Farhan Kihamu
Baada ya majibu ya Kamati imeonekana wengi wanadai haki haijatendeka, maswali mengi nayojiuliza ni kuwa ili haki iwe imetendeka basi ilipaswa Yanga kuonekana imeshindwa? Bado kuna ukakasi kwenye tafakuri ya hili suala.
Maisha ya mpira wa miguu au hata taasisi yoyote watu huja na kuondoka ila taasisi zinasalia, sidhani kama Yanga wanamlazimisha Kiungo Maestro asalie kwenye timu yao bali wao wanataka taratibu tu zifuatwe, DEJAN ALIONDOKAJE SIMBA? Mnakumbuka?
Yanga ni klabu ambayo ina Wanachama na Mashabiki wake ambao wamechagua Viongozi kuwawakilisha kwa niaba yao, Yanga pia ina wabia kibiashara ambao wanataka kuona sura safi ya taasisi ambayo wameweka pesa zao, ulitarajia wakubali vitu viende kienyeji?
Mimi kama ningekuwa Mshauri wa Feisal najua ni ngumu yeye kuweka wazi timu ipi inamtaka kwakuwa FIFA wana mtego wa INFLUENCE OF THIRD PARTY yani shinikizo kutoka pande flani ndio maana huwezi kuona timu inayomtaka ikajitokeza ila kuna room ya Feisal na Yanga kuifikia.
Kwakuwa Feisal ana mkataba na Yanga kwa mujibu wa Kamati basi aende tu kuomba value yake pale Jangwani, watampa thamani yake halisi kwakuwa Feisal wa 2020 hawezi kuwa na value ile ile kwasasa kisha Kijana akasake maisha yake kwa kudeposit mzigo watakaosema.
Leo hii tutashangilia kwakuwa lipo Yanga ila kesho linaweza kutokea Simba, Mtibwa au Namungo kuwa Mchezaji kaamka tu anasema hana furaha na anahisi kuteswa hivyo anavunja mkataba na kuondoka, HAPANA vitu haviendi hivyo.
Kulipwa kidogo tofauti na wengine sio dharau kwakuwa kila Mtu ana namna yake ya kujadili mikataba yake, labda kutopewa gari sio dharau ukirejea kwenye mkataba kuna sehemu mliahidiana hivyo? Sio suala la kutokuwa na furaha bali suala na kimkataba mmekubaliana vipi.
Kila Kijana wa Kitanzania anamtakia heri Feisal na tunapenda kuona wenzetu wakipata maslahi mazuri sana ila mwisho wa siku kuwa na Menejimenti sahihi ambao watakupa thamani yako sahihi, mpira umebadilika sana kinachoandikwa ndicho kinapaswa kutekelezwa.
Tupo wengine ni Freelancers, wapo wengine wanalipwa ujira mdogo tu ila mwisho wa siku ni makubaliano yenu tu.