Makapuku Forum

Makapuku Forum

ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
.
Hizi hapa timu 7 zilizotangulia kutinga hatua ya Robo Fainali hadi sasa::

CR Belouizdad
ES Setif
Petro Atletico
Raja Casablanca
Wydad Casablanca
Mamelodi Sundowns
Espérance de Tunis
.
Nafasi moja imebaki kati ya Al Ahly vs Al Hilal
Screenshot_20220320-090303_Instagram.jpg
 
SAIDO AAGA UKAPERA
.
Wakati Yanga usiku wa jana ilikuwa uwanjani kuvaana na KMC katika mechi ya Ligi Kuu, nyota wake kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza alikuwa akiuaga ukapera kwa kufunga ndoa na bibie Uwera Samantha.
.
Screenshot_20220320-090514_Instagram.jpg
 
CAF CONFEDERATION CUP
.
ASEC MIMOSAS SIMBA SC
19:00
Stade de I’mitie
.
Msimamo Kundi D
1. Simba — 7
2. Berkane — 6
3. Asec Mimosas — 6
4. US Gendermarie — 4
Screenshot_20220320-090614_Instagram.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

Asec Mimosas vs Simba SC ( CAFCC ).

Ni mechi ngumu kwa timu zote mbili, Asec ni mwenyeji kikanuni lakini kimazingira ni mgeni kama Simba, wote wanacheza katika ardhi ya ugenini nchini Benin.

Katika mechi tano za mwisho Asec hawana wastani wa kutisha katika kufunga magoli, hiyo si sababu inayoweza kuwafanya Simba wa-relax, Asec wamefunga magoli sita katika mechi tano, wastani wa goli moja kwa kila mechi na kubaki moja.

Kwanini ni vizuri Simba wakiingia na 3-4-3?, ni mfumo unaohusisha walinzi watano lakini si kama wanazuia muda wote muda mwingi, Chelsea inatumia walinzi watano ambao ni Antonio, Thiago, Cesar, Reece na Alonso na hawapaki basi.

Kwenye football kuna roles and position ( nafasi na majukumu ), mfano inawezekana position yako ikawa ni kucheza mbele ya mabeki lakini jukumu lako likawa kuchezesha timu na hapa ndipo wanapoingia viungo aina ya deep lying playmakers mfano Jorginho, Jorginho anacheza mbele ya mabeki lakini jukumu lake mama ni kuchezesha timu na hapa ndipo inapokuja tofauti ya nafasi na majukumu ( roles and position ).

3-4-3 inakuwa na walinzi watano lakini wawili wanacheza kama wing backs in roles yani wachezaji ambao wakati timu inashambulia wanabadilika na kuwa mawinga wa asili, majukumu yao ni kufanya mikimbio katika half spaces au kutengeneza overloads kwenye wings na pia wanaweza kuwa chiefs creators wa timu ( watengezaji wa nafasi za kufunga ) huku midfielders ( viungo ) wakicheza katika nidhamu ya kulinda nafasi ( positional play ).

Asec ni wazuri wanapokuwa na mpira, ili kuwadhibiti unahitaji angalau vitu viwili, fanya pressing ( kuweka presha kwenye mpira ) au vunja njia za pasi ( cut the passing lane ) kutoka kwa mchezaji A kwenda kwa B, Simba wakiwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye midfield watapata numerical advantage na kuwarahisishia kufanya mambo hayo mawili kwa ufasaha.

Ukiwa na central midfielders wawili, wing backs wawili hapo utatengeneza 3 vs 4 na kama kila mchezaji atatekeleza majukumu yake kuna asilimia kubwa ya kufanikiwa kuliko kufeli, kumbuka pia nyuma kuna walinzi watatu ambao wanazuia zaidi, kitu cha msingi zaidi kwa Simba ni kuulinda mpira.
Screenshot_20220320-090859_Instagram.jpg
 
Hii battle ya TOP FOUR ni ya moto sana pale EPL, mtu akiteleza tu basi kaliwa mwakani UEFA kwenye bomba

Hapo Arsenal, Manchester United na Tottenham hawapo kwenye michuano ya kimataifa

West Ham na Chelsea bado wana vipute vya Ulaya, waendelee kupambana huku hofu kubwa ikiwa uchovu na majeraha
Screenshot_20220320-091036_Instagram.jpg
 
SIMBA CHUNGENI HAWA WAWILI
.
Stephane Ki -
Karim Konate -
.
Katika mechi ya leo Simba inapaswa kuwa makini sana na mastaa wawili wa Asec; Stephane Ki na Karim Konate ambao kwa pamoja wamefunga mabao matano kati ya sita iliyofunga hatua ya Makundi.
.
Ki ndio aliifungia Asec bao pekee katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ambao Simba ilishinda mabao 3-1.

Screenshot_20220320-112830_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom