Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Baadhi ya wasomi wamesema tabia ya baadhi ya wazazi kuwapeleka watoto wao shule za bweni za msingi kuna hasara nyingi kuliko faida.
Wakizungumza na Mwananchi, wasomi hao wamesema kuwa mwalimu pekee hatoshi kumjenga mtoto kimaisha
Walisema itakuwa bora kama watoto hao wakipelekwa shule za bweni wanapoingia kidato cha kwanza kwa sababu wanakuwa na akili za kujitambua.
Muhanyi Nkoronko ambaye ni mtafiti wa masuala ya elimu alisema watoto wadogo ni vyema waachwe chini ya uangalizi wa wazazi ili wajengwe kimaadili na kuelekezwa nini wanapaswa kufanya katika umri wao.
“Wazazi wengi wanapeleka watoto bwenini kwa kisingizio cha kukosa muda wa kukaa na watoto kutokana na kazi nyingi na wengine eti wanataka wapate muda zaidi wa kusoma lakini hasara ni nyingi zitakazowapata huko ikiwemo watoto kutokuwa wanaeleweka, kupata malezi duni na kujifunza tabia ambazo hazistahili,” amesema Nkoronko
Mwanasaikolojia Seby Wisdom amesema umri wa miaka mitano hadi tisa kwa mtoto huutumia katika kuangalia watu wanaomzunguka wanafanya nini na kuiga baadhi ya tabia zilizozoeleka
“Katika mazingira hayo ikiwa ni nyumbani na mama na baba wanaongea vizuri anajua ndiyo njia sahihi ya kuzungumza na kama wanaongea vinginevyo inakuwa sawa na hilo,” anasema Wisdom.

Hassan Shehata
Herve Renard
Stephen Keshi
Hugo Broos
Djamel Belmadi
Aliou Cissé