'Solar Orbiter' ni kifaa kilichorushwa kwenye anga za juu (space) kwaajili ya kurekodi tabia na mwenendo wa Jua. Kilirushwa rasmi februari 10, 2020 na inatazamiwa kumaliza kabisa kazi zake mpaka Desemba, 2026.
Chombo hicho kinatarajiwa kufanya mizunguko 22 kuzunguka Jua na mpaka sasa kimeshamaliza mizunguko 04.
Picha unayoiona hapo ilipigwa na chombo hicho Machi 07, 2022 kutokea umbali wa kilometers milioni 75, kutokea hapo iliweza kuchukua picha ya muundo mzima wa Jua kwa ubora unaofikia pixels milioni 83.
Changamoto mojawapo kubwa ya sayari ya Mars ni kani yake ya mvutano (gravity) ni ndogo hivyo inashindwa kushikilia vizuri paa la hewa (atmosphere).
Atmosphere' ya Mars ni nyembamba sana, chukua mfano ukirusha jiwe kwenda juu kwenye sayari yetu ya Dunia kasi ambayo jiwe litakua linashuka kuja chini huwa ni taratibu mpaka likifika kwa karibu ndio hushuka kwa kasi.
Sasa kwa namna atmosphere' ya Mars ilivyo, kama utarusha jiwe kwenda juu, kasi inayotoka nayo juu ndio inayofika nayo chini hivyo hivyo tena huongezeka zaidi kadri inavyoshuka chini.
Hivyo basi, ili binadamu aweze kuishi huko itabidi sayari ya Mars kwa mfululizo atmosphere' yake iwe inaongezewa ujazo huku kwenye ardhi yake ikifanyika namna ya kuongeza Mass ili kuleta balance nzuri ya gravity.
Jambo kama hilo kutokea wanasayansi wanasema labda kwa karne zijazo lakini sio karibuni.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.