TFF NI NYUMBA YA KUPANGA?
TFF ni taasisi yenye kusimamia maslahi ya mpira wetu, TFF sio nyumba ya kupanga ambayo Baba mwenye nyumba aseme hiki tufanye hiki tusifanye hata kama hakina maana
TFF sio nyumba ya kupanga ambayo Mwenye nyumba aseme leo nyama hapana, aseme sitaki Mtu abandike picha ukutani na kuhojiwa kusiwepo! TFF ni mali yetu wote
Shida kubwa iliyopo Shirikisho ni mentality ya nyumba ya kupanga, wakisema kitu sisi Wapangaji tusihoji kwakuwa hatukuchangia tofari wala madirisha, wala hatukutoa mia ya uwanja, SIO KWELI
Wakati mmesaini mikataba yote klabu hawajui kitu zaidi ya kupelekewa figure na kuambiwa watekeleze, hakuna kuhoji bali kutekeleza, huo sio uongozi bali DICTATORSHIP
Klabu zimeenda kutekeleza kitu ambacho hawajui msingi wake, ndani ya miaka miwili wadhamini wawili wanaondoka bila fidia kwa klabu, shida kubwa ikiwa ni ninyi TFF na Mentality za BABA MWENYE NYUMBA
TPLB ipo kwa ajili ya maslahi ya klabu zote ila mmeitoa meno, mmeifanya kama kamati na ninyi mmejipa majukumu yote, TPLB haina Viongozi bali CEREMONIAL LEADERS, Kila kitu kinafanyika Karume
Matokeo yake ndio haya! Mguto hana makosa, Kasongo hana makosa tena wasipewe jumba bovu tatizo lote ni ninyi hapo KARUME, ndio maana siku zote huwa nawaambia bodi iwe huru isajiliwe kama Kampuni
Kila siku agenda lakini mpo kwenye total failure! Nyie msimamie mpira, nyie msimamie timu za taifa, nyie msimamie Ligi, Guys muelewe DIVISION OF POWER haikwepeki, mjitathimini ikiwemo hata kujiuzulu sio kwa ubaya
Kila mkataba kisheria ambao TPLB atasaini ninyi mnapata 10% kisheria, tatizo nini mtake kila kitu mfanye ninyi??? Kuna siri gani ambayo hatuijui
Whenever we are given an oppurtunity to elect leaders, we are given a blank cheque! We elect hyenas to take care of goats
When DIGALA speaks????_______