Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kila la heri mnyama
Screenshot_20220126-112823_Instagram%20Lite.jpg
 
Farhan Jr

Homeboy Shomari Kapombe yupo kwenye ubora kwa muda mrefu sana, lakini kama Binadamu ana muda hajapumzika, Kila akiamka ni juu ya siti za Bus au Ndege kuelekea uwanjani

Hana wa kumlaumu zaidi ya kulaumu ubora Mkubwa aliokuwa nao, Yes! Ni kifurushi kamili cha beki wa pembeni, chini ya mstari na juu ya mstari, bado Simba hawajapata anaekaribia

Kapombe ni utamaduni sahihi wa Simba, ndio a Ball playing defender kama yeye! Ndio utamaduni huo tangu zama za Victor Costa, Pawasa, Christopher Massawe, wanamaliza mechi jezi haijachafuka

Nawaelewa Simba walipomleta Israel Patrick Mwenda kwenye kikosi, wakihitaji kile ambacho Shomari anawapa lakini kinahitaji muda, katikati ya muda na mafanikio ni uvumilivu, wampe Kijana muda atavaa viatu

'Ubaya' wa Simba ni kuwa haijawahi kubadilika, ni eidha ubadilike kuendana na Mfumo au Mfumo ukubadili au Mfumo ukutupe, Simba haijawahi kumtupa Mchezaji bali Mfumo tu unamtupa

Kuna kipindi Watu mlikuwa mnahoji kwanini Zimbwe Jr au Kapombe wa Stars ni tofauti na Kapombe wa Simba?? Well simple ni Mfumo, kuna identity ya Simba ambayo haijawahi kubadilika

Unataka kuamini?? Basi kumbuka wakati Sven anashinda mechi ila timu haichezi vyema, Mashabiki walikuwa wanamind sana, Simba anataka kushinda na kucheza vizuri

Simba wana Mfumo wao na Wachezaji wao, ndio maana Homeboy kupumzika itakuwa ngumu kwa muda, Mfumo unamuhitaji sana

Ndio maana hata Chama aliporejea na kuanza dhidi ya Mtibwa 'Real Madrid' ni kama vile alikuwepo muda wote, simply ni kuwa Simba ni Mfumo nae anafit mfumo wao
Screenshot_20220126-152914_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom