Makapuku Forum

Screenshot_20220127-045647_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220127-045704_Opera%20Mini.jpg
 
Baadhi ya Watu wametoa wito kwa Jumuiya za Kimataifa kumdhibiti Bilionea Elon Musk na kasi yake ya teknolojia na urushaji wa roketi ili kuiepusha Dunia na majanga hii ni baada ya roketi ya Bilionea huyo kuonesha inakaribia kugonga ndani ya mwezi na kulipuka.

Mtaalamu wa Software, Bill Gray amesema Roketi hiyo inatarajia kugonga mwezi na kulipuka March 04,2022 lakini anasema athari yake itakuwa ndogo.

Roketi hiyo (Falcon 9 ) ilikwenda katika anga za juu mwaka 2015 lakini baada ya kukamilisha safari yake, hakikuwa na mafuta ya kutosha ya kukirejesha Duniani na badala yake kilibakia katika anga za juu, hii itakuwa mara ya kwanza kwa roketi isiyoongozwa kugongana na mwezi.

Roketi hiyo iliachwa katika anga za juu baada ya kukamilisha kazi ya kutuma satelaiti ya hali ya hewa katika safari ya maili milioni ikiwa ni sehemu ya mpango wa uvumbuzi wa anga za juu wa Kampuni ya SpceX ya Elon ambayo ni kampuni ya kibinafsi ambayo lengo lake kuu ni kuwawezesha binadamu kuishi katika sayari nyingine.
Screenshot_20220127-173019_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewajeruhi kwa risasi Watuhumiwa watatu wa ujambazi (Mrisho maarufu Bonge na wenzake wawili) baada ya Watuhumiwa hao kupanga njama za kufanya tukio la ujambazi January 26,2022 saa mbili usiku Mbagala Zakhem karibu na duka la Rosemary Kimario ambaye ni Wakala wa Huduma za Kifedha (Tigopesa, Airtel Money, M Pesa, NMB, DTB na CRDB )

"Watuhumiwa hao wa Ujambazi wakiwa na pikipiki walifika eneo la tukio kwenye harakati za mwisho za kutaka kuvamia na kupora pesa lakini walibaini wanafuatiliwa na Askari Polisi walifika haraka eneo hilo ndipo Majambazi hao walianza kurusha risasi ovyo, Polisi walijihami na wakawashambulia Wahalifu hao ambao walijeruhiwa na kupelekwa haraka Hospitali lakini ilibainika wamepoteza maisha"

"Watuhumiwa hao walikutwa na Bastola ikiwa na magazine moja yenye risasi 11, pia walikutwa na noti bandia za elfu kumi zenye thamani ya Tsh. 1,180,000 ambazo hutumika kuwazubaisha Mawakala kama Wateja wanaotaka huduma kisha baadaye huwapora pesa halisi kwa kuwatishia kwa Bastola"

"Tunawataka Raia Wema kuendelea kutoa taarifa za Wahalifu mapema ili Jeshi la Polisi lifanye kazi ya kuzuia matukio hayo" Muliro Jumanne Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
Screenshot_20220127-174427_Instagram.jpg
 
Luteni wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Denis Urio amesoma mawasiliano ya ujumbe mfupi wa simu kati yake na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikiwemo ya yeye kuomba na kutumiwa nauli ya Sh500,000 kwa ajili ya kuwasafirisha washtakiwa.

Shahidi huyo wa 12 wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu amesoma meseji hizo leo Alhamisi Januari 27, 2022 mbele ya Jaji Joachim Tiganga

Soma zaidi maelezo ya ushahidi wa Luteni Urio kupitia tovuti ya Mwananchi
Screenshot_20220127-174702_Instagram.jpg
 
YANGA imefanikiwa kupigana vita kubwa kumbakisha winga wao mpya Chico Ushindi aliyekaribia kusitisha dili hilo, lakini neema ikamwangukia kiungo wao wa zamani, Mukoko Tonombe ambaye amepata mshahara wa kufuru.

Katika dili la miaka miwili ambalo Mukoko amesaini na TP Mazembe mabosi wa Yanga wametumia akili kubwa kuwakamua Wakongomani hao kuhakikisha kiungo huyo anabadili akili yake kukubali dili hilo.

Mukoko sasa atakuwa akilipwa mshahara wa Dola 8000 (Sh18.4 milioni) kwa mwezi na Mazembe pesa ambayo hakuna staa yeyote wa Yanga anaweza kuivuta katika kikosi hicho, wakati akiwa Yanga alikuwa akichukua Dola 3000 (Sh7 milioni) kwa mwezi.

Mbali na pesa hiyo, Mazembe pia wamemshawishi zaidi wakimpa kiasi cha Dola 100000 (Sh230 milioni) kama ada ya usajili katika dili hilo la miaka miwili.

Hata hivyo, Yanga nao wamepiga bao na watapewa Ushindi kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu na sio miezi sita tena kama ilivyokuwa awali.
Screenshot_20220127-174907_Instagram.jpg
 
Cristiano Ronaldo : "Najua nikiamua juu ya jambo langu, hata watu wakisema siwezi, bado nitafanikisha, najiona mimi ndio mwanasoka bora wa dunia. Kama huamini kuwa wewe "Ni bora zaidi, hautakaa ufanikiwe katika kile unachoweza."
Screenshot_20220128-162953_Instagram.jpg
 
| MASTAA WATATU YANGA KUIKOSA MBAO KESHO
.
FEISAL SALUM
KHALID AUCHO
YANICK BANGALA
.
Ikumbukwe Msimu wa 2016/17 Mbao iliichapa Yanga bao 1-0 CCM Kirumba na kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho, lakini 2019 kwa mara ya kwanza Yanga ilipata ushindi dhidi ya Mbao uwanja huo ikishinda 1-0 lililofungwa na Sidney Urikhob.

Screenshot_20220128-163203_Instagram.jpg
 
Liverpool Kuikomalia Saini ya Dybala
.
Liverpool imetuma maombi kwenda Juventus ili kuipata saini ya staa wa timu hiyo na Argentina Paulo Dybala, 28, katika dirisha hili.
.
Hata hivyo hadi sasa Juventus haijajubu chochote huku mkataba wa staa huyo ukiwa unaelekea mwishoni kwani unamalizika mwisho wa msimu.
.
Hiyo inatoa ishara yakuwa na asilimia nyingi za Liverpool kwamba wanaweza kuipata huduma yake kama mchezaji huru.
.
Dybala ni miongoni mwa wachezai tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Juventus na mabosi wa timu hiyo wamejaribu kufanya mazungumzo mara kadhaa na wawakilishi wale lakini hakuna muafaka uliofikiwa.
.
Taarifa zinadai mazungumzo hayo yanakwama kwa sababu Dybala anahitaji ongezeko la mshahara kwenye mkataba mpya kwa kiasi ambacho Juve imeona haiwezi kukitoa.
Screenshot_20220128-171406_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom