Makapuku Forum

Makapuku Forum

DJUMA SHABANI ANATISHA NDANI YA DIMBA

Na @EmanuelMwayomboJr

Djuma Shabani ni moja ya Mabeki wa pembeni wanaotisha katika ligi yetu msimu huu kutokana na kiwango Cha kuvutia ndani ya kiwanja akiwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya timu pinzani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao na kuisaidia Klabu yake ya Yanga.

Siku zote Djuma Shabani akivuka mstari wa katikati ya Kiwanja hugeuka kuwa kama kiungo mshambuliaji mikimbio yake kuelekea katika eneo la wapinzani wake huwa na faida kubwa kwa timu yake ndiyo maana mara nyingi kwa sasa mabao ya Yanga hutengenezwa kutoka upande wa kulia eneo ambalo Djuma Shabani husimama.

Djuma Shabani huyu ni mwalimu wa kupiga krosi sahihi katika box la wapinzani kwa upande wa Mabeki wa pembeni katika ligi yetu kwa sababu ana uwezo wa kupiga Mpira mrefu na ukafika eneo sahihi mfungaji akatupia (hapa Mayele kafaidika zaidi) pia ana uwezo wa kupiga krosi za chini nazo zikawa na faida kwa timu yake tofauti na Mabeki wengine wa pembeni ambao mara nyingi Mipira yao huishia kwa Mabeki wa timu pinzani hivyo katika eneo hili Djuma ni mwalimu wao hakuna kama yeye.

Mfalme wa zamani wa kabila la Hun (Attila the Hun) aliwahi kusema siyo vibaya kujifunza kwa aliye kuzidi hivyo ni wajibu wa Mabeki wa pembeni kujifunza kutoka kwa Djuma Shabani kama wakiweza kucheza kama anavyo cheza mwamba huyu itakuwa na faida kubwa kwa Vilabu vyao na Taifa letu.

Katika ulimwengu soka hivi sasa Mabeki wengi wa pembeni hutumika kutengeneza nafasi za kufunga huku mawinga wakigeuka kuwa wafungaji zaidi hivyo Djuma Shabani anatupa somo unaweza kuwa mlinzi wa pembeni na ukawa kinara wa Assist kama ambavyo yeye ameshafanya akiwa katika ligi ya DR Congo.
Screenshot_20220408-150649_Instagram.jpg
 
Shaffih Dauda

Iconic celebrations

Mbunge @jerrysilaa ameweka style ya Mayele Fiston, raia wa Congo anaecheza Yanga

Mbunge @babutale ameweka style ya Sakho, raia wa Senegal anaecheza Simba

Well! Mayele tayari amekula mkataba wa matangazo pale GSM kwenye maduka yao, hii imetokana na ubora wake uwanjani na sanaa yake ya ushangiliaji, anavuna pesa zake

Huyu POS wa Simba ni muda wowote kama ataendelea na ubora wake basi kwa style yake ya chumvi kama Serge Gnabry basi anaweza kupata matangazo kama ya chumvi, ni pesa hizi

Well, wageni wamekuja kwetu kucheza mpira, kuvuna pesa za mpira na kuvuna pesa za nje ya mpira ila sisi tupo tumetulia! Ofcourse Mchezaji hupewi endorsement kisa kipaji sana bali nje ya kipaji kuna kipi nyuma?

Watu hawaendi kwa Cristiano Ronaldo kisa mabao, bali wanaenda kwakuwa ana kitu extra nyuma ya kipaji, tuna kazi kubwa ya kufanya football iwe profession yenye pesa nyingi

Ni suala langu, letu na sote pamoja kuwa na workshops kwa ajili ya wachezaji wetu wazawa ili tupige hatua kubwa

WHEN DIGALA SPEAKS???______
Screenshot_20220408-150804_Instagram.jpg
 
Baada ya Wayne Rooney kutoa mtazamo wake kuhusu Cristiano Ronaldo ambapo Rooney alisema;

“Ronaldo anafanya vizuri sana ila sio Ronaldo yule akiwa kwenye miaka 20” akielezea kuhusu Ronaldo na Manchester United

Ajabu ni kuwa Ronaldo alienda kucomment kwenye post hiyo kwenye ukurasa wa SKY SPORTS kwa kuandika “Two jealous” ambapo tafsiri ya haraka ni Wayne Rooney na Jamie Carragher (Legend wa Liverpool) kuwa wawili hao wana wivu

Rooney alijibu jana kuhusu comment hiyo ya Ronaldo kwa kusema;

“Kila Mchezaji ni lazima awe na wivu na Ronaldo, magoli aliyofunga, makombe aliyobeba, tuzo nyingi lakini pia ana six packs, hata Messi anamuonea wivu Ronaldo” alimaliza Rooney
Screenshot_20220408-150934_Instagram.jpg
 
Mara ya mwisho kwa Super Ben kufunga bao kwenye mechi ya ligi kuu ilikuwa Mei, 2021

Baada ya miezi 11 jana amefanikiwa tena kuweka kimiani kwenye mchezo wa Coastal dhidi ya Simba
Screenshot_20220408-151119_Instagram.jpg
 
Mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya SIMBA dhidi ya ORLANDO PIRATES unaotarajiwa kuchezwa Aprili 17, 2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, waamuzi watatumia msaada wa video [Video Assistant Referee-VAR] pale itakapobidi kutumia ili kuhakikisha maamuzi yanakuwa sahihi.

Tayari orodha ya waamuzi wa mchezo huo imeshajulikana sambamba na wale watakao ongoza VAR.

Orodha ya waamuzi hao ni kama ifuatavyo;

Referee: Haythem Guirat (Tunisia)
Assistant Referee 1: Khalil Hassani (Tunisia)
Assistant Referee 2: Samuel Pwadutakam (Nigeria)
Fourth Official: Sadom Selmi (Tunisia)
Video Assistant Referee: Ahmed Elghandour (Misri)
Assistant VAR: Youssef Wahid Youssef Misri.

Tayari kila anayehusika na mchezo huo ikiwa ni pamoja na vilabu, wameshapewa taarifa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) juu ya uwepo wa matumizi ya VAR kwenye mchezo huo.

VAR itatukika kwenye mechi zote za timu zilizofuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CAF.
Screenshot_20220408-151233_Instagram.jpg
 
Wakati waamuzi wa mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na Orlando Pirates, Jumapili Aprili 17 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwekwa hadharani, Simba imeruhusiwa kuingiza jumla ya mashabiki 60,000 katika mchezo huo.

Idadi hiyo ndio ukomo wa mwisho wa namba ya mashabiki ambao Uwanja wa Benjamin Mkapa inaweza kuingiza katika mechi moja.
Habari za uhakika kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na lile la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimefichua kuwa Simba imeruhusiwa kuingiza idadi hiyo ya mashabiki baada ya kupeleka ombi CAF.

"Simba wameruhusiwa kuingiza jumla ya mashabiki 60,000 Jumapili, Aprili 17 katika mechi yao dhidi ya Orlando Pirates," kilithibitisha chanzo chetu.
Screenshot_20220408-151536_Instagram.jpg
 
UONGOZI wa timu ya Pamba ya Mwanza umekiri kuwa hatua ya kuahirisha mchezo wa hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba umevuruga mipango na ratiba yao lakini wamekubali yaishe.

Mchezo huo ulipaswa kuchezwa Aprili 13 mwaka huu saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo taarifa kwa umma ambayo imetolewa leo asubuhi na Pamba imesema mchezo huo umehairishwa na utapangiwa tarehe mpya baada ya wenyeji Simba kuomba kwa ajili ya kupata muda wa kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini utakaopigwa Aprili 17 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Afisa Habari wa Pamba, Moses William amesema walikuwa wameshafanya maandalizi mbalimbali kwa ajili ya mchezo huo ikiwemo kuandaa mchezo wa kirafiki ambao ungechezwa usiku jijini Dodoma ili kuwaandaa wachezaji wao kuzoea mazingira ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ambako mchezo wao ungechezwa usiku.

"Japokuwa tulikuwa hatujaondoka Mwanza lakini tulikuwa tumeshaanza maandalizi ikiwemo mchezo wa kirafiki ambao ungechezwa usiku katika moja ya mikoa ambayo tungepita tunakwenda Dar es Salaam, lakini sasa hakuna namna tunajipanga na mechi ya ligi dhidi ya JKT Tanzania Aprili 17," amesema.

Screenshot_20220408-151709_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom