Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,937
MSIKIE TRY AGAIN KUHUSU KIBARUA CHA KOCHA PABLO FRANCO
.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amezungumzia Kuhusu kocha Pablo Franco kunyooshewa vidole na baadhi ya mashabiki, Try again amesema kocha hana shida.
.
“Kocha amechukua ubingwa wa Mapinduzi, amefanya vizuri kwenye mechi nyingi tangu alipojiunga na Simba, sioni tatizo la kocha.
.
“Japo nasisitiza si jambo la kawaida kwa Simba kupoteza mechi mfululizo, inaumiza na yanamuumiza kila mwana Simba hivyo tunaangalia nini cha kufanya.
.
“Kama klabu tutafanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi, mashabiki na wapenzi wa Simba watulie Simba ina viongozi makini na tutapata majibu sahihi kwenye hili,” amesema.
.
Kuhusu kuuweka rehani ubingwa, Try Again amesema “Ndio kwanza tuko kwenye mechi za mzunguko wa kwanza, bado tuna mechi nyingi msimu huu ambazo tunaamini tukijipanga vizuri tutatetea ubingwa wetu msimu huu,”.