Makapuku Forum

Makapuku Forum

1632812399463.png
 
Matokeo ya mechi za ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara 2021/22.
1632812704722.png
 

Waziri Gwajima aagiza kuandaliwa kwa kadi maalum itakayotumika kufuatilia uwazi na uwajibikaji​

1632813489939.png


Serikali imeagiza kuandaliwa kwa kadi maalum {Performance Scorecard} itakayotumika kufuatilia uwazi na uwajibikaji kila ngazi inayohusika na usimamizi wa masuala ya mnyororo wa ugavi wa dawa hadi kwa mtumiaji wa mwisho {mteja}, katika ngazi ya kituo cha afya.


Agizo hilo limetolewa leo Jiji ni Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa kikao na wataalamu na wadau wa masuala ya mnyororo wa ugavi wa dawa.


Dkt. Gwajima amesema, ni kweli wataalamu na wadau hao kwa pamoja wameisaidia nchi kutengeneza miongozo mingi mbalimbali ya masuala ya usimamizi wa dawa lakini inashangaza kwamba bado wananchi wana kilio cha ukosefu wa dawa.

“Miongozo iliyotengenezwa inatosha kwa sasa na mifumo iliyopo inawasiliana na wataalamu wanaweza kutambua ufuatiliaji wa dawa kwenye mfumo wa dawa kuanzia ngazi ya Taifa hadi vituoni.


Ameongeza kuwa Wadau hao wameendelea kufanyia kazi na hata kuishauri Serikali kuongeza bajeti ya dawa, sasa mmeshauri pia MSD isitegemee bajeti ya vituo badala yake ipewe bajeti yake ili ijitegemee, Serikali ni sikivu na inafuatilia.

“Mmefanya vitu vingi upande wa miongozo, juzi tu mmetueleza tutumie dawa gani nchini zinazotufaa kwa mazingira yetu na ambazo zinadumu, tukazindua mwongozo wa matibabu.” amewaeleza wataalamu hao.


“Ipo pia miongozo mingine mbalimbali ukiwamo ule wa kupima viashiria vya utendaji kazi katika mfumo wa ugavi na ule wa kufuatilia mauzo ya dawa na fedha zitokanazo na mapato hayo {faida} zitumikaje.Mmefanya kazi nzuri”.


Dkt.Gwajima aliendelea kusema kuwa Serikali haina shida na hilo,kwani wameshashafanya vikao mbalimbali na wakati wote, fedha nyingi zimekuwa zikitumika kuboresha huduma za afya.

“Lakini pamoja na haya yote yaliyofanyika, bado tuna changamoto ambazo na ninyi ni mashahidi, bado wananchi wanalalamika hamna dawa. Tulienda Halmashauri ya Same, nikaingia ‘stoo’ ya dawa nikaziona zipo, nikaenda kwenye kikao, kuongea na wananchi, wakasema hatupati dawa.

“Sasa unahusianisha vipi, {tunasema} dawa muhimu zipo asilimia 95, wananchi wanasema hawapati dawa, hapa ndipo kwenye mtihani, miongozo tumeitengeneza, lakini wananchi wanasema hamna dawa, wakati huo huo kuna kituo A dawa zinaharibika na huku kituo B kina uhitaji. Tunafanyaje?,” amehoji.
Dk. Gwajima amesema Serikali inazidi kufanya mabadiliko makubwa ili kuimarisha mifumo yake ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ikiwamo ujenzi wa viwanda mbalimbali.

“Katika ngazi ya kitaifa kuna mabadiliko makubwa, Makambako, Njombe tuna kiwanda kitazalisha dawa aina mbalimbali, tunaanza na gloves, vidonge vya kunywa, maji, na ‘antibiotik’, kwa hizo aina tano tu za bidhaa tutaokoa bilioni 33,” amesema.

Ameongeza “Hivyo wananchi wanataka uwazi, ukweli na wenyewe wawe sehemu ya kuona kinachoendelea… mtengeneze ‘tracking tool’ inayoonesha {dawa} zilitoka zikafika huko, kama bidhaa zilitoka kwa mgonjwa, kuna cheti cha daktari ziwe zipo na ushahidi kwamba alipata fulani.


“Kama tulienda kununua nje ya MSD tulinunua kwa thamani ya makubaliano yaleyale au kuna mmoja wetu alipotoka akaenda kununua nje ya makubaliano iwe kwenye kadi maalum ya ufuatiliaji.

“Mniambie kama mtu alienda kununua nje ya MSD, kuna utaratibu au anaelekeza vinginevyo naye aingie kwenye ‘perfomance score card’ kwamba hakuwajibika, kamati ya dawa nayo ifanye kazi yake, tuone.


Ameongeza “Bidhaa zinapitwa na wakati tujue, asilimia ngapi inapitwa na wakati, tunakuwaje na bidhaa zilizoisha muda na wadau wapo, mahitaji yapo, maana yake ufuatiliaji na tathmini hapa hatujawekeza vizuri pamoja na miongozo yote tuliyonayo.


“Kuna watu wanawaelekeza wagonjwa kwenye maduka kule, kumbe ni ya akina Gwajima, lazima ioneshwe kwenye ‘perfomance score card’ tujue wangapi amewaelekeza kule, TAMISEMI nao wapo hapa waelewe maana wana vituo zaidi ya asilimia 70 tunaenda kwenye ‘perfomance score card’ kama ilivyo kwenye ajenda ya lishe na malaria.” amesisitiza.


Naye,Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi amesema kikao hicho ni matokeo ya kikao cha awali ambacho, kiliainisha maeneo 16 ya mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya ambayo yalionesha thamani na upotevu wa fedha uliotokea.

Tanzania ina viwanda vipya zaidi ya 18, vingi vipo katika hatua za majaribio kwenye uzalishaji wa bidhaa na bado kuna wawekezaji wengi wanaokuja nchini kuwekeza.
Akitolea mfano amesema katika Mkoani wa Pwani kipo kiwanda cha majitiba {drip} ambacho nacho tayari kimeanza kufanya majaribio na kwamba mapema kesho Waziri Gwajima anatarajiwa kuzindua kiwanda cha barakoa kilichosimikwa huko Kigamboni.

“Kwa hiyo viwanda vipo mbalimbali lengo letu kufikia mwaka 2030 Tanzania inakusudia kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha dawa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi kuwa zinatengenezwa ndani ya nchi, kutoka asilimia 88 hadi 50.


“Kwa kasi ya Serikali ya awamu ya sita, {Tanzania} itaweza kufikia lengo hilo la kuzalisha zaidi ya asilimia 50 ya dawa ndani ya nchi,” amebainisha Msasi na kusisitiza kwamba kikao hicho kitajadili kwa kina yote yaliyoagizwa na Waziri Gwajima.
 

Korea Kaskazini yarusha kombora kwenye Bahari ya Mashariki​

1632813661121.png

Jeshi la Korea Kusini limesema Korea Kaskazini imerusha kombora moja kuelekea katika Bahari ya Mashariki, huku Korea Kaskazini ikisema hakuna mtu anayeweza kuinyima nchi hiyo haki yake ya kujilinda.​


Wakuu wa vikosi vya jeshi vya Korea Kusini pamoja na wizara ya ulinzi ya Japan, wamesema Jumanne kuwa kombora hilo la masafa mafupi limerushwa kutoka jimbo la kaskazini la Jagang linalopakana na China, kuelekea kwenye bahari hiyo inayojulikana pia kama Bahari ya Japan.

Tukio hilo limefanyika siku chache baada ya Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, ambaye ana ushawishi mkubwa, kutangaza kuwa nchi hiyo iko tayari kurudi kwenye meza ya mazungumzo. Hata hivyo, Jong amesema ili hilo kufikiwa inawapasa kuhakikisha kuna hali ya kuheshimiana na kuachana na mitazamo ya kudhaniana vibaya.

Katika siku za hivi karibuni, Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in alirudia wito wake wa muda mrefu kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutaka kuwepo kwa azimio la kumalizika vita vya Korea hizo mbili kama njia ya kurejesha amani. Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo kadhaa vya kimataifa kutokana na mipango yake iliyopigwa marufuku ya kutengeneza silaha za nyuklia na makombora.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini, Boo Seung-chan amesema wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa leo na Korea Kaskazini, katika wakati ambao ni muhimu sana kuleta utulivu kwenye Rasi ya Korea.

Tangazo la kurushwa kombora hilo limetolewa saa chache kabla ya Balozi wa Korea Kaskazini kwenye Umoja wa Mataifa, Kim Song kuitaka Marekani kuachana na "sera yake ya uhasama" kuelekea nchi hiyo.

Akihutubia jana katika Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, Song amesema hakuna mtu anayeweza kuinyima nchi yake haki ya kujilinda, kutengeneza, kumiliki na kufanya majaribio ya mifumo yake ya silaha ambayo ni sawa na ile ya Korea Kusini pamoja na mshirika wake Marekani.

''Kwa kuzingatia kwamba ushirikiano wa kijeshi wa Korea Kusini na Marekani unaongeza kitisho kwa Korea Kaskazini, hakuna mtu anayeweza kutunyima haki ya kujilinda. Tunatengeneza mifumo yetu ya ulinzi kwa lengo la kujilinda na kwa usalama na amani ya nchi yetu. Kwa kuzingatia kwamba ushirikiano wa kijeshi wa Korea Kusini na Marekani unaongeza kitisho kwa Korea Kaskazini, hakuna mtu anayeweza kutunyima haki ya kujilinda,'' alifafanua Song.

Song amesema ana uhakika kwamba matarajio mazuri yatafunguliwa kwenye uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini na Korea Kusini, iwapo Marekani itajizuia kuitisha nchi hiyo.

Kwa miaka mingi Korea Kaskazini imekuwa ikitengeneza makombora yenye uwezo sio tu ya kuipiga Korea Kusini na Japan, lakini pia ina vichwa vya nyuklia vya masafa marefu yanayoweza kufika hadi Marekani. Kulingana na takwimu za shirika la Marekani linalohusika na udhibiti wa silaha, kuanzia mwezi Agosti mwaka 2020, Korea Kaskazini ilikuwa na vichwa vya makombora ya nyuklia 30 hadi 40.

Wakati huo huo Marekani imelaani vikali jaribio la kufyatua kombora lililofaywa na Korea Kaskazini, ambalo linasababisha kitisho kwa jirani zake na jumuia ya kimataifa. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeitaka nchi hiyo kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya kuachana na matumizi ya silaha za nyuklia.
 
1632814927527.png


Tunazitaka alama tatu za Biashara​


Timu yetu leo itashuka katika Uwanja wa Karume mkoani Mara saa 10 jioni kucheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Biashara United.
Katika mchezo wa leo tunahitaji kupata alama tatu muhimu ili kurudisha imani kwa mashabiki wetu na kupunguza presha kwa wachezaji hasa baada ya kupoteza mechi ya Ngao ya Jamii Jumapili iliyopita.
Kuelekea mchezo wa leo Kocha Msaidizi Seleman Matola ameweka wazi kuwa utakuwa mgumu kutokana na uimara wa wapinzani hasa wanapokuwa nyumbani ingawa tumejipanga kuwakabili kwa hali yoyote.
Matola amewataka mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa hamasa wachezaji huku akiahidi kupambana hadi mwisho kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu ugenini.
“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na lengo letu ni moja kushinda ili kuanza ligi vizuri kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi,” amesema Matola.
TAARIFA YA KIKOSI
Kikosi kimewasili hapa mkoani Mara jana kikitokea jijini Mwanza kikiwa na wachezaji 23 ambao wote wapo tayari kwa mchezo wa leo.
KANOUTE, ONYANGO, MKUDE KUKOSEKANA
Nyota wetu Sadio Kanoute na Joash Onyango hawakusafiri na timu kutokana na kupata majeraha katika mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Jonas Mkude alipatwa na msiba ambapo alikwenda kushiriki mazishi ya mtoto wake mkoani Morogoro hivyo alichelewa katika maandalizi ya mchezo huku Ibrahim Ajibu na kiungo Abdulsamad Kassim wakibaki Dar es Salaam.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom