Makapuku Forum

Makapuku Forum




I take a little smoke in the evenin'
I take a little whiskey on ice
I never get behind on killin' my mind
It's just the kind of thing I like
Just the kind of things I like

The minute that I saw you walkin' over
I figured I was diggin' my grave
And you had the shovel, I knew you were trouble
But you're just the kind of trouble I crave
Just the kind of trouble I crave
And mama always set a good example
Daddy always gave me good advice
Jesus tried to steer me in the right direction

But the devil always made me think twice
Devil always made me think
Someday I'm goin' six feet under
And when they got me standin' at the gate
They'll tally up my sins, and won't let me in
Say "Son, you're just a little too late"
"Son, you're just a little too late"

Just sikiza guitar, katika waimbaji wa country wa kipindi hiki Stapleton anafanya vizuri sana
Usiku mwema
 
Rais Samia ametuma salamu za pole kwa wafiwa kutokana na vifo vya Watu 9 waliofariki kwa ajali ya gari Mkoani Njombe.

Akitoa salamu hizo kwa niaba ya Rais katika Ibada ya kuaga miili hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Jimbo Katoliki Njombe, RC wa Njombe, Waziri Kindamba, amewasihi Waombolezaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

“Nichukue nafasi hii kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye naye ameguswa sana na msiba huu”

Watu hao waliofariki ni miongoni mwa Vijana kutoka Umoja wa Vijana Kanisa Katoliki Njombe (UVIKANJO) na walifariki kwa ajali ya gari April 24,2022 katika eneo la Igima Kibaoni walipokuwa wakitoka kutembelea kituo cha kulea Watoto yatima kilichopo Ibumila Wilayani Njombe.
Screenshot_20220427-033354_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamke mmoja kutokea Jimbo la Tennessee nchini Marekani, Sheila Downey (68) amekamatwa baada ya kudaiwa kumchoma Mumewe kwa kisu hadi kupelekea kifo chake baada ya ugomvi uliotokana na mabishano baada ya Mume kulalamika kutopenda ladha ya kahawa aliyoiandaa Mkewe.

Polisi walipofika eneo la tukio, walimkuta Mzee wa miaka 81 akiwa amechomwa kisu mara kadhaa na Mkewe ndani ya nyumba yao na alipelekewa Hospitali akiwa katika hali mbaya ingawa alipata nafasi ya kuzungumza na Polisi hao na kutoa maelezo yake kuhusu tukio ambalo lilimsababishia majeraha kwamba Mkewe ndiye amemchoma kisu.

"Baada ya ugomvi Mke alienda kwenye chumba cha kufulia nguo na kujaribu kunywa bleach lakini Mumewe alifanikiwa kumzuia baada ya hapo, Mwanamke huyo alichukua kisu na kumchoma Mume mara kadhaa bila kuacha" Polisi

Sheilah Downey hakuwa nyumbani wakati Polisi walipofika lakini aliwekwa chini ya ulinzi aliporejea ambapo aliwekwa kizuizini katika jiji la Memphis, Tennesse ambapo ameshtakiwa kwa mauaji ya daraja la kwanza, anashikiliwa bila dhamana na kesi yake inasikilizwa tena leo Aprili 26, 2022.
Screenshot_20220427-033514_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya Moscow, nchini Urusi imeamuru kukamatwa kwa mali na fedha za kampuni ya Google, zenye thamani ya USD Milioni 7, hii inatokana na kesi inayohusu vikwazo ambavyo kampuni ya teknolojia ya Marekani imeweka kwenye chaneli ya YouTube ya kampuni moja maarufu ya televisheni nchini humo.

Kampuni ya Alphabet Inc.'s ama Google haikujibu mara moja ombi la maoni, Mashirika ya habari ya Urusi yaliripoti kuwa kesi hiyo inahusu Televisheni ya GPM Entertainment ya Gazprom Media Holding, ambayo iliwasilisha kesi, ikiitaka Google kurejesha ufikiaji wa akaunti yake ya YouTube.

YouTube, ambayo imezuia vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na Serikali ya Urusi duniani kote, iko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa wadhibiti wa mawasiliano wa Urusi na wanasiasa.

Urusi imezuia makampuni mengine ya kigeni ya mtandao, ikiwa ni pamoja na Meta Platforms Inc.'s (FB.O) Facebook na Instagram, huku ikipambana kudhibiti mtiririko wa taarifa baada ya kutuma makumi ya maelfu ya wanajeshi nchini Ukraine Februari 24, 2022. YouTube bado inapatikana kwa sasa.
Screenshot_20220427-033619_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka Wabunge na Madiwani kukataa kupitisha miswada ya Sheria yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya Wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.

Kinana amesema Sasa ni wakati muafaka kulitazama vyema kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.

Kinana ameyasema hayo mjini Korogwe ambapo amesema "Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni, mkiletewa sheria pelekeni kwa Wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya Watu muwasidie wakue"

"Wabunge sheria ikija Bungeni waambieni (Serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane na Wananchi"
Screenshot_20220427-033738_OGInsta%2B.jpg
 
Katibu Mwenezi CCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akiwa kwenye Mkutano wa Viongozi Kilimanjaro leo April 26,2022 amewataka Wana CCM kuitekeleza Ilani ya Chama hicho ili kuwaletea Wananchi maendeleo ambapo amesema hiyo ndio namna bora ya kulinda Dola na sio kutumia marungu na mapanga.

"Ni lazima sisi wana CCM tuitekeleze vizuri Ilani yetu ya uchaguzi kuwaletea maendeleo Wananchi ili kulinda dola tuliyonayo, huwezi kulinda dola kwa marungu na mapanga"
Screenshot_20220427-034105_OGInsta%2B.jpg
 
Kufuatia mvua ilionyesha April 23,2022 Mjini Geita iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha kuezua paa za Kaya 42, Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amefika eneo la Katumaini Mzingamo mtaa wa Nyamalembo kata ya Mtakuja kusikiliza na kutoa pole kwa Wananchi waliobomolewa nyumba zao.

RC Senyamule ametoa Tsh. Elfu 50 kwa kila Kaya kwa Familia 9 zilizoathirika zaidi na mvua hiyo ikiwa ni sehemu ya kujikimu kwa chakula kwa kipindi hiki.

“Leo tumekuja kutoa pole kwa familia zilizoathirika na mvua zinazoendelea hapa mjini kwetu na pole hizi zimetoka kwa Mh. Rais wetu Samia Suluhu Hasaan na ameniagiza nisije mikono mitupu wakati mnapitia changamoto ya kurudisha makazi yenu basi msiwaze kuhusu chakula” RC Geita
Screenshot_20220427-034327_OGInsta%2B.jpg
 
Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong-un jana usiku ametoa hotuba ya kibabe katika gwaride la kijeshi na kuapa kuongeza silaha za nyuklia nchini humo, gwarid hilo limefanyika katika kuadhimisha mwaka wa kuanzishwa kwa Majeshi ya Korea Kaskazini ambapo makombora kadhaa yaliyopigwa marufuku ya masafa ya mbali (ICBMs) yameoneshwa kwenye gwaride hilo.

Itakumbukwa March mwaka huu, Korea Kaskazini ilijaribu makombora hayo ya masafa marefu kwa mara ya kwanza tangu 2017 na kufanya wapate shutuma nyingi kutoka kwa Jumuiya za Kimataifa ikiwemo nchi ya Marekani.

Marekani pia iliiwekea Korea Kaskazini vikwazo kadhaa baada ya jaribio hilo la ICBM, iliyoundwa kwa ajili ya usambazaji wa silaha za nyuklia lakini hata hivyo, Kim hajakatishwa tamaa na shutuma hizo kufikia sasa.

Kim amesema wataendelea kuchukua hatua za kuimarisha na kuendeleza uwezo wa nyuklia wa Taifa hilo kwa kasi ya juu... kwenye swipe nimekuwekea picha za kwanza kabisa kutoka kwenye gwaride hilo ambapo Kim alihudhuria akiwa na Mkewe anayeitwa Ri Sol Ju.
Screenshot_20220427-034429_OGInsta%2B.jpg
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewatangazia Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El Fitr itakuwa siku ya Jumatatu May 02,2022 au Jumanne May 03,2022 kutegemea kuandama kwa Mwezi.

Sherehe za Eid kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es salaam, Swala ya Eid itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi.

Baraza la Eid litafanyika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 8 mchana.
Screenshot_20220427-034524_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema leo kuwa Marekani inaamini Ukraine inaweza kushinda vita dhidi ya Urusi iwapo itapatiwa silaha madhubuti.

Austin ameyasema hayo nchini Poland muda mfupi kabla ya kupanda ndege kuelekea mjini Ramstein nchini Ujerumani kwa mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya kujihami (NATO) unaofanyika leo Jumanne.

Licha ya onyo kutoka Urusi Austin amesema Marekani imetenga kiasi dola milioni 165 kwa ajili ya silaha na dola nyingine milioni 300 kwa msaada zaidi wa kijeshi nchini Ukraine.
Screenshot_20220427-034646_OGInsta%2B.jpg
 
Bodi ya Twitter imekubali kumuuzia Kampumi hiyo Tajiri zaidi duniani, Bilionea Elon Musk kwa USD Bilionea 44 baada ya awali Kampuni hiyo kupinga dau lake, Elon Musk amepania kufanya mabadiliko kadhaa kwenye mtandao huo ikiwemo kulegeza masharti ya maudhui.

Musk ni Mtu tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes huku akikadiriwa kuwa na utajiri wa tamani ya USD Bilioni 273.6, fedha nyingi amezipata kutokana na hisa zake katika Kampuni ya kutengeneza magari ya umeme Tesla ambayo anaiendesha.

Musk pia anaongoza kampuni ya safari za anga za mbali SpaceX.
Screenshot_20220427-034744_OGInsta%2B.jpg
 
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Kagera Tadei Mayunga amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo alasiri eneo la Shelui, Igunga.

Meneja Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka jeshi la Polisi.

Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Aprili 26, 2022 majira ya saa tisa alasiri ambapo dereva wa gari hilo anadaiwa kuwa na hali mbaya.
Screenshot_20220427-034855_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo katika kupindi cha mwaka mmoja tu alichokaa madarakani.

Amesema kwa sasa Rais yuko katika nchini Marekani ambapo amesema ziara hiyo imemkutanisha na viongozi wakubwa akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ambaye nchi yake Ina ushawishi mkubwa duniani.

Kinana ameyasema mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa wana CCM wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.
Screenshot_20220427-035010_OGInsta%2B.jpg
 
Miili tisa ya waumini wa kanisa katoliki mkoani Njombe waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Igima wilayani Wanging'ombe Aprili 24, 2022 imeagwa katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Njombe.

Akizungumza wakati wa ibada ya kuaga miili hiyo, Mkuu wa Mawasiliano wa Jimbo hilo, Padri Eusebius Kyando amesema Umoja wa Vijana Katoliki Jimbo la Njombe pamoja na walezi wao walipata ajali wakiwa wanarudi katika safari yao ya kitume walikokwenda kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Dorothea Upendo kilichopo Ibumila Parokia ya Mtwango.

Amesema watu watatu walifariki papo hapo na wengine sita walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitlini.
Screenshot_20220427-035112_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom