Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.

Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.

Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”
Screenshot_20220312-171839_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya dereva bajaji Mkazi wa Miuji aliyeuawa kwa kupigwa na kipande cha bomba la chuma nyuma ya shingo yake huku ikielezwa kuwa chanzo cha tukio ni ugomvi uliotokana na marehemu (enzi za uhai wake) kudai kurudishiwa chenji yake Tsh. 400 baada ya kutoa Tsh. 500 kununua sigara moja inayouzwa Tsh. 100.

Aidha Polisi Dodoma wanaendelea kufuatilia tukio la mauaji yaliyotokea March 9, 2022 eneo la Mtumba Jijibi Dodoma ambapo mwili wa Mwanamke mwenye miaka 40 mfanya usafi mkazi wa Mtumba ulikutwa mtaroni akiwa ameuawa baada ya kukabwa shingo na kubakwa.
Screenshot_20220312-172107_Instagram.jpg
 
Youtube imesema inafunga uwezekano wa Watu Duniani kote kutazama channel zote ambazo zinafadhiliwa au kumilikiwa na Serikali ya Urusi kufuatia Urusi kuivamia Kijeshi Ukraine.

Mtandao huo unaomilikiwa na Alphabet Inc's Google umesema kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine kinameingizwa kweny ukiukwaji wa maadili ya Youtube na video zote za kutisha za matukio ya yanayojiri Ukraine zitaondolewa.

Awali Youtube ilitangaza kuzifungia Channel za Urusi za RT na Sputnik Barani Ulaya pekee.
Screenshot_20220312-172230_Instagram.jpg
 
"Kamati Kuu ya CCM imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa Polisi nchini ambao hauridhishi na kulalamikiwa na Wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na Maofisa na Maaskari wa Jeshi hilo kinyume na mwongozo wa utendaji kazi wa Jeshi hilo (PGO)”

"Kamati Kuu ya CCM imempongeza Rais Samia kwa kuunda Tume kuchunguza matukio ya uhalifu yaliyopelekea mauaji Tanga na Mtwara, Kamati Kuu pia imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa Polisi nchini ambao hauridhishi na kulalamikiwa na Wananchi" ——— Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM.
Screenshot_20220312-172342_Instagram.jpg
 
Marekani na washirika wake wameamua kusitisha uhusiano wa kawaida wa kibiashara na Urusi, huku Rais Joe Biden akiapa kuwa nchi za Magharibi zitamfanya Vladimir Putin alipe gharama ya uvamizi wake nchini Ukraine.

Biden ametangaza hatua hiyo mpya, ambayo itawezesha mataifa ya Magharibi kuweka viwango vya juu vya ushuru kwa bidhaa za Urusi, kwa uratibu na washirika wa NATO, Kundi la mataifa ya G7 na Umoja wa Ulaya.

Marekani na Ubelgiji pia zimesema kuwa zitakataza mauzo ya bidhaa za anasa kwa Urusi katika kile ambacho rais wa halamashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amekielezea kama pigo la moja kwa moja kwa matajiri wa Urusi. v
Screenshot_20220312-172508_Instagram.jpg
 
Rais Samia ametoa agizo kwa Waziri wa Katiba na Sheria kuunda kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya siasa.

Ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea maazimio ya awali kutoka Kikosi Kazi alichokiteua cha kufuatilia hoja zilizojitokeza katika Mkutano wa Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi Dodoma December 15 hadi 17,2021.

Rais Samia amemwagiza Waziri wa Katiba na Sheria kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) na Zanzibar Law Society (ZLS) kutengeneza kanuni hizo.
Screenshot_20220312-172623_Instagram.jpg
 
Rais wa Marekani, Joe Biden amesema Marekani na Washirika wake wameamua kusitisha uhusiano wa kawaida wa kibiashara na Urusi, huku Rais Joe Biden akiapa kuwa nchi za Magharibi zitamfanya Vladimir Putin alipe gharama ya uvamizi wake nchini Ukraine.
Screenshot_20220312-172728_Instagram.jpg
 
Hassan Kanema (45) mkazi wa Amani Gongo Stoo Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja amekutwa akiwa amefariki dunia chumbani kwake Kwa siku nne bila ya kufahamika kuwa amefariki huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakifahamiki hadi sasa.

Mwenyekiti wa Amani Gongo Stoo, Amani Maabadi amethibitisha "Wananchi tushirikiane usikubali kukaa pekee yako wakati unaishi na wenzio ili ukipata tatizo uwaaambie, kilichotokea ni kama maiti kanyimwa haki yake ya kusitiriwa maana Mtu akifariki lazima apate haki zake"

"Ana kawaida siku mbili tatu humuoni, siku hiyo tulikuwa tumegonga baada ya kupata wasiwasi kidogo, baadaye saa 4 akawa ameingia akiwa ameshika kiatu kimoja, tukamuuliza akasema kiatu kimoja nimekiacha ofisini Mtu akija ajue nipo, alipoingia hakutoka hadi tumekuja kukuta maiti" Mama mwenye nyumba, Bi Latifa
Screenshot_20220312-172923_Instagram.jpg
 
Baadhi ya Wanawake nchini Ukraine wameamua kutokimbia Nchi yao kama walivyofanya wenzao badala yake wanajitolea kuwapikia chakula Wanajeshi walio mstari wa mbele kupambana na Warusi.

Wanawake hao wanapika chai na vyakula vingine kupitia majiko ambayo wameyaweka pembezoni mwa Barabara Kaskazini Mashariki mwa Kyviv.

Mwalimu mmoja aitwaye Victoria Yermakova (45) na Mumewe ndio Wamiliki wa Majiko hayo na ndio walikuja na hilo wazo na wanasema kwa siku wanalisha Wanajeshi na hata Raia wa kawaida wanaopambania Nchi yao wapatao 5000 hadi 6000.
Screenshot_20220312-173129_Instagram.jpg
 
Nabi aliliambia Mwanaspoti, baada ya mazoezi ya juzi waliporejea kazini ripoti ya madaktari inaonyesha wachezaji wasiopungua wanne wamerejea kazini.

Yanga juzi ilianzia gym mara baada ya kutoka mapumziko ya siku mbili ikitoka kuichapa Geita Gold kwa bao 1-0 kwenye mechi iliyopigwa, jijini Mwanza wikiendi iliyopita na kwa mujibu wa Nabi amepokea ripoti ya kurejea kwa Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Khalid Aucho, Farid Mussa na Chico Ushindi, jambo ambalo kwake ni faraja kubwa.
Screenshot_20220312-173331_Instagram.jpg
 
KATIKA kuhakikisha analipa kisasi cha mabao 2-0 ilichopewa Simba ugenini na RS Berkane, Kocha wa Simba, Pablo Franco ametumia muda mfupi uliosalia kuwachora wapinzani wao hao kutoka Morocco.

Pablo ametumia muda wake na wasaidizi wake kuwasoma Berkane kupitia video za mechi zao ukiwamo ule wa baina yao uliopigwa Morocco, ili kupata dawa ya kuwamaliza Kwa Mkapa.

“Miongoni mwa vitu tulivyoona wanapokuwa nyumbani wapo tofauti na ugenini, huwa wanazuia zaidi na kumiliki mpira zaidi ili kujilinda na hata kushambulia kwao ni kwa nidhamu si kama inavyokuwa nyumbani,” alisema.

Screenshot_20220312-173437_Instagram.jpg
 
KAGERE: TUTAPAMBANA KUSHINDA
.
"Tunatambua ni mchezo mgumu, tunajivunia mashabiki wetu tunawaomba waje kwa wingi. Wachezaji tutapambana kushinda na kukaribia malengo yetu"
Screenshot_20220312-173704_Instagram.jpg
 
"Kikosini nina Yassin Mustafa, Feisal Salum Fei Toto, nimeshaanza kuwatumia, uchezaji wao sio ule wa nguvu, wanaonekana ni waoga, wanaogopa kuumia tena sasa nataka kutumia mchezo na Somalia kuwajenga ili wasiniangushe dhidi ya KMC"
.
"Kuna wachezaji wengine walikuwa nje ya uwanja sikuwatumia kwenye mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Geita Gold kwa matatizo mbalimbali wamerudi kama Chico Ushindi, Khalid Aucho, pia watacheza ili kujiweka fiti."
.
"Kuna timu kutoka Malawi, Kenya na Uganda tupo kwenye mazungumzo nazo tucheze mechi za kirafiki.

- Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi.
Screenshot_20220312-173757_Instagram.jpg
 
BOCCO KUIKOSA BERKANE, THADEO ANAANZA
.
Nahodha wa Simba, John Bocco hatakuwa sehemu ya kikosi dhidi ya RS Berkane na hakuwa sehemu ya mazoezi jana jioni kwani amepewa mapumziko kutokana na majeraha ya misuli ya nyuma ya nyama za paja aliyoyapata katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji na kushindwa kuendelea na mchezo.
.
Kulingana na mazoezi hayo taarifa njema katika kikosi cha kwanza Simba kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga anaweza kupewa nafasi ya kuanza kama hakutakuwa na mabadiliko.

………
Screenshot_20220312-173907_Instagram.jpg
 
Pitso ana kazi nzito sana, katoka tu kusaini kandarasi mpya juzi tu

Kwa matokeo yalivyo mpaka sasa Mamelodi wana alama 10 na Ahly wanazo nne pekee
Screenshot_20220312-174033_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom