

Shaffih Dauda
Nilisema kitu kuhusu thamani ya Mchezaji na namna gani ambavyo anaweza kutengeneza pesa kupitia thamani yake, nilisema kuhusu mikataba lakini pia kuhusu corporates
Nilisema Mchezaji ni vyema akawa na viungo muhimu zaidi kwake, ambao ni WAKALA na Mwanasheria, kwakuwa hizi ni field muhimu zaidi kwenye football
Kwanini wachezaji wetu wengi wazawa wamekuwa wakilia kuhusu mikataba, kuhusu pesa wanazolipwa na wengi wakiamini hawapewi thamani kama wapewavyo wageni?
Majibu ni kuwa wanakosa Professionals wa kusimama kwa niaba yao! Mchezaji wetu anachojua ni kusaini na kuchukua pesa kisha kuondoka, hapitii mkataba, hasomi kilichomo yeye anaanguka tu saini
Wakati mwingine Mchezaji hafahamu hata umuhimu wa kutia saini kila page yake ya mkataba, wakati mwingine Mchezaji hapitii vifungu (clause) za kimkataba, ambazo zingine ni kandamizi
Mfano wengi hujifunga kwenye IMAGE RIGHTS (Haki za picha zao) nyingi hutumika bureee, wengi hujikuta wakipromote bidhaa ambazo dunia ya kimpira kwasasa zinaenda kwa mfumo wa comission, lakini huku ni ngumu kwakuwa hatuna watu muhimu nyuma yetu
Huku kwetu Mchezaji anacheza akiwa na stress kuwa anamaliza mkataba, akiwa na stress za pesa nzuri (Greener pasture) lakini vyote hivyo anapaswa kupigana mwenyewe, lakini ukiwa na WAKALA yeye anasimama kwa niaba yako kwakuwa ni Business, deals anakuwa nazo tayari
Ukiwa na Mwanasheria wako yeye ndie mtu wa kukutafsria kilichomo kwenye mkataba, yeye atakuelekeza kuhusu muhimu wa INITIALS kila ukurasa, yeye ndie anajua utaondoka vipi ukiwa ndani ya mkataba, hizi zote ndio dunia ya mpira
Mmoja atasema wachezaji hawana pesa ya kuwa na watu wote hao! Well simple, lakini mfumo wa dunia hivi sasa ni partnership, watu watasimamia deal na kuvuna kitu kutokana na deal, baada ya hapo watapambana tena
Tuwaambie kweli wachezaji wetu, mikataba ni CONFIDENTIAL sana, inahitaji akili sana ili kupata maslahi ya kimpira, nje na hapo tutaendelea kulalamika tu, WE NEED TO CHANGE
WHEN DIGALA SPEAK YOU LISTEN