[emoji3578][emoji3578] George Ambangile
ITS GOOD FOOTBALL
[emoji1593]Simba SC na St George wameitendea haki hii siku ya leo , kwa kuonesha kandanda safi kwa dakika zote 90+ . Inawezekana ikawa mechi ya preseason ya mwisho kwa Simba SC kabla ya mitanange ya kimashindano kuanza
[emoji1593]Kocha Maki alibadili mifumo kama mara tatu , alianza na 4-4-2 dakika kadhaa zikapita akabadilisha kwenda 4-2-3-1 ( Okrah nyuma ya Habib , Sakho na Kibu katika wing zote mbili, Mkude na Kanoute kwenye kiungo wa kati ) na mwisho baada ya kuingia Kapombe akabadilisha kwenda 3-4-2-1 ( Back 3 ya Kapombe Outtara na Inonga ) huku Akpan na Okwa katikati , Wingbacks Banda na Mzamiru na Chama Jr & Phiri nyuma ya Dejan . ( Tactically Flexible )
[emoji1593]St George wenyewe wamecheza takribani dakika zote kwa kutumia 4-2-3-1 ambayo kuna wakati kwa kiasi fulani ilikuwa inabadilika kuwa 4-3-3 hasa wakiwa na mpira
[emoji1593]Simba SC kuna wachezaji wengi wenye kasi, kitu kimoja nilichoona ambacho naamini hata kocha kaona ni wakipoteza mpira wanachelewa kufika kwenye tukio na pia wakiwa mpira kwenye kiungo wanaharakisha pasi na mipira kupotea . Nafikiri kama kutakuwa na ufanisi mzuri sana wa pasi katika wakati sahihi ile kasi ya ushambuliaji itafaidika ( Chama Jr anarahisisha soka [emoji91])
[emoji1593] St George wana wachezaji wengi sana ambao kiufundi wapo vizuri , wanacheza pasi fupi fupi kwa kutengeneza pembe tatu na wanahama kwa pamoja nafikiri kuna muda wanazidisha bila sababu ( over play )
NOTE
1: Nafikiri Okrah anacheza vizuri kwenye namba 10 na bado una Chama Jr ... hiyo ni kazi ya kocha Maki , ni faida kuwa na wachezaji wazuri kila eneo
2: Outtara , nafikiri baada ya kuondoka kwa Wawa Simba walihitaji Ball Playing CB . [emoji91]
3: Inonga anatakiwa kucheza " simple football " kuna muda anajitengenezea matatizo . Beno good game [emoji91]
4: Yule Abel [emoji91] miguu yake hatari
5: Kiungo cha St George , Nahodha wao na Panom Gattouch wanaubonda vizuri
6: Chama Jr hana adabu [emoji91]
7: Kwani dirisha la usajili limefungwa ? Kuna wachezaji pale St George