Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20221018-043310_OGInsta%2B.jpg
 
DERBY KUAMUA HATMA YA NABI YANGA.
.
Tayari kumekuwa na taarifa za chini chini kocha huyo Mtunisia hana muda mrefu kabla ya kutupiwa virago kwani mabosi wake hawataki kuona timu yao inapata matokeo mabaya zaidi.
Screenshot_20221018-043426_OGInsta%2B.jpg
 
Umeiona hii picha? Huu ni utamaduni wa Real Madrid kuwa Rais wa klabu atasafiri na Malegend kadhaa kuhudhuria tuzo ambazo Kijana kutoka Madrid atabeba tuzo, kwao wachezaji wao wa zamani ni taswira ya klabu, uhusiano wao hautamatiki baada ya kustaafu bali hudumu daima.

Zinadine Zidane, Ronaldo de Lima na Luis Figo wakiwa na Rais Perez ambaye ndie aliyewasajili kwenye zama za Galacticos hawa wote wana Ballon dor na jana walishuhudia Karim akibeba tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.
Screenshot_20221018-103713_OGInsta%2B.jpg
 
Karim Benzema anakuwa Mfaransa wa tano kubeba tuzo hiyo baada ya Raymond Kopa, Jean Pierre Papin, Zinadine Zidane na Michel Platin.

Baada ya nyota Stanley Mathews kushinda Ballon dor akiwa na miaka 41, Benzema anakuwa Mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo akiwa na umri mkubwa ndani ya miaka 66.
Screenshot_20221018-103849_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Super Sadio Mane alipoitwa jukwaani kuchukua tuzo ya Socrates iliyotokana na mchango wake kwa jamii ya Senegal alipewa mic aelezee kuhusu tuzo hiyo na vitu anavofanya huko kwao.

Bahati mbaya sana MC hakuelewa utamaduni wa sisi waafrika lakini pia hakuelewa imaan ya Mane inataka nini, Mane ni Muislam na hapaswi kujisifia vile anavyofanya kwao ile ni kama sadaka hupaswi kusema.

Mane alipopewa nafasi ya kuongea ni kama alipata wakati mgumu sana kuongea, alishukuru kwanza kisha akasema “Ni kama hivyo ulivyosema tu” yani hakutaka kujazia sana maneno akamwambia MC ni kama hivyo ulivyosema.

Wakati Mane anapata hicho kigugumizi, Legend mwingine wa Afrika, Didier Drogba ambaye nae alikuwa MC aligundua mapema sana na aliona kama Mane hawezi kujielezea sana akamuwahi na kusema “Thank you Sadio” kisha Mwamba akashuka na kuondoka zake.

MANE atafundisha mengi sana, anatufundisha mstari kati ya mali na ubinadamu, umaarufu na uungwana kisha pesa na roho safi! Vyote vimekuja kwake ila Mane na imaan yake safi ya kiislam na roho yake ya kiungwana imesalia.

IMAAM wa msikiti wa Liverpool atakuwa amemmiss sana, kwakuwa alikuwa wa kwanza kuingia msikitini kusafisha miswala na kusafisha vyoo, muungwana na Mtu safi kutoka Bambali huko Senegal.
Screenshot_20221018-104021_OGInsta%2B.jpg
 
CR7 HAKUNA TIMU ZINAMTAKA
.
Cristiano Ronaldo anaripotiwa ataendelea kubaki Manchester United kwa sababu hakuna klabu nyingine inayotaka kumsajili. CR7 alitaka kuondoka dirisha lililopita na huenda akahitaji hilo litokee pia Januari. Hata wachezaji wenzake wataka aondoke, lakini shida hakuna timu inayohitaji huduma yake kwa sasa. View attachment 2382315
So sad
 
Farhan Jr

Ukizungumza na Washindi wote watakwambia its lonely at the top, watakwambia pale juu pana upweke mkubwa sana, watakwambia kufanikiwa ni mateso sana.

Niliwahi kusimama darasani wakati nafundisha watoto wangu wa Kinondoni Islamic nakumbuka lilikuwa Form6 lile darasa, nikawaambia Watoto wangu dunia tunayoishi inataka kuona KIASI tu, usifanikiwe sana na usifeli sana.

Muulize Diamond wa Bibie Sandra, muulize Ali kijana wa Saleh Kiba au muulize Cristiano Ronaldo ukipata wasaa hata Mama yangu Lady Jay Dee, watakwambia its lonely at the top, juu pale pana upweke sana.

Wakati mwingine namtazama sana MO Hussein yupo juu mno kwasasa na tayari wengi wamemchoka kwakuwa tuna tabia ya kukinai mafanikio ya Mtu, amini usiamini watu wanasubiri MO akosee tu waseme, MO anafahamu kuwa pale juu pana upweke mkubwa sana ila hawezi kusema hadharani.

Nakumbuka niliwaambia watoto wangu siku ile darasani kuwa mafanikio yanatisha sana, nikawapa visa vingi mfano cha Whitney Huston, Michael Jackson niliwauliza maisha yao yaliishaje? Hata Mama yangu Brenda Fassie yaliishaje? Au hata Albert Mangwea, its lonely at the top.

Washindi wanapitia mengi sana, hawawezi kusema kirahisi! Leo hii wengine hawataki tu ngoma za Diamond ila hawana sababu, hawapendi tu uwezo wa MO Hussein bila sababu, hawamkubali tu Ronaldo bila sababu! Waulizeni watawaambia, pale juu panatisha sana.

Washindi wakisema kitu mbele ya waliofeli basi wanaambiwa wanajisikia, wakikaa kimya wataambiwa wanajiona, wakipatia watapondwa na wakikosea watatukanwa, wanafahamu hilo.

FORM 6 wa Kinondoni Islamic 2019 nadhani kama wanasoma hapa wanakumbuka wosia huu, niliwaambia mafanikio yanatisha sana! Its lonely at the top, siku moja nikirudi tena kushika chaki nitawaambia vizuri Wanafunzi wangu.

View attachment 2388705
Hata kama mafanikio yanatisha lakini sio sawa na umasikini aisee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom