Kundi la mataifa tajiri duniani ya G7 leo hii lifanya mkutano wa dharura kuhusu aina mpya ya kirusi cha Covid-19 ambacho kimebadilika kabisa kilichopewa jina la Omicron, ambacho kisambaa kwa kasi.
Kirusi hicho kimelazimisha mataifa kufunga mipaka yao, huku wataalamu wakiwa katika uchunguzi wa kina wa kutaka kujua athari zake katika jitihada za kukabiliana na janga.
Mkutano huo umeitishwa na Uingereza ambayo inashikilia kiti cha mataifa hayo lakini pia ni moja kati ya mataifa ambayo idadi kubwa ya athari za kirusi hiko imegundulika.
Kirusi Omicron ambacho kwa mara ya kwanza kiligundulika Afrika Kusini kunasababisha changamoto mpya ya jitihada ya ulimwengu katika kuliangamiza janga la Covid-19. Nchi kadhaa zimeweka vizuizi kwa hofu ya kwamba uenda hali mbaya ikajirudia.
Mkali wa hizi kazi Mwimbaji Chris Brown amempigia salute Mwimbaji staa wa Nigeria Wizkid ambaye weekend hii iliyoisha siku ya Jumapili ameijaza 02 Arena London Uingereza kwa maelfu ya Mashabiki waliomiminika kumtazama.
Chris Brown hakuishia tu kufanya suprise kwenye Tamasha hilo na ku-perform bali ameileta mpaka kwenye Instagram yake kwa furaha akieleza kufurahishwa kwake na mafanikio ya Wizkid na kujivunia Wizkid pia ambae anasema wamekuwa Washkaji kwa zaidi ya miaka 10.
Show hii ya Wizkid ambayo imefanyika kwenye ukumbi wenye uwezo wa kuchukua Watu elfu ishirini imetajwa kuvunja rekodi ya ticket kumalizika ndani ya dakika 12 tu kwa mujibu wa Mtandao wa Metro Uingereza, rekodi ambayo pia imewahi kuvunjwa na Spice Girls na Bendi ya Rock ya Rolling Stones ambao ticket zao ziliisha ndani ya dakika 13.
Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita pamoja na upepo mkali vimesababisha mapaa kwenye nyumba kadhaa na Kanisa la AIC Chato kuezuliwa na Watu wanne ambao ni Waumini wa Kanisa hilo wakijeruhiwa.
Wakizungumza na @AyoTV_ katika Kata ya Minkonto Chato kijiji cha Minkonto baadhi ya Waumini na Wananchi wa eneo hilo wamesema mvua hizo zimeanza jana majira ya saa 11 jioni na kusababisha hasara ya mali inayokadiriwa kufikia shilingi milioni 10.
"Sisi tulikuwa ndani tulikuwa tunasali ghafla tukasikia mvua inanyesha huku imeambatana na upepo mkali muda huo tupo Kanisani, tukawa tunapiga muziki tukasikia radi tukazima muziki baada ya hapo tukasikia kanisa linadondoka tukiwa ndani, tunaomba serikali itusaidie" ——— Waumini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mkandarasi anayejenga chuo cha VETA Wilayani Chunya Mkoani Mbeya kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kwa muda uliokusudiwa na Wana-Chunya waanze kupata mafunzo kuanzia mwezi Februari 2022,
Ametoa agizo hilo leo Novemba 29, 2021 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya ambapo amesema malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila makao makuu ya mikoa kunajengwa Chuo kikubwa cha VETA
Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chunya kitakachogharimu shilingi bilioni 1.6 kinajengwa katika kata ya Mbugani,kinatarajiwa kuhudumia jumla ya kata 20 zenye wakazi wasiopungua 211,039.
Waziri Mkuu ameziagiza pia Halmashauri za Wilaya kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji na wawahamasishe wananchi kupanda miti na kushirikiana nao kupitia kamati zao za mazingira ili walinde vyanzo hivyo kuanzia ngazi ya kijiji kwa manufaa yao.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.