Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220424-061223_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220424-061238_Opera%20Mini.jpg
 
April 28, 2022, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atasafiri hadi Ukraine kukutana na Rais Zelensky wa Ukraine, ambapo anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa Msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Guterres pia atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kujadili kuongezwa kwa usaidizi wa kibinadamu kwa Ukraine.

Umoja wa Mataifa umesema Guterres atakutana pia na Rais Vladimir Putin April 26,2022 ambaye atampokea nchini Urusi, ili kufanya mkutano wa kikazi na kupata chakula cha mchana na Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema Guterres alikuwa akiomba hadhira tofauti na Putin huko Urusi na Zelensky huko Ukraine kujadili hitaji la dharura la kuleta amani.
Screenshot_20220424-064936_OGInsta%2B.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amezungumzia zoezi linaloendelea la kuwapanga Madereva wa bajaji na bodaboda mkoa wa Dar es salaama na kusema Madereva hao hawawezi kuondolewa katikati ya Jiji .

Chongolo ameyasema hayo katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala ambapo amesema Madereva hao ni Watu muhimu na hawawezi kunyanyaswa kwasababu wanajitafutia riziki halali, ambapo amewasihi Watu waache kutoa taarifa za kupotosha umma kuwa wanaondoshwa mjini.

“Kinachofanyika sio kuwazuia bodaboda na bajaji wasiingie mjini bali ni kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi vitakavyoweza kutambulisha Watu wanaohitaji kutumia usafiri huu”

Chongolo amesema Madereva bajaji baadhi yao ni Watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri asilimia 10, hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum kwa ajili yao ili wasigombanie abiria na watu wengie wasiokuwa na ulemavu.
Screenshot_20220424-065351_OGInsta%2B.jpg
 
Afisa wa Taliban amesema mlipuko wa bomu kwenye Msikiti na Shule ya kidini kaskazini mwa Afghanistan jana Ijumaa uliua zaidi ya Watu 30, wakiwemo Wanafunzi.

Naibu Waziri wa Utamaduni na Habari wa Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema bomu hilo katika mji wa Imam Saheb mkoani Kunduz pia liliwajeruhi Watu 43, wengi wao wakiwa Wanafunzi.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini tawi la Dola la Kiislamu nchini Afghanistan lilidai kuhusika na mashambulizi ya mabomu yaliotokea siku moja kabla, likiwemo dhidi ya msikiti wa Kishia katika mkoa wa Mazar-e-Sharif, ambamo Waumini wasiopungua 12 wa Kishia waliuawa.
Screenshot_20220424-065456_OGInsta%2B.jpg
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Dkt. Philip Mpango amewaasa Wananchi wa Kijiji cha Kasumo na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutumia fursa za miradi inayopelekwa na Serikali katika mkoa huo kikamilifu ili kujiletea maendeleo.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi waKigoma katika Kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mara baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga.

Amesema Serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika mkoa huo ikiwemo madaraja, barabara na ile ya elimu na kuwaasa Wazazi kuhakikisha wanawapeleka Watoto wao kupata elimu inayotolewa bila malipo na Serikali.

Aidha amewapongeza Wananchi wa Buhigwe kwa kukubali kutoa eneo la hekari 149.9 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Tehama kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha songambele mkoani Kigoma, Mpango amesema Serikali Itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa mkoa huo katika masuala ya miundombinu pamoja na mawasiliano.
Screenshot_20220424-065555_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia amesema makala maalumu ya The Royal Tour iliyozinduliwa nchini Marekani itasaidia kukuza Sekta ya Utalii katika Soko la Kimataifa.

"Aprili 18 nimeshiriki katika uzinduzi wa makala maalumu iitwayo “Tanzania: The Royal Tour”, nchini Marekani. Makala hii inakusudia kutangaza na kukuza sekta yetu ya utalii katika Soko la Kimataifa, na kuongeza fursa zaidi za ajira zitokanazo na utalii na uwekezaji nchini"
Screenshot_20220424-065648_OGInsta%2B.jpg
 
Mpiga debe mmoja wa eneo la Makambako Mkoani Njombe amefariki dunia kwa kukanyagwa na tairi za gari katika kichwa chake kutokana na kuanguka wakati akifukuzia basi linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kupata posho yake ya kupakia abiria.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema "Mpiga debe alikuwa amefuata fedha yake kwa ajili ya abiria aliokuwa amewapakia na kwa bahati mbaya ule malango wakati unajifunga alisukumwa na akadondokea kwenye uvungu na tairi za nyuma za gari ambazo zilimpitia”

RPC Issah ametoa wito kwa Wafanyakazi wa maeneo ya stendi kuwa makini na kuangalia usalama wao wakati wa kufanya kazi zao.
Screenshot_20220424-065737_OGInsta%2B.jpg
 
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 95 wa Kijiji cha Lwanzali kilichopo Lupembe Halmashauri ya Wilaya ya Njombe amekutwa ameuawa ndani ya nyumba yake huku upelelezi wa awali ukionesha kuwa chanzo ni kutokana na Mzee huyo kutuhumiwa kufanya ushirikina katika Familia yake.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema "Tumejaribu kwenda katika eneo lile na imebainika huyu Mzee walikuwa walikuwa wanamtuhumu kuwa anafaya mambo kishirikina katika Familia yake”

Kamanda Issah amesema Polisi wanaendelea kuchunguza ili kubaini ni nani aliyehusika na mauaji hayo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Screenshot_20220424-065832_OGInsta%2B.jpg
 
Mtoto Salah Jackson (5) mwenye ulemavu wa viungo, mkazi wa kijiji cha Makiwaru, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kutokana na njaa na kisha mama yake mzazi kumzika kimya kimya usiku wa manane.
Mtoto huyo anadaiwa kuzikwa na mama yake mzazi aitwaye Rebecca Siowi (30) usiku wa kuamkia Aprili 22, 2022 nyumbani kwa bibi yake walikokuwa wakiishi yeye pamoja na mama yake baada ya mume kumtelekeza na watoto watano.

Tukio hilo liligundulika baada ya mtoto huyo kutoonekana jioni ya Aprili 21 nyumbani alikokuwa akiishi kwa bibi yake, ambapo bibi yake huyo alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake huyo bila mafanikio ndipo Aprili 22 alipobainika kuwa amezikwa.

Akizungumzia tukio hilo leo Aprili 23, 2022 Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amekiri kuwepo kwa tukio hilo, akisema baada ya kupata taarifa hiyo kutoka kwa wananchi walifika eneo la tukio kuona sehemu alipozikwa mtoto huyo.
Screenshot_20220424-065932_OGInsta%2B.jpg
 
Maandalizi ya Kongamano la Tume Huru ya Uchaguzi Kuelekea Katiba Mpya linalotarajiwa kufanyika Mei 7,2022 07 Mkoani Mwanza.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amekutana na viongozi wa Ngome za Vijana, Wazee na Wanawake mkoani humo.
Screenshot_20220424-070037_OGInsta%2B.jpg
 
Simba imezima uvumi uliowashtua mashabiki wake juu ya mastaa wake watano kukutwa na maambukizi ya Uviko-19.
Meneja wa Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally amesema bado hawajapokea majibu ya vipimo vya Uviko na kwamba taarifa hiyo haina ukweli.

Ally amefafanua zaidi akisema kikosi chao kilifanya vipimo hivyo jana jioni na kwamba utaratibu ni kuwa majibu yatatoka ndani ya masaa 24 kutoka muda ambao walipima
Screenshot_20220424-070130_OGInsta%2B.jpg
 
Afisa wa Taliban amesema mlipuko wa bomu kwenye Msikiti na Shule ya kidini kaskazini mwa Afghanistan jana Ijumaa uliua zaidi ya Watu 30, wakiwemo Wanafunzi.

Naibu Waziri wa Utamaduni na Habari wa Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema bomu hilo katika mji wa Imam Saheb mkoani Kunduz pia liliwajeruhi Watu 43, wengi wao wakiwa Wanafunzi.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini tawi la Dola la Kiislamu nchini Afghanistan lilidai kuhusika na mashambulizi ya mabomu yaliotokea siku moja kabla, likiwemo dhidi ya msikiti wa Kishia katika mkoa wa Mazar-e-Sharif, ambamo Waumini wasiopungua 12 wa Kishia waliuawa.
View attachment 2198336
Wakati mwingne ukitafakari unaona watu wanaridhishwa ujinga kwenye nyumba zao za ibada
 
Mpiga debe mmoja wa eneo la Makambako Mkoani Njombe amefariki dunia kwa kukanyagwa na tairi za gari katika kichwa chake kutokana na kuanguka wakati akifukuzia basi linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kupata posho yake ya kupakia abiria.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema "Mpiga debe alikuwa amefuata fedha yake kwa ajili ya abiria aliokuwa amewapakia na kwa bahati mbaya ule malango wakati unajifunga alisukumwa na akadondokea kwenye uvungu na tairi za nyuma za gari ambazo zilimpitia”

RPC Issah ametoa wito kwa Wafanyakazi wa maeneo ya stendi kuwa makini na kuangalia usalama wao wakati wa kufanya kazi zao.View attachment 2198339
Daaah marehemu hana sauti ila kuna namna ilitokea
 
Mtoto Salah Jackson (5) mwenye ulemavu wa viungo, mkazi wa kijiji cha Makiwaru, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kutokana na njaa na kisha mama yake mzazi kumzika kimya kimya usiku wa manane.
Mtoto huyo anadaiwa kuzikwa na mama yake mzazi aitwaye Rebecca Siowi (30) usiku wa kuamkia Aprili 22, 2022 nyumbani kwa bibi yake walikokuwa wakiishi yeye pamoja na mama yake baada ya mume kumtelekeza na watoto watano.

Tukio hilo liligundulika baada ya mtoto huyo kutoonekana jioni ya Aprili 21 nyumbani alikokuwa akiishi kwa bibi yake, ambapo bibi yake huyo alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake huyo bila mafanikio ndipo Aprili 22 alipobainika kuwa amezikwa.

Akizungumzia tukio hilo leo Aprili 23, 2022 Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amekiri kuwepo kwa tukio hilo, akisema baada ya kupata taarifa hiyo kutoka kwa wananchi walifika eneo la tukio kuona sehemu alipozikwa mtoto huyo.
View attachment 2198344
Kuna watu wana ujasiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom