Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,081
- 464,013
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha shughuli za ujenzi katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Makoani Tanga zinakamilika haraka.
Amesema kuwa Wizara hiyo inapaswa kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Ngorongoro waliojiandikisha kuhama kwa hiari "Zoezi hili linaloendea la kuimarisha miondombinu ikiwemo upimaji wa viwanja litawanufaisha wakazi wa Msomera pamoja na hao wanaohamia eneo hili"
Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Jumapili, Aprili 24, 2022 alipokagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Mkoani Tanga kwa ajili ya wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhamia kwenye Kijiji hicho ili kupisha shughuli za uhifadhi kwa maendeleo ya Taifa.
Aidha, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuendelea kuandaa mazingira mazuri ya ufugaji "Wizara hii inapaswa pia kuhakikisha kwamba kunakuwa na miundombinu wezeshi ya wafugaji yakiwemo malambo ya kunyweshea mifugo, majosho, ujenzi wa kliniki ya kutibu magonjwa ya mifugo katika eneo hilo.”
Akitoa maelekezo kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Majaliwa ameitaka iendelee kuwekeza nguvu katika kuimarisha miundombinu ya elimu "Kama tunavyoona hapa shule ya msingi inajengwa, sekondari inajengwa, zahanati zinakarabatiwa lakini pia ujenzi wa kituo cha afya na barabara unaendelea, ongezeni nguvu"
Majaliwa pia ameitaka Wizara ya Maji iendelee kuhakikisha kiwango cha maji katika eneo hilo kinakuwa toshelevu kwa kuchimba zaidi ili hata majosho na malambo yapate maji ya kutosha. Maji ambayo tayari yameshachimbwa na kuyapata ni mengi kuliko mahitaji lakini tuongeze kiwango"

mtoto mlito mlito