

Shaffih Dauda
Kwenye nchi kama Tanzania kuna michezo mingi na wanamichezo wengi sana, hoja yangu ni kiwanda cha michezo kama biashara nje ya uwanja, uringo au court
Kampuni zinawekeza pesa au kutoa mikataba ya wadhamini kwa kutazama, POTENTIAL ya mchezo husika, RASILIMALI ya mchezo husika na mwisho MODE OF THE SPORT, nikimaanisha ni mtu mmoja mmoja au ni timu?
Hiyo ni sehemu ya kwanza, sehemu ya pili ni kuwa ICON IN SPORTS, yani kwenye michezo hiyo ni Staa?? Hapa watu hupenda kutumia neno COUNTRY STAR, mfano kwenye Football hii Tanzania tuna Mbwana Samatta ambaye alikuwa na endorsement na kampuni ya vinywaji
Kwenye country star kuna vingi wanavitazama, lakini inaweza kutokea nchi ikawa na Mastaa wengi tu na watu wakawatumia kama nembo zao kibiashara na kujipigia pesa nyingi nje ya mchezo wao
Mfano kwenye boxing namtazama sana Hassan Mwakinyo namna anavyojitofautisha, Boxer kama huyu ni rahisi kuwa COUNTRY STAR kwenye mchezo wake, nakumbuka aliwahi kuwa na mkataba mzuri sana na kampuni moja wapo nchini, anajibrand sana
Kuna kitu wanamichezo wetu wanapaswa kukibadilisha, kuamini ukiwa na Management basi pesa hupati nyingi ila HAPANA, unahitaji kuwa na watu wanaopush vitu vyako binafsi na kusimama kwa niaba
Wengi huamini jina ndio linauza hiyo ni HAPANA, kwenye dunia yetu Kampuni hufanya kazi na Wataalam, mfano Mtu wa masoko wa mchezaji anaweza kudraft proporsal akaipeleka kwenye kampuni kadhaa kisha akaidefend, mnapata endorsement nzuri tu
Kosa ni kuamini kuwa Kampuni zinafuata jina, kampuni zinafuata system na profesionalism, ikitokea tofauti wakupigie mchezaji ambaye una majukumu labda kuelekea kwenye game? Jibu ni HAPANA, wanaconsult na Menejiment au muwakilishi wako
Tumia akili kidogo, mpe mtu kazi, mpe copyrights zako akasake endorsement kisha mnagawana asilimia flani, hivi mnafahamu kuwa Ronaldo na Mendes hivi sasa ni Business Partners?? Mendes analeta dili, wanagawana percent na maisha yanaenda
Kama Ronaldo anafanya kwanini sio wewe? The corporate world works differently from streets
DIGALA WAS HERE