Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211126-081531_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20211126-081552_Opera%20Mini.jpg
 
• Mwili wa Askari mmoja wa Magereza Kitale Kenya umekutwa kwenye nyumba yake ya kupanga akiwa amefariki huku ikielezwa kwamba alijiua kwa kujipiga risasi kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao ikiwemo kudaiwa kodi ya nyumba ya miezi miwili.
Screenshot_20211127-044842_Instagram.jpg
 
Sio tu Serikali ya Marekani imetangaza kuzuia kuingia nchini humo Wasafiri kutoka Mataifa 8 ya Afrika ikiwemo Afrika Kusini kuanzia Jumatatu November 29 2021 kutokana na aina mpya ya kirusi cha corona kuibuka South Afrika kikitwajwa kuua Watu kwa kasi, ninayo list ya Nchi zote ambazo mpaka sasa zimetangaza zuio kwa angalau Nchi 6 za Afrika kati ya hizi 8 ambazo Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji na Malawi.

Nchi hizi 16 ni Marekani, Italy, Austria, France, Japan, Uingereza, Singapore, Netherlands, Malta, Malaysia, Morocco, Philippines, Dubai, Umoja wa Falme za kiarabu, Jordan, Guatemala na Switzerland.

Mpaka leo mchana kulikua na Wagonjwa 59 waliogunduliwa kuwa na kirusi hicho kipya kiitwacho B1.1.529 nchini Afrika Kusini, Hong Kong na Botswana.
Screenshot_20211127-045206_Instagram.jpg
 
• Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameingia kwenye uwanja wa vita kama alivyoahidi kuliongoza Jeshi la Nchi hiyo kupambana na Wapiganaji wa Kikosi cha Ukombozi cha Watu wa Tigray (TPLF) ambacho kimeungana na makundi mengine yanayoipinga Serikali katika muungano mpya unaotaka kuuuondoa utawala wa Waziri Mkuu Abiy.

Mapigano yalianza Novemba mwaka 2020 ambapo Serikali ya Ethiopia ilitangaza kufanya mashambulizi kwa Waasi wa waliokuwa Chama tawala kiitwacho The Tigray People's Liberation Front (TPLF) ambapo Chama hicho kilichokuwa na Wafuasi wengi kilitofautiana na Waziri Mkuu Abiy Ahmed juu ya mabadiliko ya kisiasa katika taifa hilo ambalo linategemea mfumo wa ushirikiano.

TPLF iliongoza Nchi kwa miaka 27 hadi mwaka 2018 kabla ya kile kinachoripotiwa kuwa ni 'kutengwa' na Serikali ya Waziri Mkuu Abiy (45) ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019 kwa kitendo chake cha kumaliza vita na Nchi jirani ya Eritrea lakini sasa kwenye vita hii na TPLF hana dalili ya kutaka kumaliza vita kwa mazungumzo na sasa vita hii imefikisha mwaka mmoja akisisitiza "Tutamzika Adui huyu kwa damu na mifupa yetu na kufanya utukufu wa Ethiopia kuwa juu tena"
Screenshot_20211127-045918_Instagram.jpg
 
Serikali ya Marekani imetangaza kuzuia kuingia nchini humo Wasafiri kutoka Mataifa 8 ya Afrika ikiwemo Afrika Kusini kuanzia Jumatatu November 29 2021 kutokana na aina mpya ya kirusi cha corona kuibuka South Afrika ambapo Nchi nyingine ni Botswana, Zimbabwe, Namibia, Lesotho, Eswatini, Msumbiji na Malawi.
Screenshot_20211127-050036_Instagram.jpg
 
Club ya Manchester United imefikia makubaliano na club ya Lokomotiv Moscow ili kumbeba Kocha Ralf Rangnick (63) ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Maendeleo ya Michezo katika club ya Lokomotiv Moscow.

Ralf ambaye aliwahi kuwa kocha wa RB Leipzig ya Ujerumani, ameshafundisha club mbalimbali kama Hannover 96, Schalke 04 na VFB Stuttgart.
Screenshot_20211127-050145_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyokaa kupitia kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, imewahukumu Washtakiwa wawili Mwapulise Mfikwa (29) na Manase Mhada (25) kunyongwa hadi kufa kutokana na kukutwa na hatia ya kumuua Eva Merikion Mgaya (28) nyumbani kwake katika kijiji cha Ihanga wilayani Njombe.

Washtakiwa wao walitekeleza mauaji hayo baada ya kuvamia nyumbani kwa Eva walipofika kwa lengo la kuiba, akisoma hukumu hiyo Jaji Filmin Matogolo amesema tukio la mauaji lilitokea May 08, 2015 baada ya wawili hao kwenda nyumbani kwa Wilfred Vitus Ng’olo ambaye ni Mume wa marehemu wakiwa na bunduki iliyotengenezwa kwa njia za kienyeji ambapo walivamia, kuiba na kunyang’anya fedha .

Washtakiwa hao pia walichukua simu ya Mume wa marehemu na kumpiga risasi Eva Merikion Mgaya kifuani kwa kutumia bunduki hiyo na kusababisha kifo chake papohapo na kisha kutoweka mpaka walipokuja kukamatwa baada ya upelelezi juu ya mauaji hayo.
Screenshot_20211127-050835_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom