

Farhan Jr
Niliandika kuhusu BUSARA lakini sikueleweka, ni ngumu kueleweka kwakuwa watu wanasahau mapema sana kuhusu ‘hatari’ ya sheria hata Hakimu anaiogopa sana.
Mmewahi kufikiria japo kwa uchache wakati Simba anagomea kuvaa nembo ya Mdhamini, kama TFF wangetumia hiyo sheria ingekuwaje? Sheria inatisha sana, haifai hata kuifuata kwa 100%.
Nilitegemea BUSARA mbili zitumike kwa TFF kwanza, ndio ni jukumu Mama la TFF kuomba ITC lakini kama Mwanao Yanga alikuwa nje ya muda wewe kama Baba kwanini hukumwambia mapema? Msahihishe ni Mwanao wa kumzaa.
Yaani Mwanao anataka kuoa na unafahamu ana wake wanne tayari, anakuja kuomba ridhaa ya kwenda kuoa utakubali aende bila kumuelimisha kuwa haiwezekani? Mpe elimu
BUSARA ya pili kwa TFF huyo Yanga ni mtoto wako kuhusu hilo sakata kuna Kiongozi yoyote wa Yanga (Anayetambulika) alizungumzia kwenye media? Mna njia zenu za mawasiliano na shauri lipo kwenye kamati kwanini msingesubiri kutoa taarifa baada ya kamati?
Naomba kidogo leo niwape ukubwa wa neno busara, naomba sote tukasome andiko moja na anaetaka nimtumie link “How LaLiga economic controls go beyond Financial Fair Play” lina madini sana.
Hii ni baada tu ya Financial Fair Play kutambulishwa Ulaya, LA LIGA wakakaa na klabu zao zote kuona namna gani hii sheria haiwaumizi na kuhakikisha klabu zao zinafanya vyema, tumeelewana?.
Alisimama Jose Guerra ambaye ni Cooperate General Director wa LA LIGA alisema kuna vitu havipo kwenye FFP tutaviongeza lakini walilegeza baadhi ya vifungu na ndio maana Barcelona kasajili sana licha ya kuanguka kiuchumi, ni kifungu hicho.
Wenzetu klabu zao kwanza na wanazilinda kivyovyote vile, wanatumia sana busara kwenye sheria kwakuwa wanajua wazi wakisimama hapo hakuna aliye salama eneo hilo.
Ni ngumu kueleweka ila makaratasi yapo ila kwa ground hayatumiki sana, Chelsea, Leicester na Man City walipaswa kupigwa rungu la FFP, mnaelewa kilichotokea? PENDANENI BABA NA MTOTO WAKO!