Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220208-180432_Instagram.jpg
 
Coastal mambo siyo mambo
.
Huko kwa ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union, katika michezo minne iliyopita ya Ligi Kuu Bara ambayo imecheza imepoteza yote hali ambayo inaonyesha dhahiri kuna upepo mbaya unaoikumba tofauti na mwanzo wa msimu huu.
.
Coastal ilianza na kichapo cha bao 1-0, kutoka Mtibwa, ilifungwa na Yanga bao 2-0, ikifungwa na Namungo bao 3-1, ikilazwa bao 2-1 na Kagera Sugar.
.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Melis Medo alisema; “Hatuko sehemu mbaya wala nzuri kwa sababu tumepishana pointi chache na walioko juu yetu, vita ndio kwanza inaanza maana tumebaki na mchezo mmoja kabla ya kuelekea mzunguko wa pili ambao huwa ni mgumu zaidi.”
.
Katika michezo 14 iliyocheza, Coastal imeshinda minne, sare tano na kupoteza mitano ikishika nafasi ya nane na pointi 17.
Screenshot_20220208-180604_Instagram.jpg
 
Imemchukua Aliou Cisse [Kocha wa Mzawa wa Timu ya Taifa ya Senegal] miaka nane (8) kushinda kombe kwa nchi yake. Senegal haikumfuta kazi wala kumwambia ajiuzulu, wala hawakuajiri kocha wa kigeni.

Muda wote alipewa ushirikiano wa kila aina kuandaa na kujenga kikosi imara ambacho kimefanikiwa kushinda taji la AFCON.

Hili ni somo kwa mataifa mengi ya Afrika kuamini watu wao, kuwapa ushirikiano, kuwa na subira, mafanikio yatakuja.

THE BLACK MAN CAN DO IT
Screenshot_20220208-220524_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom