Makapuku Forum

Makapuku Forum

"Hawezi kuwa Mshikaji wangu wa kwenda kununuliana bia Bar ila atasalia kuwa mchezaji bora kuwahi kupambana nae uwanjani, Arsenal ilikuwa timu kamili sana" Roy Keane, akimzungumzia Patrick Viera
Screenshot_20210921-112308_Instagram.jpg
 
ZENGWE JANGWANI

Na @davidfelician10

Tusilale hivi hivi bila ya hii kitu

Kabla ya Michuano ya Champions league Africa kuanza, timu ziliingia Sokoni kusajili na malengo yao makubwa ilikuwa ni michuano hiyo

Naam, Ngoma nagwa, Ngoma ngumu, timu imetolewa tena hatua ya Awali kabisa

Hii watu wanamezea lakini wengine ni ngumu kumeza

Nikiangalia Return of Champions,, nashindwa kumeza mate

Nikiutazam mkataba wa Kilimanjaro na Zanzibar,, hii nayo ndo nashindwa kabisa kufungua hata macho

Tuliwatuma Sokoni wanasafiri mpaka Nchini Dr Congo,, wakatuletea Yannick Bangala, Djuma Shaban, Jesus Moloko, FISTON MAYELE

Lakini tukawatuma mpaka UGANDA kwa Khalid Aucho

Mzee wangu Kijijini kulee Kanyigo akawa ananiuliza vipi walishafika hao wachezaji?

Majibu yangu yalikuwa magumu, nimjibu vipi wakati baadhi yao hawakuwa na ITC,, daah Mzee wangu ilibidi nimzimie Simu, lakini Bahati nzuri majirani walimpa Matokeo DHIDI YA Rivers United

Walivyowawamba jumla ya Mabao mawili kwa YAI na timu kutupwa Nje ya Michuano

Na hivi Sasa Mzee yule anauliza, Je Kuna FAIDA gani sasa ya wale wachezaji kusajiliwa

Nikamjibu Kuna TPL, NGAO YA JAMII NA MAPINDUZI CUP

Nasikia simu ameivunja na hataki kusikia tena Jina la YANGA SC, DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
Screenshot_20210921-112453_Instagram.jpg
 
CONFIRMED|

Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa utaendelea kuvaa nembo yenye vivutio vya utaliiya Visit Kilimanjaro & Zanzibar kwenye jezi zao upande wa mkono wa kushoto katika mechi zao za ndani.
.
Uongozi umesema kutokana na mechi hizo zinarushwa na Azam TV hivyo upo uwezekano wa kuonekana na watu wa mataifa ya nje na ikawa kivutio kwa Watalii.
.
Tutarajie kuwaona Yanga wakitumia jezi hizo katika mechi za Ligi Kuu, Kombe la ASFC, na Mapinduzi CUP.
Screenshot_20210921-113209_Instagram.jpg
 
Kesi ya Morrison yasogezwa mbele
.
Mahakama ya usuluhisho masuala ya mpira kimataifa ‘CAS’ imesogeza mbele hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji Benard Morrison iliyokuwa itolewe leo Septemba 21, 2021.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na mwanasheria wa Yanga imesema kuwa hukumu imesogezwa mpaka Oktoba 21,2021.
Screenshot_20210921-113420_Instagram.jpg
 
KAZE YANGA
.
Wananchi wameamua kumrejesha kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo Kocha Mrundi, Cedrick Kaze.
.
Habari za awali zinaeleza kwamba anakuja kuwa msaidizi wa Nasreddine Nabi.
Screenshot_20210921-113634_Instagram.jpg
 
Farhan Jr


Ukiwatazama TP Mazembe kwa mujibu wa FOOTBALL DATA BASE, ni klabu ya tano kwa ubora barani Afrika, wakiwa na alama 1572 akizidiwa nane tu na Esperance ya Tunisia

Kuna stori kuwa TP Mazembe ameshuka sana! Well kwangu hii SIO KWELI! Mazembe anaweza asiwe kwenye ile level tunayoitaka ila hajaporomoka hivyo

Ukisema Mazembe ameshuka sana vipi Esperance kwenye points ndie alieshuka zaidi kwenye ile tano bora, akiwa ameanguka kwa alama 49, wakati Mazembe kashuka kwa 25

Tunaweza kuwa sahihi labda kwa wakati mwingine kutokana na Mazembe kulinganishwa na historia yake mwenyewe haswa ya 2010, kutwaa ubingwa Afrika na kucheza fainali Klabu bingwa duniani

Lakini bila shaka mnakumbuka niliwahi kusema kitu kwenye GRB MODEL! Growth, Results Oriented and Business! Mazembe amefanya sana biashara kupitia PRINCIPLE OF PERCENTAGE RESALE!

Kwenye model kitu cha mwisho ni biashara, Mazembe wameifanya na kitu cha kwanza baada ya kufika mwisho ni GROWTH! ni hao sasa Mazembe wanakuja tena upya, wamesajili top talents kama Tsemanga Soze kutoka AS VITA

Nadhani hii ilikuwa mechi sahihi sana hii kwa Simba na Mazembe na kila Mtu alipanga kikosi chake cha kazi, kwa kuamini ni game muhimu kwenye kufunga maandalizi! Mazembe ana game na Sanga Balende ya ligi, Simba ana ngao dhidi ya Yanga

Kule Morocco, Mazembe walifungwa na Club Mohamed, wakaenda sare na Wydad Casablanca kisha wameshinda dhidi ya Simba! Kocha akisema wazi dhidi ya miamba alikuwa anaweka watu ili apate matokeo

Nadhani ni muda wa kuwapongeza Simba sasa! Kuna scale wameifikia kimkakati! Kucheza na Mazembe, FAR Rabat tena wote wamekupa watu ni hatua! Ni hatua mpaka baadhi ya watu waliamini Simba kucheza na Mazembe ni kujitafutia mechi rahisi
Screenshot_20210921-114950_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Wakati Clatous Chama anaomba kuondoka baada ya ofa ya RS BERKANE, ni sababu zilizoeleweka vyema na Viongozi

Akaenda zake Kaskazini mwa Afrika! Lakini baada ya muda mfupi ikaja ofa nyingine ya Rally Bwalya nae kuhitajika Kaskazini mwa Afrika

Ikabidi kwanza Simba wakae kama Viongozi, kuitazama ishu ya Bwalya sio tu kwenye engo ya Kifedha pekee bali kwenye engo ya timu haswa kiufundi

Kuna Mmoja aliwaambia duniani haijawahi kutokea SMOOTH TRANSITION kama utaondoa uti wa mgongo wa timu, hapa ni lazima tuchange karata vyema

Kuna mmoja akasema kuondoka kwa Triple C maana yake ni kuwa Bwalya anaweza kupewa advanced role (kusogea juu zaidi) na kucheza kama ambavyo Triple alikuwa anacheza haswa kwenye Playmaking

Kuna kitu kipo kwenye falsafa ya Simba! Kuanzia kwa Viongozi mpaka Mashabiki nayo ni POSSESSIVE FOOTBALL, kumiliki na kucheza soka la Kibrazili, which simply means unahitaji akili hizo kwenye timu

Ni sababu hii ya kupenda mpira burudani, mpaka Omog alionekana hana maana mbele ya Masoud Djuma, ni sababu hizo Sven alikuwa anashinda lakini Mashabiki wananuna kutokana na kutocheza mpira wao wa Kitamaduni (Pira Biriyani)

Kifupi Rally Bwalya ametazamwa kwenye jicho hilo, ni sehemu muhimu kwenye Kiungo cha Simba, kuanzia touch zake, akili yake ni wazi Simba kwenye kiungo itajengwa kupitia yeye

Alipoulizwa Bwalya mwenyewe anasemaje kuhusu ofa mezani, ni wazi mtoto kutoka Zambia aliwaambia anahitaji muda nchini, anahitaji kuonesha kitu zaidi na akiamini kuna sehemu ataelekea

Simba wametumia akili, there's nothing like smooth transition ukiuza watu muhimu, kata mti panda mti
Screenshot_20210921-120058_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

MZEE HASSAN DALALI NURU KWENYE GIZA LA SIMBA 2

Tuliishia wakati inaelekea kukagua uwanja wa Bunju, akiwa anakatisha kwenye pori ghafla alikutana na chatu mkubwa sana

Huku akicheka Mzee Dalali anasema alilazimika kujibana sehemu kwa utulivu mpaka chatu akapita kuelekea kwenye mbuyu mkubwa uliopo eneo hilo, hii ni moja kati ya kumbukumbu zake za Bunju

Wakati tukiendelea kupiga stori, nikamgusia kuhusu sakata la FRIENDS OF SIMBA na FANS OF SIMBA! Ikiwa ni moja kati ya vita kubwa sana aliyopigana Mzee Dalali enzi za uongozi wake

Mzee Dalali kwanza anamkumbuka Marehemu Omari Gumbo aliekuwa Makamu wake! Huku akicheka ananiambia, alilazimika kumuita Gumbo YANGA ili kubalance upepo ilikuwa vita haswa

Sasa ngoja niwape mkasa wa kundi la FRIENDS OF SIMBA ambao wengi hivi sasa ni Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi, wapo wakina Mulamu Nghambi, Mohamed Dewji, Crescentus Magori, Marehemu Hanspope na wakina Try Again

Kuna sakata lilitokea la kadi na ikapeleka Wanachama 600 kufutiwa Uanachama wakiwemo hawa FRIENDS OF SIMBA, sakata hili lilifika mpaka mahakamani wakati huo

Ikumbukwe FRIENDS OF SIMBA walikuwa Wafadhili na ndio wanasajili wachezaji, kufutiwa Uanachama kulipelekea Simba kuyumba sana kiuchumi, Mzee Dalali kupitia ujanja wake akafanya kitu

Kupitia mkutano mkuu wa klabu ya Simba akawashawishi Wanachama wabadili kadi za Uanachama! Waondokane na zile za kubandika na waende na za picha, yeye alikuwa na akili yake

Alitaka watapokubali kubadili kadi basi achapishe kadi 100 za mwanzo ili awape FRIENDS OF SIMBA wawe tena Wanachama wa klabu na wawe na sifa za kuwa Viongozi

Itaendelea......

Screenshot_20210921-120537_Instagram.jpg
 
Wizara ya Afya nchini Kenya inawatafuta Watu 4,000 waliopata dozi ya kwanza ya chanjo ya Covid 19 ya AstraZeneca kwenye Kaunti ya Nandi kufuatia Watu hao kutorudi kupata dozi ya pili ya chanjo hiyo licha ya muda wao wa kupata ya pili kufika.

Wizara imesema Watu hao wamepuuzia licha ya kutumiwa meseji mara kwa mara kukumbushwa, Watu 28,600 wamechanjwa kikamilifu chanjo zote mbili Katika Kaunti hiyo ya Nandi huku wakisema walisikia zina madhara ikiwemo damu kuganda lakini hakuna yeyote aliepatwa na madhara hayo miongoni mwao.
Screenshot_20210922-040651_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiambatana na Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Liberata Mulamula leo tarehe 21 Septemba, 2021 wameshiriki katika ufunguzi wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) unaofanyika Jijini New York Marekani.
Screenshot_20210922-040949_Instagram.jpg
Screenshot_20210922-041011_Instagram.jpg
 
Mwili wa Mtoto aitwae Talia Essau Moshi mwenye umri wa miaka minne ambaye anadaiwa kufariki kutokana na kupigwa na Msichaan wa kazi za ndani ( House Girl) katika kata ya Moshono jijini Arusha, umeagwa leo na kusafirishwa kuelekea Marangu Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.

Msichana huyo wa kazi ambae tayari Polisi wanamshikilia ana umri wa miaka 13 ambapo siku ya tukio Mama wa Marehemu amesema alipigiwa simu na Msichana huyo na kuambiwa Mtoto anaumwa ambapo alipofika nyumbani alimkuta Mtoto ameshafariki huku majibu ya Hospitali baadae yakieleza kwamba chanzo cha kifo ni Mtoto kupigwa na kuachiwa majeraha mbalimbali ikiwemo kichwani.

“"Nilipigiwa simu na Msichana wa kazi akaniambia Mtoto wangu anaumwa, anaharisha.... nikamuuliza sasa hivi anaendeleaje? akaniambia nimempa dawa amelala, nikamwambia akiamka unipe niongee nae lakini zikapita kama dakika 10 akanipigia tena”

“Akaniambia Dada leo usichelewe amezidiwa, ndio nikawahi kuja huku nikakuta Mtoto wangu ameshafariki tayari amekua wa baridi, Majirani wakampeleka Hospitali ile kukaguliwa wakaambiwa ana majeraha yaliyovimbia damu kuanzia kichwani, mwilini wakasema ndio kitu kilichosababisha kifo chake” ——— asema Janeth Temba, Mama wa Marehemu. RIPTalia
Screenshot_20210922-041521_Instagram.jpg
 
Club ya Simba SC imeingia mkataba wa udhamini wa miaka miwili na Emirates ACP wenye thamani ya Tsh milioni 300, nje ya pesa hiyo pia Emirates watakuwa wanatoa tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi kwenye Timu ya Simba katika kipindi chote cha miaka miwili.
Screenshot_20210922-041640_Instagram.jpg
Screenshot_20210922-041702_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA

Wanaume Nchini Saudi Arabia kisheria hawaruhusiwi kuuza madukani kwao nguo za ndani za kike, sheria ambayo ilianzishwa mwaka 2012———> “ Wanawake wanakosa kujiamini na wanaishiwa pozi wanapoingia kwenye maduka yanayouza nguo za ndani wakakutana na Wauzaji wa kiume" ilisema Serikali.
Screenshot_20210922-042446_Instagram.jpg
 
UNAAMBIWA

Ufilipino wamepitisha Sheria ambayo inamtaka kila Mwanafunzi anayehitimu iwe ni Shule ya Msingi, Sekondari au Chuo ahakikishe amepanda miti 10 kabla ya kukabidhiwa cheti cha kuhitimu lengo likiwa ni kuwafanya Vijana wasaidie juhudi za kutunza mazingira.

Ufilipino ina zaidi ya Wanafunzi milioni 12 wa Shule za msingi na takribani Wanafunzi milioni 5 wanaohitimu High School na Wanafunzi elfu 50 wanaohitimu Vyuoni kila mwaka, kwa sheria hii inawezesha takribani miti mipya milioni 175 ipandwe kila mwaka.
Screenshot_20210922-042551_Instagram.jpg
 
Mahakama nchini Rwanda imemkuta na hatia ya ugaidi Mwanasiasa Paul Rusesabagina na sasa Waendesha mashtaka wametaka Mwanasiasa huyu ambae ushujaa wake wa kuokoa maelfu ya Watu kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994 uliigizwa kwenye filamu ya ‘Hotel Rwanda'' ahukumiwe kifungo cha maisha jela.

Rusesabagina mwenye umri wa miaka 67 alishtakiwa kwa makosa tisa ikiwemo kuwa Mwanachama wa kundi la kigaidi, kufadhili ugaidi, mauaji na ujambazi wa kutumia silaha.

Watoto wa Rusesabagina ambae ana uraia wa Rwanda na Ubelgiji ambae amekua akiishi Marekani, amekua akiikosoa Serikali ya Rwanda huku akimuita Rais Paul Kagame dikteta wanasema Baba yao alitekwa nyara akiwa Dubai na kupelekwa kwa ndege hadi Rwanda bila yeye kufahamu.

Waziri wa Sheria wa Rwanda aliiwahi kuiambia Al-jazeera TV kwamba ‘kulikua na Mtu alikua anafanya kazi na Rusesabagina kwa muda mrefu ambae pia alikua akifanya kazi na idara yetu ya upelelezi wa makosa ya uhalifu ambae alikubali kumlaghai na malipo yalitumwa kusaidia kufanikisha kumleta hadi Rwanda lakini Serikali haikuhusika kumsafirisha”
Screenshot_20210922-042722_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom