Farhan jr
LIONEL MESSI NA ANTONELLA, MAANA NYINGINE YA MAPENZI - PART 2
Wakati wapo zao njiani na Mshikaji wake Lucas, huku wakipiga stori mbalimbali huku wakipitia EP ya Diamond ule usiku wa mbalamwezi pale Rosario, hatimae wakakaribia getini nyumbani kwa wakina Antonella
Walipokelewa na Dada zake Antonella ambao ni Carla na Paula, huko Lucas akiwachangamkia sana Binamu zake! Bila kusahau Messi alikuwa tu mkimya anaendelea kuwatazama wakiwa wanakumbatiana
Lucas kama ilivyo kwa watoto, akamsahau Mshikaji wake Messi yeye akawa busy na Binamu zake wawili, huku Messi akijiinamia kwenye kiti akisubiri zoezi la msosi, ale kisha waondoke zao
Wakati wote huo Messi akiwa mpweke, Antonella alikuwa akimtazama tu! Ikabidi atoke kwenye kiti chake na kujongea mpaka alipo Messi, kisha akamsalimia na kuketi pembeni yake, Messi alikuwa mwingi wa aibu
Lucas anasema ni kama vile Swahiba wake alitamani ardhi ipasuke aingie ndani, mdomo ulijaa mate na sauti ilikuwa haitoki kwa usahihi, wote huo ulikuwa ni uoga na aibu, kiukweli Messi alituangusha sana mwanzoni
Ndio vile Mungu hakupi vyote na akikupa kilema basi anakupa na mwendo! Ingekuwa watoto wetu wa Bongo, angechangamka kama wanajuana miaka mingi, huenda angetupia voko hapo hapo! Ila sio kwa Messi
Wakati Antonella anampigisha stori Messi, Lucas alikuwa akicheka muda wote jinsi Gwiji alivyotulia, sio yule Messi wa uwanjani akilambisha wachezaji nyasi, akikimbia kama mshale na kufunga mabao ya kideo
Lakini licha ya ugumu wote, usiku ule ndio ulikuwa mwanzo wa Messi kuzoeana na Antonella, taratibu wakaanza kupeana nafasi, kuonana na kucheza wote mitaani Rosario wakiwa na umri wa miaka tisa tu
Wakati Messi akiwa kwenye kiwango bora sana, baada ya miaka kama miwili wakati ametimiza miaka 11, alipokea taarifa mbaya sana ambayo iliwaumiza familia yake mpaka Antonella
Jioni moja wakati Messi kakutana na Antonella…..
ITAENDELEA……..