Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wengi waliamini Steven Gerrard na Frank Lampard watakuwa na nyakati bora sana kwenye Ukocha ndani ya EPL, lakini hali imekuwa tofauti sana ni Patrick Viera ambaye anaonesha utofauti mkubwa sana.

Ameibadili Crystal Palace yenye wachezaji wengi wa kawaida na kuwa timu tishio kwa vigogo.
Screenshot_20220830-050433_OGInsta%2B.jpg
 
2017 Kijana Romeo Lavia alikutana na Jadon Sancho nae akamkabidhi jezi yake ya Borrusia Dortmund.

2022 Romeo Lavia yupo Southampton anakipiga EPL na alikabana na Jadon Sancho wa Manchester United.

Kuna vitu wanavyofanana kihistoria, wote wamepita Manchester City academy kabla ya kuondoka kwenda kujaribu maisha sehemu nyingine.

Never stop believing.
Screenshot_20220830-050600_OGInsta%2B.jpg
 
“Jezi ya Real Madrid ni nyeupe ila inaweza kuchafuliwa kwa jasho, tope na damu lakini kamwe haipaswi kuchafuliwa kwa aibu”

- Santiago Bernabeu, mchezaji na Rais wa zamani wa Real Madrid.
Screenshot_20220830-050718_OGInsta%2B.jpg
 
𝐗𝐀𝐕𝐈 𝐒𝐈𝐌𝐎𝐍 ndani ya ligi kuu soka Uholanzi.

Mechi -3
Mabao -4
Assists - 2

Kijana amejipata sasa, anauwasha
Screenshot_20220830-051710_OGInsta%2B.jpg
 
Golikipa Yann Sommer ameweka rekodi mpya kwenye Bundesliga ya kuokoa michomo zaidi ya 19 kwenye mechi moja dhidi ya Bayern Munich.
Screenshot_20220830-052130_OGInsta%2B.jpg
 
Kulia yupo Arjen Robben na kushoto yupo Frank Ribery, mabeki waliteseka sana na hawa Mafundi wawili.

Once upon a time in Munich
Screenshot_20220830-052231_OGInsta%2B.jpg
 
Oleksander Zinchenko ilibidi aingie uwanjani kumshinikiza Refa amalize mechi dhidi ya Fulham

Tayari ameiva na sasa ana damu ya Arsenal.
Screenshot_20220830-052451_OGInsta%2B.jpg
 
Huko Hispania vita ya kiatu imeanza mapema sana

Lewandowski - Mabao
Benzema - Mabao

Moto unawaka mapema tu
Screenshot_20220830-052827_OGInsta%2B.jpg
 
Paul Pogba ameripoti Polisi juu ya kutaka kutapeliwa na Rafiki zake wa karibu na Kaka yake wa damu, Mathias Pogba ambapo uchunguzi wa suala hilo unaendelea hivi sasa.

Stori yao ni ndefu sana ila inasemekana Mathias na Rafiki wa utotoni wa Paul wanamlalamikia kuwa hawasaidii kwa chochote kitu ambacho Pogba anakipinga na amesema wazi kuwa mara zote amewasaidia.

Inasemekana kuwa wakati wapo jijini Paris walimchukua Pogba na kwenda nae sehemu wakimlazimisha awape kiasi cha Pauni million 13 mbele ya watu wawili wenye silaha, kwakuwa wamekuwa wakimlinda mara zote bila yeye kujua, kitu ambacho kilimshangaza Pogba.

Mathias ambaye ni Kaka yake aliwahi pia kurekodi video na kusema atawaambia dunia juu ya Pogba ambaye watu wanamwona kama Staa, huku wakisema aliwatuma waende kwa Mganga ili amroge Kylian Mbappe.

Mengi yamejiri kuhusu sakata hilo na inasemekana haya yanakuja baada ya Pogba kumtimua nyumbani kwake mmoja kati ya Rafiki zake ambaye aliiba kiasi cha Pauni 200,000 kwenye kadi zake za benki.

Tayari uchunguzi juu ya Matapeli hao umeanza na Pogba amekuwa akitoa ushirikiano mzuri kwa mamlaka.
Screenshot_20220830-052942_OGInsta%2B.jpg
 
Hili sakata la Pogba nakumbuka hata Emmanuel Adebayor yalimkuta kama haya na alilalamika sana, kuna kitu hakipo sawa kwenye mtazamo wetu juu ya Ndugu zetu ikitokea wamefanikiwa.

Nahisi kuna mentality kuwa lazima ule kama anayetafuta.
Screenshot_20220830-053035_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati tunashangaa sakata la Paul Pogba na Ndugu yake Mathias, tusisahau sakata la Emmanuel Adebayor pia na familia yake, Jamaa alisimulia mengi mpaka kutaka kujiuwa mara kibao.

Adebayor aliwahi kulaumiwa hakumsaidia Kaka yake mpaka amefariki lakini anasema alipopewa taarifa za kuuguwa kwa Kaka yake alisafiri mpaka Togo ili kumjulia hali Kaka yake.

Kwa mshangao mkubwa sana alipofika Mama yake alimwambia huwezi kumwona kwasasa ila atoe pesa na wao watahudumia, Adebayor aliwapa pesa nyingi sana japo baadae walipinga.

Kama hivyo haitoshi Adebayor alisimulia kisa cha Dada yake ambaye alimwambia anataka nyumba ya Pauni 1.2 Million nchini Ghana na Ade alimtumia hizo pesa ila ajabu aliporejea Afrika na kutaka kwenda kuiona nyumba akagundua ameipangisha na hakai yeye.

Mbaya zaidi alimnunulia hiyo nyumba ili Dada yao huyo aishi na mdogo wao ila ajabu alimtumja hadi mdogo wake ili apangishe, Adebayor alipohoji alitukanwa sana kwenye simu na Dada yake.

Kwa kumalizia Adebayor aliwahi kuwekewa kikao na Ndugu zake wakitaka amjengee kila mmoja nyumba na awalipe mshahara kila mwisho wa mwezi kwakuwa yeye ana pesa.

Baadhi tu ya mambo ambayo Adebayor alipitia na naona stori nyingine kwa Paul Pogba.
Screenshot_20220830-053126_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom