[emoji599] BUMBULI BYE BYE YANGA
.
Rasmi Uongozi wa klabu ya Yanga, kupitia kwa Kaimu Mtendaji Mkuu, Simon Patrick umethibitisha kuachana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli, hivyo kwa sasa nafasi iko Wazi na Wenye Sifa wanaruhusiwa kutuma Maombi.
WAFAHAMU NYASA BIG BULLETS
.
Wapinzani wa Simba SC katika hatua ya awali ya CAFCL, Timu ya Nyasa Big Bullets makao yake Makuu yapo katika jiji la Blantyre, Malawi [emoji1156] inautuia Uwanja wa taifa wa Kamuzu unaoingiza jumla ya mashabiki 40,000.
.
Ilianzishwa mwaka 1967 wakati huo ikijulikana kama Bata Bullets baadaye ikaitwa Total Big Bullets na cabla ya jina la sasa iliwahi kujulikana kama Bakili Bullets.
.
Ndio klabu kubwa zaidi ya soka ambayo inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki, idadi ya mataji pamoja na hali nzuri ya kiuchumi. Katika mechi za nyumbani imekuwa ikitumia jezi za rangi nyekundu na ikiwa ugenini huvaa rangi nyeupe.
.
Idadi kubwa ya wachezaji wa timu ya taifa ya Malawi ambao huitwa kutokea kwenye Ligi ya ndani ni wale wanaotokea katika kikosi cha Nyasa Big Bullets. Mfano wa nyota wanaounda kikosi hicho ni Sankhani Mkandawire, Yamikani Fodya, Chiukepo Msowoya, Righteous Banda na Erick Kaonga.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.