Makapuku Forum

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema chanzo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuyumba ni pamoja na kuwepo kwa matumizi yasiyo na tija kwa wagonjwa ikiwemo kurudia kufanya vipimo mara kwa mara katika hospitali tofauti.

“Kwanini NHIF iko katika hatari? ni sisi wenyewe wananchi. Leo nimeenda Muhimbili hospitali, nimeenda kufanya kipimo cha X-ray na vipimo vingine nimeandikiwa na dawa, kesho naenda private [hospitali binafsi] nafanya kipimo, naandikiwa dawa, ugonjwa huo huo. Sasa hapo kwanini NHIF isife kama tunaenda kwa mtindo huu?” amesema Waziri Ummy.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametangaza kuondoa katazo lililokuwa likizuia Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya Nchi kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao cha pamoja baina ya LATRA, Wamiliki wa stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa waliotengeneza vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa vibali na LATRA baada ya kukidhi vigezo.

Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa vyoo, sehemu ya mapumziko kwa abiria, viburudisho na sehemu ya maegesho.

Kutokana na hilo RC Makalla ameridhia vituo binafsi vitamo vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa Wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa Mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.
 
muandishi wakujitegemea
 
Daah

Nilipata kusikia mwaka fulani kuwa huko canada waalimu waliwahi kuandamana wapunguziwe mishahara maana wanalipwa mishahara mikubwa mno

Nikasema acheni waafrika tudharauliwe tu hawa watu tusijifananishe nao hata kidogo
 
Auntie nahamia Austria 🤣🤣🤣🤣
 
Upuuzi ntupu 63% ya bajeti inaenda kwenye matumizi tu 37% ndio inafanya mambo ya maendeleo. Wananunua 'mavieite' halafu anakuja na propaganda za kipuuzi tu. Wanatujua watz tulivyo mabozozo maana na hili litapita tu.
 
Si tuliambiwa inafilisika sababu wamekopesha na kujikopesha mikopo isiyo na tija!! Leo anakuja kuisafisha!! Aisee hili linchi🙌🙌🙌🙌
 
Tengeneza tatizo, then litatue🤣🤣
 
Safi sana Dr wa uchumi nakuelewa vyema sana. Ongeza tozo zingine Mwanawane tuchangie maendeleo vizuri
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…