Makapuku Forum

GEITA Gold itawakosa nyota wake wanne akiwamo beki Kelvin Yondani wakati itakapoikabili Azam katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa leo mjini hapa.
Nyota hao watakosekana kwa sababu mbalimbali, huku wenyeji wakiwa na kiu ya kuendeleza wimbi la ushindi kwani mchezo uliopita ilishinda 2-0 dhidi ya KMC.

Katibu wa Geita, Simon Shija alisema maandalizi yanaendelea, ila itaikosa huduma ya Kelvin Yondani anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Mussa Gadi (mgonjwa), Aaron Katambo na Yusuph Kagoma wenye matatizo ya kifamilia.
 
Kesho litakufa jitu
 
KISA MOTO, SAFA YAISHTAKI SIMBA CAF
.
Shirikisho la mpira wa miguu la Afrika Kusini (SAFA)
limeishitaki klabu ya Simba
kwa kamati ya nidhamu ya CAF kutokana na kufanya vitendo ambayo ni kinyume cha sheria za CAF Katika mchezo dhidi Orlando Pirates mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo walichoma uvumba katikati ya dimba na kupelekea kuharibiwa eneo la kuchezea.
.
 
INONGA BEKI BORA MSIMU HUU
.
Mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Daruweshi Saliboko amemtaja beki wa Simba, Henock Inonga Baka kuwa ndio Beki Bora msimu huu;
.
“Kwa mtazamo wangu ukiniambia nitaje beki bora msimu huu basi nitasema ni Inonga, kwani nimemshuhudia uwanjani tulipocheza na Simba na pia namuangalia akicheza dhidi ya timu nyingine,” amesema Saliboko na kuongeza:
.
“Beki anayejiamini na anaongoza wengine, tofauti na baadhi ya tabia za wachezaji ambao wanakuwa waoga kukumbushana majukumu mmoja anapojisahau.”
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…