Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amewataka Wazazi ambao Watoto wao wanaingia Kidato cha Kwanza wahakikishe wanawapeleka Shule hata kama hawana sare (uniform) kwasababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Samia Suluhu Hassan ameshawalipia ada.

DC Godwe ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari ndani ya Wilaya hiyo, huku akigusia pia suala la uwepo wa vyakula Shuleni na umuhimu wa kuwa na Wasimamizi wa Kike kwenye magari ya Shule binafsi ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Watoto.

"Wazazi wote ambao Watoto wao wanaingia kidato cha kwanza wasijali hata kama Watoto hawana uniform hakikisheni Watoto wote mnawaleta Shule hatutaangalia kwamba hana uniform ama nini bali aje na mambo yatakwenda taratibu hatuwezi kusubiri mpaka kumkosesha Mtoto masomo wakati anaweza kuja na kuendelea na masomo, avae nguo zake za Shule ya Msingi aje”

Katika hatua nyingine DC Gondwe amewapongeza Wazazi, Walimu na uongozi wa Halmashauri ya Kinondoni kutokana na matokeo ya Kitaifa ambapo wilaya hiyo imeongoza nchi nzima na kuwa ya kwanza kwa kufaulisha shule ya Msingi kwa asilimia 98.53.
Screenshot_20230110_044556_OGInsta%2B.jpg
 
Timu ya Mlandege FC ya Viziwani Zanzibar imetinga fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitupa nje Namungo FC kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4.

Mchezo huo wa nusu fainali ya pili katika kombe hilo ulilazimika kwenda mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mlandege itacheza fainali dhidi ya Singida Big Stars iliyoitoa Azam FC kwa mabao 4-1.

FT: Mlandege FC 1-1 Namungo FC (Penalti 5-4)
Screenshot_20230110_044730_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imeshauriwa kufanya mabadiliko ya jina la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA) uitwe jina la mkoa husika (Mbeya) ili kuondoa mkanganyo kwa wageni wanaoingia na kutoka mkoani humo kwa shughuli mbalimbali.

Ombi hilo limetolewa leo Jumatatu Januari 9, 2023 na Spika wa Bunge ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson aliposhiriki kikao cha bodi ya barabara mkoa kilichoongozwa na mkuu wa mkoa, Juma Homera.

“Uhalisia wa viwanja vya ndege duniani ni lazima utaitwa jina la mahali husika kijografia au jina la mtu, huwezi kutumia jina la Songwe ambalo ni mkoa mwingine kwenye eneo la mkoa wa Mbeya, jambo hili linawachanganya watu wengi, hivyo unahitaji mabadiliko,” alisema Dk Tulia.

Screenshot_20230110_044927_OGInsta%2B.jpg
 
Kiungo wa Simba, Clatous Chama ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwezi Desemba akiwapiku John Bocco wa Simba na Fiston Mayele wa Yanga.

Chama alifunga mabao mawili na kuhusika katika mengine tano ndani ya mwezi huo.

Screenshot_20230110_045042_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' amekutana na wakuu wote wa Idara na vitengo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Muheza katika kikao alichokiitisha kwa wilayani humo.

Mbunge huyo amesema lengo kuu la kikao ilikuwa ni kuweka mikakati ya pamoja na kujadili changamoto zinazojitokeza kwenye majukumu ya kila siku ya kuwatumikia wananchi wa Muheza.

Waliohudhuria Kikao hicho wengine ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Sekretarieti ya CCM ya wilaya ikiongozwa na Katibu wa CCM wilaya, Simon Leng’ese.

Screenshot_20230110_045137_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha wa Simba, Juma Mgunda amechaguliwa kuwa kuwa kocha bora wa mwezi Desemba akiwapiku kocha Nasreddine Nabi wa Yanga na Hans Pluijm wa Singida Big Stars.

Mgunda katika mechi tano alishinda nne na sare moja.
Screenshot_20230110_045233_OGInsta%2B.jpg
 
Roberto Martinez ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa Ureno. Kocha huyo aliinoa Ubelgiji kwenye Kombe la Dunia 2022 wakiishia hatua ya makundi.

Martinez alijiuzulu nafasi ya ukocha kwenye timu ya Taifa Ubelgiji mara baada ya kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora katika kundi F, likiwa na timu za Canada waliotoka huku Morocco na Croatia zikisonga mbele.

Kocha huyo aliwahi kuifundisha timu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu England kabla ya kwenda kuinoa Ubelgiji.
Screenshot_20230110_045341_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka nchini Nigeria zimesema kuwa zaidi ya watu 30 wamevamiwa na kutekwa na kundi la watu wasiojulikana katika kituo cha treni nchini humo.

Jeshi la polisi nchini humo limesema waliotekwa ni abiria waliokuwa wakisubiri treni na kwamba wanaendelea kuwasaka wahusika wa tukio hilo.

Hadi sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na uvamizi huo.

Screenshot_20230110_045435_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameendelea na ziara yake katika mikoa ya Nyanda za Juu kusini ambayo ni Rukwa, Songea, Mbeya, Njombe, Iringa na Ruvuma.

Bashe amefanya ziara kwa siku mbili mkoani Mbeya ambapo ametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kukaguwa maghala ya kuuzi mbolea ya ruzuku, kutembelea mawakala wanaouza mbolea na skimu za umwagiliaji.

Katika ziara hiyo Bashe amesikiliza na kutatua kero mbalimbali za wakulima ikiwemo ya upatikanaji wa mbolea hiyo maeneo ya vijijini.
Screenshot_20230110_045544_OGInsta%2B.jpg
 
Staa wa soka, Gareth Bale 󠁧󠁢󠁷󠁬󠁳󠁿 ametangaza kustaafu soka Nyota huyo amecheza mechi za taifa lake Wales 111 pia amechezea klabu za Southampton, Tottenham Hotspurs, Real Madrid na LAFC.
Bale amebeba La Liga mara tatu, Supercopa mara 1, Champions League 5, European Supercup 3, Club World Cup 3, MLS Cup 1.
Screenshot_20230110_050122_OGInsta%2B.jpg
 
Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho amefichua juu ya dili lake na Yanga kabla ya kuangukia Simba na kufichua ameitisha kikao cha dharura na mabosi wake ili kuwapa mpango kazi wake na namna atakavyofanya kazi na mastaa aliokutana nao wakiwa Dubai.

"Unajua kabla ya kuja Simba niliwahi kufikia hatua nzuri kimazungumzo na Yanga ila mambo fulani ya msingi hayakwenda sawa, ndio maana nilishindwa kujiunga nao mwanzoni mwa msimu huu,”

Screenshot_20230110_050325_OGInsta%2B.jpg
 
KIKOSI cha Simba jana kimeanza mazoezi Dubai kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara na ile ya kimataifa, huku kocha mkuu mpya, Roberto Oliveira 'Robertinho' akisema anafahamu kila kitu kuhusu Yanga na kutamba hana presha nao kabisa.

Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kurejea kutoka Zanzibar, kocha huyo Mbrazili alifichua analijua soka la Tanzania na amekuwa akilifuatilia kwa ukaribu tangu akizinoa Rayon Sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na Vipers ya Uganda, hivyo anajua kila kitu kuhusu wapinzani na wataji wa jadi wa klabu aliyojiunga nayo, yaani Yanga.

Robertinho alisema anafahamu kuna ushindani mkubwa kwa michuano ya ndani ikiwemo upinzani wa timu yake ya sasa Simba dhidi ya Yanga kila zinapokutana na hata upinzani wa timu nyingine na kwamba alishajiandaa mapema kukabiliana nao hata kabla ya kuja kujiunga Msimbazi.

Kocha huyo mwenye falsafa za kujilinda na kushambulia kwa pamoja mwanzo mwisho, alisema kwa bahati nzuri Yanga anaifahamu hata kabla ya kuja Simba na aliwahi kuifunga mara kadhaa alipokutana nao tangu akiwa Rayon Sports ya Rwanda na hata msimu huu waliitungua kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi lililofanyika Agosti 6 mwaka jana.

"Naamini kuwepo wangu hapa nchini, unaifanya nitafahamu zaidi vitu vingi mbali ya wapinzani wetu Yanga, kwani imani yangu Simba itakuwa bora zaidi dhidi yao ikiwemo kupata matokeo bora kwa mechi zinakuja na hata kwenye ushindani dhidi ya wapinzani wengine," alisema Robertinho

Screenshot_20230110_050434_OGInsta%2B.jpg
 
Arsenal wamevaa jezi nyeupe kwenye mchezo wao dhidi ya Oxford ikiwa ni kampeni yao waliyoipa jina “No more Red” ikiwa ni vita dhidi ya unyanyasaji kwa watoto ambapo wanafanya hivyo kuunga mkono harakati dhidi ya vitendo hivyo.

Arsenal wakishirikiana na Adidas hutoa jezi hizo kwa Wanaharakati duniani wa haki za watoto, huwa haziuzwi bali hutolewa bure na msimu uliyopita walichapisha jezi 70 na kuzigawa zikiwa ni toleo maalum.
Screenshot_20230110_050630_OGInsta%2B.jpg
 
Golikipa Hugo Lloris ambaye pia ni Nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa ametangaza rasmi kustaafu timu ya taifa, Lloris aliitumikia Les Blues mara ya mwisho kwenye world cup 2022.
Screenshot_20230110_050804_OGInsta%2B.jpg
 
Nyota Joao Felix yupo mbioni kujiunga na Chelsea kwa mkopo akitokea Atletico Madrid kwa mujibu wa Mwandishi @fabriziorom ambapo mkopo huo utadumu mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Screenshot_20230110_050933_OGInsta%2B.jpg
 
Nyota Gareth Bale amestaafu rasmi soka akiwa na umri wa miaka 33, kwenye taarifa yake ameshukuru klabu zake zote nne alizocheza ambazo ni Southampton, Spurs, Real Madrid na LAFC pamoja na Wales.

Na hili ndilo kabati la Gareth Bale:

x Champions League
x La Liga
x Copa del Rey
x Supercopa de España
x UEFA Super Cup
x FIFA Club World Cup
x MLS Cup
Screenshot_20230110_051228_OGInsta%2B.jpg
 
Moja kati ya nyota tegemeo kwa timu ya taifa ya Argentina (Wanawake) ni Yamila Rodriguez ambaye ana tattoo ya Cristiano Ronaldo kwenye mguu wake wa kushoto.

Alipoulizwa kwanini ana mchoro wa sura ya Ronaldo kwenye mguu alimjibu Mwandishi kuwa kwake yeye Wachezaji wake bora wa muda wote ni Cristiano Ronaldo na Diego Maradona.
Screenshot_20230110_051323_OGInsta%2B.jpg
 
Ureno imemtangaza Kocha Roberto Martinez kuwa mrithi wa Fernando Santos ambaye ndie alikuwa Kocha wa timu ya taifa Ureno.

Martinez ambaye hakuwa na nyakati nzuri kwenye World Cup akiwa na Ubelgiji ataripoti jijini Lisbon kuanza maisha mapya.
Screenshot_20230110_051549_OGInsta%2B.jpg
 
Nimeona taarifa ya Mwenyekiti wa kamati ya Mapinduzi Cup akizishutumu Simba na Yanga kwa kuchezesha au kupeleka vikosi ambavyo vinatajwa kuwa ni dhaifu na hivyo kutolewa mapema kwenye michuano.

Hiyo imetafsiriwa kama Kariakoo Giants hawaiheshimu michuano ya Mapinduzi, lakini mimi nina mtazamo tofauti nadhani sisi tuchague kuheshimu mpira wa miguu, nchi yetu ina timu nyingi sana ambazo bado zinaweza kuonesha mpira mzuri.

Changamoto tuliyonayo kama taifa ni kuwa tunaamini Simba na Yanga ndio mpira, lakini tuna ligi ya Simba na Yanga tu? Nawaza kama bara na visiwani zipo tu timu mbili jibu ni HAPANA, basi tufikirie kwa utofauti ili kuwa na maisha nje na Simba na Yanga.

Bado tutoe nafasi kwa mawazo mapya na kuifanya michuano hii sio tu mpira bali package ya experience, tuifikirie kwenye jicho la kiuchumi na kiutalii pia, tuikifirie kama mtoko na sio sehemu ya watu kutazama tu mpira.

Tuwaze nje ya box, tiketi zenye thamani ya kutazama mpira lakini bado ikaunganishwa na utalii ambapo kwa Watanzania gharama zake sio kubwa, hatuoni tutavuta audience kubwa zaidi? Tugeuze mpira kuwa experience.

Email ziwe wazi na Kamati ziwe tayari kupokea maoni, naamini tutapata njia nzuri ya kuinogesha zaidi michuano hii.
Screenshot_20230110_051715_OGInsta%2B.jpg
 
Ukiisoma taarifa ya TFF kuhusu sakata la Feisal Salum wamesema kwanza FEISAL ni Mchezaji wa Yanga halali tena kimkataba.

Paragraph ya pili imesema uamuzi kamili utatolewa kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika kwenye shauri hilo utatolewa Januari 9, ambayo ndio leo.

Pande mbili za kupewa taarifa ni zipi? Ni YANGA na FEISAL SALUM wala sio Umma, hivyo sisi kama Umma taarifa yetu ni kuwa Feisal ni Mchezaji wa Yanga, kivipi Mchezaji wa Yanga basi hizo pande mbili zina taarifa kamili.

Au pande mbili za shauri hilo sisi Umma tupo upande upi??

Na ndio maana hatuoni ufafanuzi wowote tena kwenye page za TFF.

Screenshot_20230110_052034_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom