Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220408-073021_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220408-073035_Opera%20Mini.jpg
 
Ed Sheeran ameshinda kesi ya hakimiliki nchini Uingereza iliyokuwa imefunguliwa kuhusu wimbo wake wa mwaka 2017 wa “Shape of You” ambao ulidaiwa ku-copy sehemu ya wimbo wa "Oh Why" uliofanywa mwaka 2015 na Sami Switch.

"Ingawa tunafurahishwa na uamuzi huu, ninahisi kama madai kama haya ni ya kawaida sana sasa na yamekuwa utamaduni huku yakifanywa kwa mawazo kwamba suluhu itakuwa nafuu kuliko kupelekana mahakamani hata kama madai yenyewe hayana msingi" alisema Sheerhan.

Andrew Sutcliffe ambaye ni Wakili wa Waandishi-wenza wa "Oh Why'' alisema kulikuwa na "ufanano usiopingika kati ya nyimbo hizo mbili na kudai kwamba Sheeran alikuwa na "Oh Why" wakati akiandika "Shape of You" mwaka 2016 wakidai kiitikio cha "Oh I, Oh I, Oh I" kwenye "Shape Of You" kilikuwa "kinafanana sana" na mstari "Oh why, Oh why, why" katika wimbo wao.

Wakati wa kesi hiyo ambayo ilidumu kwa siku 11, Jaji wa Mahakama Kuu Antony Zacaroli alihitimisha kwa kusema kwamba Sheeran "si kwa makusudi au kwa ufahamu" alinakili kifungu cha maneno kutoka "Oh Why" alipokuwa akiandika wimbo wake.

Sheeran na wenzake ambao ni McDaid na Mac walisema katika taarifa yao kwamba gharama ya kesi hii ilikuwa zaidi ya pesa kwa sababu ya stress za kujua kwamba wanatakiwa Mahakamani na hiyo inaumiza ubunifu na kuathiri hisia.
Screenshot_20220408-080709_Instagram.jpg
 
Waandamanaji nchini Ujerumani wanaishinikiza serikali yao kukubali kutonunua mafuta na gesi kutoka Urusi huku wakisema fedha wanazozipata Urusi ndizo zinafadhili vita, mauaji na uteswaji wa raia Ukraine.



Screenshot_20220408-080906_Instagram.jpg
 
Azimio la kihistoria limepitishwa leo na #UNGA kusimamisha uanachama wa Urusi katika Baraza la Haki za Kibinadamu na kueleza wasiwasi wake kuhusu haki za binadamu na mgogoro wa kibinadamu unaoendelea nchini Ukraine.

Nchi 93 zimepiga kura ya kuunga mkono Urusi kuondolewa, huku nchi 24 zikipiga kura ya hapana kupinga Urusi isiondolewe na nchi 58 hazijafungamana na upande wowote, Tanzania ni miongoni mwa nchi 58 ambazo zimepiga kura ya kutofungamana na upande wowote.

Waliopiga kura ya kutaka Urusi asiondolewe kwenye Baraza la Haki za Binadamu ni pamoja na Korea Kaskazini, Congo, Burundi, Algeria, Mali, Belarus, Zimbabwe, Ethiopia, Bolvia na nyingine ambazo jumla ni 24
Screenshot_20220408-081015_Instagram.jpg
 
Hukumu ya Mwimbaji R.Kelly ambayo ilikua isomwe May 4 2022 New York Marekani baada ya kupatikana na hatia katika makosa tisa ya ulaghai na ulanguzi wa ngono, imeahirishwa hadi June 16 2022 kutokana na ripoti ya kabla ya hukumu kuchelewa kuwasilishwa.

Vyombo vya Marekani vimesema kwa makosa haya aliyoyafanya New York miaka iliyopita anaweza kufungwa jela maisha ambapo hata hivyo hii sio kesi pekee inayomkabili Robert Sylvester Kelly kwani anayo kesi nyingine ya shirikisho huko Chicago ambayo imepangwa kuanza Agosti 1 2022.
Screenshot_20220408-081203_Instagram.jpg
 
Gumzo jingine mtandaoni ni video fupi inayosambaa ikimuonesha Kijana Raia wa Congo aitwae Muima akitangaza kwa ujasiri kwamba anafunga ndoa na Mpenzi wake aitwae Thereza ambaye ni Bibi wa miaka 85.

Mtandao wa Citizen Kenya umemnukuu Muima akiongea na Mwandishi wa habari na kusema maneno yafuatayo “Sitachagua yeyote badala yake ingawa yeye ni Mwanamke mzee na kwa kweli anaweza kuwa bibi yangu lakini bado ninampenda, hili ni chaguo langu, hii ni furaha yangu na kabla ya kuwafurahisha wengine kwanza jipende mwenyewe sio kwa kuzingatia maoni ya Mtu mwingine."

Akisimulia mahusiano yao, Muima alisema kuwa mara ya kwanza yeye na marafiki zake walikuwa wameenda kuwinda karibu na nyumba inayomilikiwa na Thereza ambapo baada ya miezi michache kupita ndipo Thereza akaanza kumpenda.

Thereza ana watoto nane na Wajukuu 20 na anasema anatarajia kuolewa na mpenzi wake huyo wa siku nyingi “nina Watoto nane na Wajukuu 20, kulingana na umri wa Mpenzi wangu anaweza kuwa Mjukuu wangu wa tano, ananipenda na mimi nampenda, niko tayari kuvaa vazi la harusi na pete katika siku yetu ya harusi" #MillardAyoUPDATES via Citizen Kenya.
Screenshot_20220408-081325_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom