Makapuku Forum

Makapuku Forum


Surely????
Sasa kwa huyu ndugu yangu Espy Atoto si atakuwa zaidi ya Gaidi
20220424_143437.jpg
 
Kwanza Simba sina shaka nayo, nilishawatabiria watacheza Fainali. Kwenye mchezo wa mpira wa miguu kocha kulalamika wakati mwingine ndio raha yake. Mpira wote tuliona, penati ilikuwa ya halali na Orlando walifungwa kwa uwezo.

Na wasitutishe huko kwao, Simba inasumbuliwa na timu ambazo wachezaji wake wana uwezo wa kiufundi mguuni. Orlando ni timu nzuri lakini wachezaji wake wengi hawana ufundi mguuni, wao power play wanaweza kucheza.

Nafikiri Onyango akirudi kwenye kikosi Simba inaweza kuhimili na kulekule unaweza kushangaa Simba inashinda. Si wanasema hapa walionewa, wakipigwa na huko kwao waseme tena wameonewa lakini nina uhakika Simba watawafunga

Nawatahadharisha Simba kwenye mipira ya kona, na mipira ya kutengwa ambayo mtu anapiga wengine wanavamia golini, wawe makini sana.

Simba sio wa kinyonge kiasi hicho, Tanzania tumeshaamka, Orlando wanaweza kufungwa kwao palepale.

- Mecky Mexime
Screenshot_20220424-161712_OGInsta%2B.jpg
 
Mechi zinazoendelea kwenye hatua Robo Fainali michuano ya Afrika na kwa kuwa tunapata kuitazama tuna mengi ya kujifunza hata namna tunavyoendesha mijadala yetu au kulaumu tunakuwa na kiwango na ubora wa michuano yenyewe.

Niwatakie kila la kheri wawakilishi wa Tanzania @simbasctanzania na kuwapongeza kwa hatua waliyofikia kwa sasa kwa namna wanavyopambana kwenye hatua ya makundi na kuhakikisha wanaingia Robo Fainali

Hatua ya Robo Fainali ni hatu inayotoa bingwa wa michuano kwa maana hiyo ni hatua yenye vilabu bora kwa michuano husika, so kunahitajika kikosi bora kupambana kupata matokeo ya jumla kwa mechi mbili kwenye hatua hii
ufundi, mbinu uwajibikaji ni wa kiwanga cha juu.

Kama wa Tanzania tunatamani kuona timu zetu zinatwaa ubingwa siku moja japo inawezekana timu kuchukua ubingwa kwa bahati lakini bado tuko mbali kusema tunautaka ubingwa ukilinganisha na vilabu ambavyo mara kwa mara vimekua vikiingia fainali.

Kuhusu mchezo wa wenyewe [Orlando Pirates vs Simba] kwenye karatasi inaonekana Simba wametoka na sio kwa bahati mbaya ni kutokana na matokeo ya Simba kwenye mechi za ugenini na kiwango kilichoonyeshwa na timu pinzani kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Hiyo haiwazuii kupata matokeo ya jumla ndani ya kiwanja na kusonga mbele japo sio kazi nyepesi, kinachohitajika ni mpango mzuri wa kuicheza mechi kutoka benchi la ufundi na utekelezaji kutoka kwa wachezaji kuhusu viongozi kutekeleza majukumu yao, sina shaka na eneo hili.

KILA LA KHERI SIMBA, KILA LA KHERI TANZANIA.

- Amri Kiemba
Screenshot_20220424-161955_OGInsta%2B.jpg
 
Didier Drogba amebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Shirikisho la soka nchini Ivory Coast baada ya kushika nafasi ya tatu.

WAGOMBEA NA IDADI YA KURA WALIZOPATA

1. Yacine Idriss Diallo 59
2. Sory Diabaté 50
3. Didier Drogba 21

Sasa rasmi kuwa Diabate Sory na Idriss Yacine wanaelekea kwenye raundi ya pili kumpata Rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo
Screenshot_20220424-162127_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom