

Farhan Jr
MUTSHIMBA MUGALU, HITAJI LA DUNIA YA SASA
Niliwahi kuhoji kwanini Pep Guardiola alimuhusudu sana Gabriel Jesus mbele ya lethal Striker kama Sergio Kun Aguero! Niliwahi kumshangaa Pep kwanini amkatae Etoo na kumuamini Messi
Nikaja pia kujiuliza kwanini Chris Mugalu anapata sana nafasi ndani ya Simba?? Kwanini anawaweka nje Meddie Kagere na John Bocco? Hili swali liliwahi kunisumbua sana
Awali ya yote nikaja kufanya homework yangu kwanza ya kuugawa uwanja! Kwenye nusu mbili, Nusu ya kwanza ni ZONE A chini ya mstari, huku ni BASIC FOOTBALL, mpira wa maelekezo zaidi na kujilinda
Juu ya mstari ambayo nimeiita ZONE B ni sehemu ya Creativity (Ubunifu) na Tactical Flexibility (Mnyumbuliko wa kimfumo na kimbinu) hii ndio sehemu ambayo unahitaji akili kama ya Mugalu mtu anaekupa vingi kwa pamoja
Manchester City pale Guardiola alimkataa Aguero kwakuwa licha ya kuwa ni Mfungaji bora ila haipi timu balance, hakabi, hachezeshi na hashuki! Lakini Jesus anakupa vyote na una uhakika yoyote atafunga kama yeye hatofunga
Ndipo hapo nakuja kumtazama MUGALU na ile concept ya STRIKER VS FORWARD! Dunia ya sasa inahusudu zaidi Forward kuliko Straika! Kwangu Mugalu ni Forward mzuri, Bocco na Kagere ni Masteika wazuri
Mugalu ni mzuri kwenye Link Up plays, kuwachezesha wengine na kuhakikisha nafasi zinapatikana na kubwa zaidi ni uwezo wake wa pressing hivi vinamfanya awe na vitu vya ziada kwa Mwalimu, ukiwa nae una uhakika kama sio yeye basi yoyote atafunga
Ni kawaida kwasasa kuona Heat Map ya Mugalu ni kubwa kuliko wachezaji wote ndani ya Simba kutokana na kuwa mchezoni muda wote! Na hata suala la kukosa mabao ndicho pia Gabriel Jesus pale City alilaumiwa nacho
Hii inatokana na uwezo wao mkubwa wa kukaa kwenye njia kila wakati na wanaonekana wanakosa zaidi kwakuwa wapo mchezoni muda wote na wanazijua njia muda wote
Mimi namuamini Chris Mugalu, kimfumo anailipa sana timu
View attachment 1955368