Farhan Jr
Nimeona post ya Kaka angu Priva kuwa niombe radhi kwakuwa amehisi nimedharau tuzo aliyoshinda Fiston Mayele kutoka kwenye page moja nchini Kongo, sijaelewa kwanini niombe radhi ikiwa sijadharau tuzo hiyo.
Niombe radhi kwasababu nimesema ulichopost kwenye page ya klabu kilipaswa kuhitimishwa vyema? Kuwa Fiston Mayele ni Mchezaji bora wa Kongo kwa mujibu wa page flani huko kwao?
Page rasmi ya klabu imepost taarifa sahihi lakini sio kamili, MVPs wawili kwa maana ya Aucho na Mayele kwa context ile wametokana na page za mitandaoni, malizia tu statement hapo kuna shida gani? Priva napaswa kuomba radhi?
Tazama hata page za timu za Ulaya kama Mchezaji ameshinda tuzo ya FWA (Football Writer’s Association) watatoa credit, akishinda BBC Sports Personality watatoa credit, iwe Ballon au FIFA Best Men watatoa credit, Priva kama hizo tuzo ni kubwa na zina uzito huo kwanini hamjamalizia taarifa?
A simple logic tu Kaka angu, page nyingine Rwanda ikitoa tuzo, Kenya ikatoa, Tanzania, Namibia, Zambia hizo zote mtapost? Ndio maana kuna tuzo zinazofahamika na Mashirikisho pamoja na klabu na ndio hizo zinachapishwa kwenye kurasa zao, simple logic Kaka.
Umeitaja Ballon dor kikawaida sana yani kama vile kitu chepesi ila nenda kasome vizuri asili ya hizo tuzo, kasome vyema Waandishi wawili waanzilishi wa hizo Gabriel Hanot na Jacques Ferran, kisha kafuatilie Pioneers wa European Cup ni wakina nani, Euro Cup ilianza 1955 na hizo tuzo zikaja 1956.
Halafu kapitie tena kuhusu Ballon dor ya French Football Magazine, imeanza 1956 ifuatilie vyema Ulaya kama walikuwa na tuzo zaidi ya hizo, kisha nenda mpaka 1995 walibadili nini kisha fika tena miaka ya 2010 FIFA wakaomba nini kutoka kwao, kisha uje uconnect na unachosema.
Ukaitaja BBC na tuzo zao kirahisi sana, lakini pia tulia nenda kawasome vyema BBC, fuatilia panel inayokaa kuteua majina shindani, fuatilia wana blessings gani kutoka vyombo vya mpira kisha uje hapa tuzungumze vyema Kaka angu.
Halafu mwisho Bro angu kafuatilie utofauti wa MAGAZINE, Newspaper na hiyo page ya tuzo, nitaomba radhi baada ya hapo, nitachutama kama ulivyosema ukishakuja na hizo content.