Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230107_063437_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230107_063452_Opera%20Mini.jpg
 
Wakala Ya Barbara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam umetoa taarifa kwa Watumiaji wa Daraja la Tanzanite kuwa uwekaji wa nembo ya Tanzanite umekamilika na Daraja limefunguliwa Jumapili tarehe 8 Januari 2023 saa Saba (7) Mchana.

“TANROADS Mkoa wa Dares Salaam inawashauri Watumiaji wa Daraja hilo kuendelea kulitumia kwa kuzingatia alama za usalama Barabarani na utunzwaji wa miundombinu adhimu ya daraja hili, tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza wakati wa uwekekaji wa nembo ya Tanzanite”
Screenshot_20230109_035725_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Kibondo hadi Mabamba yenye urefu wa KM 47.9 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami utaanza rasmi baada ya kusainiwa kwa mkataba huo wa ujenzi.

Mkataba huo umesainiwa Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativiila na Mkandarasi Chico leo January 08,2023.

Barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Kigoma na Kagera, Geita na nchi ya Burundi.
Screenshot_20230109_035906_OGInsta%2B.jpg
 
Kamati ya Kulinda Wanahabari (CPJ) pamoja na Wanaharakati wengine kote Duniani wameendelea kupaza sauti kutaka Waandishi sita wa habari nchini Sudan Kusini waachiwe baada ya kukamatwa kutokana na kusambaa kwa picha za video zinazomuonesha Rais wa Nchi hiyo, Salva Kiir akitokwa na haja ndogo.

Video hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii December mwaka jana ilimuonesha Rais Kiir akitokwa na haja ndogo hadharani huku wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye hafla.

Wafanyakazi sita kutoka Shirika la Utangazaji la Serikali la Nchi hiyo (SSBC) wamekamatwa Wiki hii, Wafanyakazi hao ni Joval Tombe (Control Room Director), Victor Lado (Camera Technician), Joseph Oliver, Jacob Benjamin na Mustafa Osman (Camera Operators) pamoja na Cherbek Ruben (Control Room Technician) .

Rais wa Muungano wa Wanabari Sudan Kusini, amesema Waandishi hao wanashukiwa kufahamu video hiyo ilivujaje, SSBC imesema video hiyo haikuoneshwa kwenye kituo hicho.
Screenshot_20230109_040008_OGInsta%2B.jpg
 
Nyani ambao wamekuwa ni kero kwa muda mrefu katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameanza kuondolewa kwenye makazi ya wananchi kwa kupigwa risasi baada ya jitihada za kuwafungia kengele na kuwawekea mitego kushindikana.

Nyani hao ambao wamekuwa wakitembea makundi kwa makundi wanadaiwa kuwa ni tishio katika wilaya hiyo kutokana na wingi wao, ambapo wamekuwa wakila mazao shambani, mifugo ikiwemo mbuzi, kuku na kuhatarisha usalama wa watoto.

Hali hiyo pia imesababisha baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na kulazimika kuyakimbia mashamba yao kutokana na nyani hao kula mazao yao kila mwaka na hawavuni chochote.

Akizungumzia leo Januari 8 katika operesheni ya kuwaondoa nyani hao, Mbunge wa Rombo ambaye ni Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuchukua hatua madhubuti ya kuwaondoa nyani hao, kwani wamekuwa ni kero ya muda mrefu.
Screenshot_20230109_040207_OGInsta%2B.jpg
 
Watu 40 wamefariki dunia na wengine 87 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana huko Kaffrine, Senegal.

Rais wa Senegal, Macky Sall ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia ajali hiyo iliyochukua uhai wa watu 40 na kuwaacha 87 majeruhi.

Rais Sall amesema Serikali itakutana kesho Jumatatu kuchukua hatua madhubuti za kuboresha usalama barabarani kufuatia ajali hiyo ambayo ilikuwa mbaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Screenshot_20230109_040404_OGInsta%2B.jpg
 
Idadi ya watu wanaopoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Malawi imezidi kuongezeka kutoka watu 661 hadi kufikia vifo 687.

Kupitia taarifa iliyotolewa Jumamosi Januari 7,2023 kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Waziri wa Afya nchini Malawi Khumbize Chiponda Januari 5 tayari kulikuwa na vifo 661 na kufikia Januari 7, watu 687 wamepoteza maisha.

“Katika saa 24 zilizopita, kumeropotiwa maambukizi mapya 427 na vifo vipya 13 na watu tisa wanashukiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo,
Tayari maambukizi yameriopotiwa katika wilaya Blantyre watu 100, Mangonchi 79, Lilongwe 60, Machinga38 Balaka 36, Salima33, Dedza 16, Dowa 15, Zomba 13, Thyolo 9, Mulanje 6." Alisema Waziri Chiponda.

Mbali na wilaya hizo Waziri huyo ametaja wilaya zingine kuwa ni”Kasungu yenye maambukizi 5, Likoma 4, Neno 3, Phalombe 3, Nkhotakota2, Karoga 2, Mchinji 1, Chiradzulu 1 na Ntcheu 1.

Amebainisha kuwa hadi Januari 7 watu 20,527 wamekumbwa na ugonjwa huo nchini humo huku watu 19,031 wakirejea katika hali zao na wengine 809 wakiwa kwenye matibabu huku akiweka wazi kwamba hospitali zote za wilaya nchini humo zimeripoti kupokea wagonjwa wa kipindupindu.

Screenshot_20230109_040506_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mwisho wa mwezi huu Serikali inatarajia kutangaza bei mpya za vifurushi vya simu, ili kila Mtanzania amudu kuvitumia.

Nape alisema Serikali inakamilisha mapitio ili kuona namna ya kusaidia kupunguza gharama ili mwananchi wa kawaida apate huduma bila tatizo.

Hata hivyo alisema wizara hiyo kwa kushirikiana na kampuni za simu za mkononi inatafuta namna ya kuwapatia simu wananchi kwa mkopo ambapo watalipa kidogokidogo huku wakiendelea kutumia.

“Mtu wa kawaida kununua simu ya Sh300,000 ni ngumu kidogo, lakini tukimwambia weka elfu thelathini upewe simu ya laki tatu, atakuwa anakatwa kidogokidogo hata kama ni kwa mwaka mzima itawezekana,” alisema Nnauye.

Screenshot_20230109_040645_OGInsta%2B.jpg
 
Mvuto wa nywele kwa mwanamke hutokea pale zinapobanwa au kuchanwa katika mitindo tofauti.
Nywele kama ilivyo kwa viungo vingine zinahitaji matunzo makubwa ili kuzifanya zionekane zenye mvuto na kupendeza wakati wote.

Zipo njia mbalimbali za kutunza nywele, lakini matumizi ya zana na vifaa vya asili vina uwezo mkubwa wa kujaza nywele na kuzirefusha kwa kiasi kikubwa.

Leo tutaangalia namna ya kujaza nywele kwa kutumia parachichi, yai na asali ambavyo vyote vinatengenezwa mchanganyiko ambao ni rutuba kwa nywele.

Namna ya kutengeneza
Chukua parachichi lililoiva, kata katika vipande vidogo vidogo, kisha vunja yai na uchote kiini uweke pamoja na vipande vya parachichi.

Mimina asali katika mchanganyiko wa parachichi na kiini kisha koroga mpaka vilainike na kuchanganyika kabisa kupata rojorojo.

Baada ya kupata mchanganyiko huo safisha nywele zako kwa maji ya uvuguvugu,kausha kwa taulo au kitambaa safi kisha paka mchanganyiko huo kwa kukata mistari na kuhakikisha nywele zote zimekolea.

Kaa na mchanganyiko huu kichwani kwa muda wa dakika 15 mpaka 20 kisha safisha tena kwa maji safi.

Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele zako.

Screenshot_20230109_041143_OGInsta%2B.jpg
 
Sekta ya utalii nchini imeendelea kuimarika baada ya athari za janga la Uviko-19, ambapo mwaka 2022 watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.29 ikilinganishwa na watalii 922,692 waliokuja nchini mwaka 2021.

Ongezeko hili la watalii ni asilimia 71.02 kuanzia Januari hadi Novemba 2022, ambapo Serikali imeweka lengo kuwa ifikapo mwaka 2025 ipokee watalii milioni tano kwa mwaka na mapato kufikia Dola bilioni 6.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana alitoa taarifa hiyo jana, katika mkutano wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) wa mashauriano baina ya sekta binafsi na sekta za umma katika sekta ya utalii.

Dk Chana alisema ongezeko hilo la watalii limetokana na jitihada za Serikali na wadau wa utalii, zikiwemo kukuza, kuendeleza na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa kutumia Programu ya ‘The Royal Tour.’

Screenshot_20230109_041248_OGInsta%2B.jpg
 
Azam FC imepokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars yote manne yakifungwa na nyota wao mpya Francy Kazadi huku la Azam likifungwa na Abdul Sopu mechi ya kwanza nusu fainali Kombe ka Mapinduzi. Singida Big Stars tayari anatangulia fainali huku anasubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili Namungo vs Mlandege
Screenshot_20230109_041421_OGInsta%2B.jpg
 
Singida Big Stars imefanikiwa kupata saini ya kiungo Kelvin Nashon akitokea Geita Gold. Nashon leo ameanzia benchi katika mechi ya nusu fainali Mapinduzi Cup dhidi ya Azam FC

Screenshot_20230109_041539_OGInsta%2B.jpg
 
Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi rasmi kikiwa Dubai huku kocha mpya Robertinho akianza kazi yake na mastaa hao ambao watatumika katika mechi za Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Azam Shirikisho.
Screenshot_20230109_041637_OGInsta%2B.jpg
 
WAKATI sakata la kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' jana likitolewa maamuzi na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji, mshambuliaji nyota wa Mtibwa Sugar, Adam Adam ameandika barua ya kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliobaki klabuni hapo.

Fei aliburuzwa na Yanga katika kamati hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuvunja mkataba kwa kulipa Sh112 milioni ambazo hata hivyo zimerudishwa na jana maamuzi yalitoka na kuamuliwa bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Lakini kwa Adam amewaomba waajiri wake kuvunja mkataba ili akatafute changamoto sehemu mpya na taarifa ambazo Mwanaspoti limepenyezewa na mtu wa karibu wa mchezaji huyo zilieleza kwamba ni kweli amefikia uamuzi huo ingawa bado viongozi wake hawajajibu chochote kuhusu hilo.

"Ni kweli anataka kutafuta changamoto kwenye timu mpya ingawa bado uamuzi wa mwisho juu ya hilo haujafanyika," kilisema chanzo hicho ambacho hata hivyo hakikutaka kuwekwa wazi.
Kwa upande wa Adam, alipotafutwa na Mwanaspoti alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sasa.
"Kama kutakuwa na jambo lolote jipya ambalo linanihusu basi mashabiki wangu watajua tu," alisema.

Screenshot_20230109_041738_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya Rais wa shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF) kusema mbaya kuhusu Zinadine Zidane kuwa hajali kuhusu Zizzou na hata angepiga simu kuomba nafasi ya Ukocha Les Blues asingepokea simu yake, nyota Kylian Mbappe ametweet kumpasua Rais wake.

Nanukuu “Zidane ni Ufaransa, hatupaswi kumvunjia heshima Legend kwa namna hiyo”

Mbappe amepongezwa na watu wengi sana juu ya hatua hiyo.
Screenshot_20230109_045438_OGInsta%2B.jpg
 
Tuna matatizo yale yale kwakuwa tuna Wachezaji wale wale.

- Thomas Tuchel, aliewahi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea.
Screenshot_20230109_045655_OGInsta%2B.jpg
 
FRANCY KAZADI

Inaitwa Poker hiyo, kaweka nne peke yake mbele ya Azam FC.
Screenshot_20230109_045814_OGInsta%2B.jpg
 
Kama Manchester United wanamtaka Weghorst wanapaswa kuwasiliana kwanza na Burnley ambao ndio wenye Mchezaji kisha wao watatutaarifu sisi, kama tutakubali basi ndipo tutavunja mkataba wake wa mkopo ila nje na hapo watapaswa kutulipa fidia au asalie hapa mpaka mwisho wa mkopo wake.

- Kazanci, Mkurugenzi wa Besiktas akijibu suala la Man United kumtaka Mchezaji ambaye yupo kwao kwa mkopo.
Screenshot_20230109_045918_OGInsta%2B.jpg
 
RIYAD Mahrez dhidi ya Chelsea msimu huu:
.
3 Mechi
️ 4 Mabao
.
FT: MAN CITY 4-0 CHELSEA
Screenshot_20230109_050236_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom