
Farhan Jr
Mpira wa miguu ni zaidi ya kazi bali maisha halisi ya watu duniani kote! Huwa napenda kutumia msemo maarufu wa "One thing about football is not about football"
Lionel Messi alivyokuwa Barcelona alifunga bao kisha akavua jezi ya Barcelona na ndani alivaa jezi ya Newell Old Boys ambayo Diego Maradano alicheza
Alifanya hivyo kutuma salaam zake za pole na heshma yake kwa Maradona ambaye ni Gwiji wa soka duniani, lakini hiyo haikuwa stori kubwa
Stori ni hiyo jezi ya Newell Old Boys! Imetengenezwa na ADIDAS na Mdhamini wake ni YAMAHA, Kampuni ya vyombo vya usafiri kutoka Japan
Kumbuka: Barcelona wanadhaminiwa na NIKE ambao ni washindani na ADIDAS, isitoshe Barcelona wana udhamini wa RAKUTEN ni Kampuni ya vifaa vya umeme na mauzo mtandaoni
Kwakuwa mpira wa miguu ni Mchezo wa kiungwana na ni maisha halisi! Licha ya kwamba Messi ni kama alipiga tangazo wakati anatoa heshma yake kwa Maradona ila si klabu, si NIKE wala RAKUTEN ambao walipiga kelele
Kuna muda maisha ni muhimu zaidi kuliko pesa na biashara, kuna wakati heshma ya mpira wa miguu ni bora zaidi kuliko pesa na biashara, hii ndio maana na THE GAME IS FAIR PLAY