Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230104_045536_OGInsta%2B.jpg
 
Staa wa Soka wa Ureno Cristiano Ronaldo leo amepokewa rasmi na ametambulishwa mbele ya mashabiki wa Club ya Al Nassr ya Saudi Arabia.

Ronaldo aliyejiunga na Al Nassr kama Mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Man United aliambatana na Familia yake kwa maana ya Watoto na Mpenzi wake Georgina Rodriguez.

Timu ya Al Nassr iliyomsajili Ronaldo na Club ya Newcastle ya England zinamilikiwa na Mmiliki mmoja na inadaiwa kuwa katika mkataba wa Ronaldo kuna kipengele cha kwenda Newcastle kwa mkopo kama watafuzu kucheza UEFA Champignons League.
Screenshot_20230104_055108_OGInsta%2B.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza ongezeko la nauli mpya za Mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam, nauli hizo zimeongezeka kwa Tsh. 100 kutoka nauli za zamani ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika siku kumi nne toka tarehe ya kutangazwa kwa taarifa hii.

Akitangaza nauli hizo leo Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo amesema nauli ya mabasi yaendayo haraka kwa njia kuu (truck route) ni Tsh. 750 kutoka Tsh. 650, njia ya mlisho (feeder router) ni Tsh. 500 kutoka Tsh. 400, njia ya mlisho na njia kuu (feeder +truck route) ni Tsh. 900 kutoka Tsh. 800 na njia ya kimara kwenda Kibaha ni Tsh. 700 badala ya pendekezo la DART la Tsh.1200.

Hata hivyo, Latra imepinga ombi la DART kuongeza nauli kwa Wanafunzi na hivyo imebaki Tsh. 200 iliyokuwepo.
Screenshot_20230104_061652_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia amemteua Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Masoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Screenshot_20230104_061826_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Dkt. Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania Mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Katanga anachukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambae uteuzi wake umetenguliwa.

Balozi Katanga amewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini Japan.
Screenshot_20230104_062001_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Dkt. Samia amemteua Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Kabla ya Uteuzi huo Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Screenshot_20230104_062454_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasssan amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania, Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu akichukua nafasi ya Moses Kusiluka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Screenshot_20230104_062610_OGInsta%2B.jpg
 
Kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji ya TFF imemuita Mchezaji Feisal Salum kwenye kikao kesho January 4, 2023 baada ya Yanga kupeleka malalamiko yake ya kimkataba dhidi ya Mchezaji huyo, haya yamejulikana baada ya barua ya wito huo wa TFF kuvuja mitandaoni.

Feisal anaripotiwa kuvunja mkataba na Yanga kwa kutumia kipengele kilichopo kwenye mkataba wake cha kuvunja mkataba kwa kurudisha Tsh milioni 112 ambazo ni pesa ya usajili na mishahara ya miezi mitatu.

Yanga bado hawajakubaliana na namna Feisal alivyovunja mkataba wake japokuwa kwa sasa zipo fununu kuwa Feisal amepelekwa Dubai na Mmiliki wa Azam FC Yusuf Bakhressa kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kujiunga na Azam FC.
Screenshot_20230104_062743_OGInsta%2B.jpg
 
Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara leo wakati wa mazungumzo yake na Viongozi Wakuu wa Kisiasa Ikulu Dar es salaam.

Akiwa Ikulu Rungwe amesema “Tumeanza mwaka kwa tangazo zuri sana, Rais ametuita tumekula ubwabwa kwanza na tumepata matangazo yake ni faraja sasa tutakwenda kufanya mikutano ya hadhara bila vizuizi na wale Polisi sio tena wa upande mmoja watakuja kutulinda wote, ni jambo la kufurahisha"

"Tumeondoka zile zama za kutishana, hawa Chama tawala, Vyama vingine hawavijui ili ni jambo jema ngoja tukaone utekelezaji wa vitendo unakuwaje, maana Rais amesema ila uelewa unatofautiana, huko kwenye vitendo tutaona Polisi wameelewa vyake na sisi tumeelewa vyetu huko kwa Wananchi tutaona"

"Hii siku imechelewa sana tulikuwa tunaingojea sana, tuwe huru tuondokane na zile zama za kwamba Mimi nimeshasema"

“Kuhusu Tanzania kukopa nje ya Nchi sio jambo baya tangu zamani, Mtu anakopa ili kile anachokopa akakifanyie kazi, Watu wanalalamika kwamba mikopo mbona imekuwa mingi na Wananchi hali zao mbaya za maisha nafikiri wangekopa wakaangalia Wananchi kwanza sababu ukisema tu unajenga reli sasa Mtu atakula reli?"
Screenshot_20230104_063312_OGInsta%2B.jpg
 
Eliza Mlimbila (17) Mkazi wa Mtaa wa Sigridi uliopo Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe amekutwa amefariki katika Mtaa wa Kahawa baada ya kubakwa, kulawitiwa na kukabwa shingo siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Baba mzazi wa Marehemu anayeitwa Meshack Mlimbila amesema Mtoto wake ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana (2022) alichelewa kurudi nyumbani siku ya jumamosi ya December 31 na alipoulizwa alikuwa wapi aliondoka tena bila kuaga mpaka alipopata taarifa za kifo chake siku ya mwaka mpya.

“Jumamosi tumetoka shambani hatukumkuta nyumbani mpaka saa tatu, aliporudi nikamuuliza lakini alivyotokatoka sikuelewa tena na kwa sababu alikuwa anaweza kutoka na kurudi, mpaka mauti unamkuta sielewi alikuwa wapi,mara kadhaa tumemuonya lakini sijui ni kwa nini haya magenge yake kwasabu unaweza ukamwambia akakuelewa halafu ukakuta tena hayupo”

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amehudhuria katika mazishi ya Eliza na kuwahakikishia Wananchi kuwa Wahusika wote watakamatwa huku akiomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi.

“Binti amezaliwa mwaka 2005 halafu anafariki kwa kusababishiwa na Mtu haiwezekani, sisi tutafuata taratibu zote kuhakikisha jambo hili tunalishughulikia na wanamakambako muwe na imani jambo la msingi niwaombe tuwe na ushirikiano”
Screenshot_20230104_072227_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema anafahamu kuwa anasemwa kwa mengi ikiwemo kuambiwa anakopa fedha nje ambapo amesisitiza kuwa ni kweli anakopa lakini anakopa kwa maendeleo na hawezi kutegemea pesa za makusanyo ya TRA pekee kuendesha Nchi.

Rais Dr. Samia ameyasema hayo mbele ya Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “ Dhamira yangu ni kuendesha Taifa lenye amani na utulivu, Taifa lenye maendeleo makubwa, nasemwa kwa mengi ‘Anakopa tu’ ndio nakopa kwa maendeleo makubwa na mnayaona na kila inayoingia nasema imeingia kwenye SGR tumekopa FDB, imeingia kwenye Daraja tumekopa World Bank”

“Nikitegemea pesa ya Kidata (Kamishna Mkuu TRA) hapa ndani, hatuendi Ndugu zangu na mie nataka nimalize mitano yangu hii mpaka mwaka 2025 nikiwa nimeifanyia kitu Tanzania, nimeiletea maendeleo ya maana Tanzania sitaweza kufanya hivyo kama hakuna utulivu ndani ya Nchi Tanzania ni yetu wala sio yangu”

“Kuhusu marekebisho ya sheria mbalimbali nimecheki na Waziri wa Katiba na Sheria amenimbia sheria kadhaa zipo njiani kurekebishwa na juzi nilikuwa na kikao na Tume ya Uchaguzi na wenyewe pia wapo njiani kurekebisha sheria ya Tume ya Uchaguzi, nawatakia mikutano mema, kwa wale wenye fedha zenu IGP yupo angeanza kupokea maombi ya mikutano lakini kwa hivyo tulivyozungumza (Mikutano ifanywe kistaarabu)”
Screenshot_20230104_072355_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Dkt. Samia leo amezungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya Katiba na hivi karibuni itaundwa Kamati itakayotoa ushauri wa namna bora ya kuukwamua mchakato huo.

“Suala la Katiba limezungumzwa na kila Mtu kwa style mbalimbali kwa majina mbalimbali, kwa bahati nzuri mwaka jana nilikaa na Chama changu tukakubaliana nasi kuungana na Vyama vingine kutoa tamko la kukubali mchakato wa marekebisho ya Katiba”

“Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya Katiba kwa jinsi tutakavyokuja kukubaliana hapo mbele lakini tupo tayari kuukwamua, wengine wanasema tuanze na Katiba ya Warioba wengine tuanze na Katiba pendekezwa lakini ile ilikuwa mwaka 2014 ni miaka minane sasa kuna mambo kadhaa yameshabadilika”

“Kwahiyo kuna haja ya kuiangalia hali halisi ya sasa hivi, yale yaliyomo mule yanatufaa au hayatufai kwahiyo inawezekana zile mbili zote zikawa sio vyanzo vizuri vya kuanzia tukaanza tuliyonayo yapi mazuri yapi yarekebishwe lakini tukakopakopa kutoka kule na mengine ambayo hizo Kamati zitakazoundwa zitakuja nayo”

“Nataka niwape faraja kwamba hivi karibuni itaundwa Kamati ya kutushauri tuendeje ambayo itakuwa na Watanzana wa Sekta na Vyama vyote, Katiba hii sio ya Vyama vya Upinzani pekee, itakuwa Kamati ya Watanzania wote ili waje na kitu ambacho kitakuwa cha Watanzania, Katiba ya Watanzania”
Screenshot_20230104_072524_OGInsta%2B.jpg
 
Club ya Simba SC leo imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu mpya Raia wa Brazil Roberto Oliviera Do Carmo (62) kama Kocha wao mpya ambaye ataongeza nguvu katika kikosi chao.

Roberto Oliviera ni kocha ambaye alijizolea umaarufu Afrika Mashariki kutokana na kuisuka vizuri Vipers SC ya Uganda ambao ndio waliwatoa TP Mazembe kwenye Club Bingwa Afrika msimu huu.
Screenshot_20230104_072713_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Dkt.Samia wakati akizungumza na Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es salaam leo ametangaza kuruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa lakini amewasihi Wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu na sio kutukanana majukwaani na kusema yeye anaweza kuvumilia lakini chawa wake wanaweza wasistahimili.

“Tunatoa rukhsa twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, za kupevuka na siasa za kujenga na sio kubomoa, sisi ndani ya CCM tunaamini kukosoa na kukosolewa na kwasababu ndio walioweka Serikali wakosoeni”

“Mimi naamini mkinikosoa mnanimbia changamoto iko hapa, na nikiifanyia kazi ile changamoto Watu wakipata imani na Mimi naendelea kubaki na ndio maana siwaiti nyinyi Vyama vya Upinzania nawaita Vyama vya kunionesha changamoto zilizopo, sio Vyama vya upinzani, mnampinga nani? ndani ya Tanzania tunapingana kweli?, tunaoneshana kasoro”

“Twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, tusiende kutukanana, sio mila zetu, kusimamajukwaani ‘Wewe Samia Suluhu wewe hauna adabu wewe, miguu yako imekwenda upande wewe kichwa kama mbuzi’, Samia Suluhu anaweza akawa na upeo mzuri wa ustahimilivu kama alionao kwasababu yananipata ila nanyamaza lakini Mshabiki wa Samia, chawa wake anaweza asistahimili akaja akavaana na chawa wako wewe uliyetukana balaaa likaanza hapo kwahiyo tusiende kuchokozana”

“Najua mtaenda kusema Serikali hii ina madeni, ni kweli lakini mseme madeni yamefanya nini, kwamba reli inajengwa n.k, mwingine akivutiwa unavyorekebisha Serikali watasema Mimi chawa wa hawa watakuganda wewe sasa”
Screenshot_20230104_073436_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom