unaowalenga Vijana na Wanawake ujulikanao kwa jina la BBT, 'Ujenzi wa Kesho Bora'.

Tangu kuanzishwa kwa mpango huo wa BBT miezi sita iliyopita tayari Tanzania imeweza kutenga jumla ya eka 600,000 kwa Nchi nzima ambapo pia tayari shughuli ya kusafisha mashamba hayo imeanza, taarifa zaidi kwenye
Screenshot_20230127_045537_OGInsta%2B.jpg
 
Jumuiya ya Afrika Mashariki imezindua rasmi Timu ya Wahakiki itakayotathmini utayari wa Somalia kujiunga na Jumuiya hiyo ikiwa ni hatua ya juu zaidi ya kuisajili Somalia ambapo Timu hii inajumuisha Wataalamu kutoka Nchi Wanachama na itakuwa Somalia ikitathmini maswala mbalimbali ikiwemo kufanya mapitio ya hali ya Somalia katika sheria za kimataifa pamoja na utayari wa Nchi hiyo kujiunga na umoja la forodha na itifaki ya soko la pamoja.
Screenshot_20230127_045630_OGInsta%2B.jpg
 
Marekani na Ujerumani zimetangaza kuwa zitatuma vifaru vya kivita nchini Ukraine ambapo Marekani itatuma vifaru 31 huku Ujerumani ikituma vifaru 14 ili kwa pamoja vikaisaidie Ukraine katika vita yake dhidi ya Urusi.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amelitembelea eneo la mafunzo ya kijeshi lililopo Mashariki mwa Ujerumani ili kuwatizama Wanajeshi wanaoshiriki katika mafunzo ya vifaru ambapo Nchi hii itaipa Ukraine vifaru 14 mwishoni mwa March 2023 ili visaidie vita yake na Urusi. #MillardAyoUPDATES
Screenshot_20230127_045742_OGInsta%2B.jpg
 
Marekani na Ujerumani zimetangaza kuwa zitatuma vifaru vya kivita nchini Ukraine ambapo Marekani itatuma vifaru 31 huku Ujerumani ikituma vifaru 14 ili kwa pamoja vikaisaidie Ukraine katika vita yake dhidi ya Urusi.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amelitembelea eneo la mafunzo ya kijeshi lililopo Mashariki mwa Ujerumani ili kuwatizama Wanajeshi wanaoshiriki katika mafunzo ya vifaru ambapo Nchi hii itaipa Ukraine vifaru 14 mwishoni mwa March 2023 ili visaidie vita yake na Urusi. #MillardAyoUPDATES View attachment 2496799
Cheupe uko vizuri!!
 
NYUMA YA MUDA TULIWAHI KUWA NA HARUNA MOSHI BOBAN.

Imeandikwa na @jr_xavihernandez.

SIMBA wanae Clatous Chama kwenye eneo la kiungo mshambuliaji, Chama ni fundi wa mpira kweli anafanya kila kitu kwenye lile eneo anatimiza majukumu vyema akiwa kama kiungo mshambuliaji.

Tokea siku ya kwanza akiwa amevalia jezi ya Simba alianza kuimbwa kwa ufundi wake aliyoyafanya ni makubwa aliondoka lakini amerudi, Kwenye kiungo mshambuliaji yeye ni mwalimu mzuri, Achana na Mwamba wa Lusaka.

Zamani Simba waliwahi kuwa na kiungo mshambuliaji mwanadamu yule alikuwa fundi, Hakuwa anatokea Zambia,Ghana,Nigeria au Mali alikuwa ni fundi mmoja kutoka hapa hapa Tanzania tu.

Alifahamika kama Haruna Moshi miguu yake ilikuwa na ufundi ambao sitaweza kuuelezea ni kamaliza kwenye eneo la kiungo alipageuza kama nyumbani kwake utake nini Haruna Moshi asifanye.

Bukta yake ikiwa mlegezo lakini uwezo wake wa kuunganisha timu ulikuwa mkubwa sana pasi zake za kubembeleza kwa washambuliaji ile ball control,kufunga mabao vyote hivyo vikafanya apewe jina la Boban unamfahamu Boban?

Ukifika pale Italy, Waitaliano wenyewe walikuwa wanamuita Croatian Maestro ni Zvonimiri Boban fundi mmoja wa Croatia kwenye dimba la kati alichafua sana ni yeye aliyeiongoza Croatia kumaliza nafasi ya 3 pale Ufaransa wakati wa kombe la Dunia miaka ya 1998.

Haruna Moshi Boban aliingia kwenye ile Simba tamu ya Ulimboka Mwakingwe VCD,Joseph Kaniki Golota,Juma Kaseja ni 2004 hiyo. Haruna alijua kunyanyua watu majukwaani kwa ufundi wake mkubwa.

Mpira ulitumwa kila ulivyofika kwenye miguu ya Haruna,Akili yake ilijua nini cha kufanya kabla ya kupokea mpira kupoteza mpira haikuwa rahisi Haruna alikuwa kiungo kweli nyuma ya muda Simba walikuwa na mtu fundi sana.

Gefle If ya Sweden hawakusita kumsajili Haruna kutokana na ufundi miguuni mwake, Inawezekana angefanya makubwa kabla ya kina Samatta lakini haikuwa hivyo akarejea nchini.

Kwenye Simba ile yenye mapafu ya Patrick Mutesa Mafisango,juu kuna Afande Kazimoto. Haruna alikuwa kioo cha Simba wakina Okwi,Uhuru na Sunzu kazi zao ni kuuweka mpira wavuni tu. muda umetukimbia tuliwahi kuwa na Boban.View attachment 2496795
unauandishi mzuri sana
 
Umoja wa Mataifa umetabiri ukuaji wa uchumi wa Ulimwengu utapungua kwa kiasi kikubwa hadi 1.9% mwaka huu.

@dw_kiswahili imeripoti kwamba Idara ya masuala ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa imesema kasi ya ukuaji wa uchumi kwa sasa Ulimwenguni imepungua kuanzia Mataifa yanayoendelea hadi yaliyoendelea, huku mengi yakikabiliwa na kitisho cha mdororo wa uchumi kwa mwaka huu wa 2023.

Ripoti ya Umoja huo ya kurasa 178 aidha imesema makisio ya ukuaji kwa mwaka huu ya asilimia 1.9, tofauti na asilimia 3 iliyokadiriwa mwaka 2022, ni ya chini mno kushuhudiwa katika miongo ya karibuni.

Hata hivyo imekisia ukuaji wa wastani wa hadi asilimia 2.7 mwaka 2024 ikiwa mfumuko wa bei na mtikisiko wa kiuchumi vitapungua.
Screenshot_20230127_045831_OGInsta%2B.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom