Makapuku Forum

Makapuku Forum

IBENGE: SIMBA HII INAWEZA KUFIKA FAINALI
.
“Simba SC kwa misimu minne sasa wamepata wasaa wa kucheza michezo migumu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, imewajenga vyema hivyo kwa msimu huu kucheza katika kombe la Shirikisho naamini wanaweza kufika fainali na hata kuchukua ubingwa.
.
“Simba wamejiandaa vizuri, ni wazi inaonesha wana kikosi imara na chenye malengo makubwa, hivyo nilitarajia upinzani tofauti.” amesema Ibenge ambaye hadi sasa hajui hatima ya kibarua chake huko Berkane.
Screenshot_20220314-103951_Instagram.jpg
 
HERSI: YEYOTE ANAUZWA TU
.
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said amesema hakuna mchezaji atakayezibiwa riziki kama atatakiwa na timu ya nje au klabu nyingine ya ndani ilimradi taratibu zifuatwe.
.
“Hatuwezi kuwabania wachezaji hata kidogo. Yeyote atakayepata nafasi ya kutoka tutamuachia atoke akajaribu maisha kwingine. Mpira sikuhizi ni zaidi ya ajira.
.
“Tulimuuza Kisinda kwa kuvuna dola 150,000 kupitia mauzo ya mchezaji mmoja tuliwanunua mastaa watatu Djuma Shabani, Fiston Mayele, na Jesus Moloko wote wanafanya vizuri.
Screenshot_20220314-104119_Instagram.jpg
 
POGBA ANASEPA ZAKE MANCHESTER
.
Kocha binafsi wa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba anayefahamika kwa jina moja Maddy amesema staa huyo ataondoka msimu huu mkataba wake utakapokwisha na hakuna mjadala kuhusu hilo.
.
“Hadi itakapofika Juni, Pogba atakuwa ameshaondoka. Hatakuwa mchezaji wa Man United. Nafikiri anastahili kuondoka na kutafuta mafanikio sehemu nyingine, pengine Man United inataka kumpa mkataba mwingine, kwa upande wangu bora watengane. Muda utafika na kila kitu kitabadilika, mchezaji mkubwa hawezi kupoteza muda kwa mashindano madogo,” amesema Meddy.
Screenshot_20220314-104222_Instagram.jpg
 
Uwanja wa Moulay Abdellah uliopo katika mji wa Rabat nchini Morocco umeharibiwa vibaya kutokana na fujo zilizojitokeza katika mechi ya 32 bora kuwania Throne Cup ambayo iliwakutanisha FAR Rabat dhidi ya MAS Fez.

Katika mechi hiyo FAR Rabat ilipoteza kwa jumla ya mabao 2-0, katika tukio hilo mashabiki wa FAR Rabat walivunja uzio wa uwanja huo na kuingia ndani ya uwanja na kufanya fujo hizo ambazo zilipelekea uwanja kuharibiwa vibaya.
Screenshot_20220314-104556_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom